OgwaluMapesa
JF-Expert Member
- May 24, 2008
- 10,942
- 437
MBIO za kuwania urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani zimeanza kwa vituko na vitimbwi vya kila aina.
Miongoni mwa vitimbwi hivyo ni watu kuanza kuzungumzia umri wa kuwania urais, wengine wakitaja majina yao. Kimsingi tutaona na kusikia mengi hadi wakati huo.
Nimemsikia Ridhiwani Kikwete, mtoto wa Rais Jakaya Kikwete, akitangaza timu yake ya watu 11 aliodai wanatosha kwa kiti cha urais 2015.
Si dhambi kwa Ridhiwani kumtaja au kuunga mkono mtu yeyote ambaye kwa busara na akili zake anadhani kuwa anafaa kuwa rais.
Hata hivyo, kwa busara zilizokamilika ni vijana wachache sana wanaoweza kujivika jukumu hilo zito mbele ya watu wazima wenye upeo na uzoefu mkubwa katika siasa za nchi hii.
Ridhiwani ni mbunge mchanga, hajafikisha hata miezi 10 ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tangu aliposhika wadhifa huo baada ya kifo cha Mbunge wa Chalinze, Said Bwanamdogo, kwa wabunge wa umri wake hata wale wakongwe na wazoefu ndani ya Bunge hilo, hajawahi kujiinua yeyote yule na kujivika kituko cha Ridhiwan kusimama na kuanika wale anaoona wanaenea katika kiti cha urais.
Hiki ni kioja kwani hata mwenye nafasi hiyo, Rais Kikwete hajaibuka popote pale hata kutaja sifa tu mbali ya majina ya watu anaoona wanaweza kurithi nafasi.
Hili la Ridhiwani ni la aina yake. Najiuliza rais ni nani kati ya wawili hao, Ridhiwan au Mzee Kikwete?
Maswali ni mengi kuliko majibu, ni rahisi kwa wenye fikra za mkato kuona kwamba huenda Ridhiwani amejivisha nafasi ya Msemaji wa Ikulu, wakati Ikulu ina msemaji wake!
Hawa wanaotajwa hapa ni watu wazima, wana uzoefu mkubwa katika siasa, wengine walianza shughuli za siasa kabla hata Ridhiwani kuzaliwa.
Najiuliza wanajisikiaje pale kijana Ridhiwani anaposimama hadharani, tena kwa kutumia chombo cha habari kinachoheshimika, na kuwataja kama wacheza mpira?
Siamini kama yeyote mwenye busara atafurahia jambo hili au kuchukia eti kwanini Ridhiwani hajanitaja, anune au akimbie kwa familia yake na kurukaruka kuwa "nina furaha kweli nimetajwa na Ridhiwani nafaa kugombea urais mwakani!"
Akifanya hivyo mbele ya watu wenye akili ategemee swali kwamba, kwanza ataulizwa "Ridhiwani ni nani? Ana ubia gani na urais 2015, Nani amemtuma kufanya vioja hivi?"
Binafsi nashindwa kutathmini malengo ya mbunge huyu kijana anayejivika uwezo wa kufanya kazi ambazo hata chama chake kwa sasa hakiwezi kufanya hivyo.
Kwa busara yake anaweza kuamini kabisa kabisa kuwa andiko hili ni la kumpinga au linamwonea, la hasha. Nitamke kwamba alichofanya kimepitiliza huenda kutokana na kujisahau au kuliewa na mazingira alipo.
Alichofanya Ridhiwani ni kikubwa mno kwa nafasi yake. Kwanza hekima, akili, umri na uzoefu aliona haumtoshi kutambua mtu anayefaa kuwa kupewa jukumu hilo zito, kazi namba moja ya kulitumikia taifa hili.
Huenda Ridhiwani anaona urais ni kazi ya kawaida kwa namna anavyomwona baba yake anavyoingia na kuishi naye kama baba ndani ya familia.
Ni vema akatambua kuwa kuishi na rais ndani ya familia moja kama baba haitoshi kukuwezesha kujua nani anafaa kuwa rais.
Rais na baba ni vitu viwili tofauti, na kuzaliwa na baba rais haitoshi kumwezesha kijana mdogo kama Ridhiwani kusimama mbele ya Watanzania na kuwatajia majina ya wanaofaa kuwa marais.
Kwanza, ni kuwadhalilisha hata wale aliowataja, naamini wenye busara waliotajwa kamwe hawawezi kufurahia hilo.
Kujitambua umri, nafasi, hata akili yako ndani ya jamii inayoitwa nchi au taifa, ni jambo muhimu sana.
Naamini Ridhiwan hajitambui kioja alichofanya kimepitiliza. Kuna watu wengi wenye hekima , uzofu, umri wa kutosha wanaoheshimika sana ndani ya jamii.
Kwa busara hata kama Ridhiwani kwa mtazamo wake au katika chanzo chochote alipata majina hayo kuwa ndio wanaoenea nafsi ya urais mwaka 2015, asingetamka yeye angetafuta mtu mwenye sifa za kuyaanika hadharani.
Leo Ridhiwani anapokuwa na ujasiri huu wa kupitiliza chama chake kipo kimya, maelfu ya wazoefu wenye busara na wakongwe wapo kimya katika hili, hata kama wanalijua lakini hawawezi kusimama na kuropoka.
Wapo wengi ambao leo hata wangesimama wakasema kama alivyosema Ridhiwani ingekuwa stahili yao hata kama wangepingana mawazo yao na umma.
Tulitegemea haya yasemwe na wazee wetu Ali Hassan Mwinyi, John Malecela, Cleopa Msuya, Pius Msekwa, Balozi Job Lusinde, Mzee Jaji Joseph Warioba, Mzee Barnabas Samatta, Mzee Augustino Ramadhan, Mzee Ndejembi, na wengineo.
Sina nia ya kumlaumu Ridhiwani, kwa hatua hii bali napenda kumshauri kwamba, kama ni siasa anazianza kwa mguu mbaya. Hekima ni pamoja na kukaa kimya hata kwa yale unayoyajua sana.
Wote ni mashahidi wa namna Rais Kikwete alivyokuwa mnyenyekevu, alijitambua mbele ya watu wanaomzidi, akafanya yale yanayostahiki kufanywa mbele yao hata kama hayakumpendeza.
Sikuwahi kusikia wala kusoma popote panapoonesha kuwa Rais Kikwete aliwahi kusimama na kudirikia kuwatajia Watanzania nani anafaa kuwa rais wa, pamoja na kwamba maisha yake yote alilelewa na kukulia katika siasa akiwa karibu kabisa na viongozi wakuu wa taifa.
Unyenyekevu huo ndio ufunguo uliomfikisha hapa alipo. Jukumu analojivika Ridhiwani hivi sasa litawafanya Watanzania wamwone kituko, acha watu waseme ‘mwana wa mhunzi asiposana hufukuta', kuwa na kiasi usipitilize.
Chanzo: Tanzania Daima