Ridhwan amtukana baba yake

Kudos Ridhwan! Ridhawan kama matanzania yeyote anahaki ya kutoa mawazo yake hata kama yatakingana na Mwenyekit wake wa Chama. Tusimhukumu Ridhwan kama mtoto wa Kikwete bali kama Mwanachama wa CCM na ikaotekea kuwa Baba yake ni mwenyekiti wa Chama. Sijasoma yote aliyoyasema lakini hayo machache yaliyowekwa hapo nasifu ukomavu wa huyu kijana. Binafsi, naona Ridhwan ameweka wazi kuwa CCM siyo chama cha familia kwamba akisema basi anauharibiua mradi wa familia. Aliyoyasema Ridhwani ndiyo malalamiko ya Wa-Tanzania wengi kushu hatima ya ya CCM na uongozi wa nchi kwa ujumla. Kwamba CCM inahitaji mabadiliko makubwa ni ukweli usiopingika. Hiki si chama kilichokuwa na muelekeo na mtazamo kuhusu maendeleo ya Tanzania na Wa-Tanzania. Nyerere katika ubinaadamu wake alijitahidi kuishi yale aliyoyafundisha lakini si CCM ya leo. Kikubwa kwa Ridhwani ni kuwasaidia vijana wenzake ndani ya CCM ambao ni uzao wa hii CCM mbovu waweze kuelewa kuwa nchi haijengwi, kuendeshwa kwa majungu, unafiki, uongo, fitna, ufisadi, uswahiba, ufadhilina, uwizi, utapeli na sifa nyingine nyingi ambazo ndiyo zimekuwa sura ya CCM ya sasa.

Kuhusu serikali, alilolisema Ridhwani ni ukweli uliowazi hauhitaji miwani kuona. Serikali imejaa watu wasiotenda kazi ama kwa vile hawana uwezo ama kwa vile hawana wakuwafuatilia, ama uwajibikaji mdogo. Kwamba wengi waliomo serikalini wanadumu kwa uongo, majungu, fitina, ufisadi, na ufadhilina si uowong wala kumtukana Rais ama Baba yake. Huu ni ukweli usiofichika. Tumekua tunawapigia kelele wanasiasa lakini adui mkubwa wa Mtanzania ni mtumishi wa umma ambaye yeye haoni kwanini awajibike kwa umma bali waliomteuwa. Kikwete amerithi watendaji wengi wabovu na yeye akaongeza wabovu wake wengine na hao ndiyo wanaomsumbua na kumuangusha. Lakini Kikwete amewapataje watendaji hao wabovu? na ni kwa vipi watendaji wabovu ndiyo wamepenyeza kwenye utumishi wa umma? Jibu liko kwenye utaratibu wa uteuzi ambao hauna uwazi, umetawaliwa na ukabila/udini; matabaka, uwenzetu, usehemu-kusini, kaskazini etc. Rais huteuwa watu kutokana na ushauri wa watendaji wakuu- hawandiyo wanapendekeza na kwa kadri mambo yalivyo wanapendekeza watu wanaowajua lakini lawama inakwenda kwa Rais. Ndiyo maana Ridhwani akitaka Tanzania ibadilike ili hata yeye asijeakatengwa na watawala wajao kwa ajili ya chuki na baba yake, ashinikize tupate katiba mpya na endelevu. Huu ubovu wote utapungua kawa kiasi kikubwa. Salaam zangu kwa Ridhwani ni kuwa wewe na ndugu zako mtapata shida sana Rais akiondoka bila kubadilisha hii katiba. Utaratibu wa Kutesa kwa zamu Tanzania ndiyo falsafa ya watawala wa sasa. wat wata kuhukumu na marafiki na wapiga debe kukukimbia kipindi tuu Rais Kikwete atakapoondoka. Bahati mbaya wewe na jamaa yako mtapata shida sana kwasababu pamoja na mapungufu yake Rais Kikwete ameachia mabadiliko yaliyotingisha misingi na mamlaka ya matajiri na wababe wa kisiasa wa-Tanzania. Hawa hawatawaachieni. Watu waliopoteza uwaziri, ukatibu mkuu na ulaji uliowazi nk watahakikisha jamii ya Kikwete haiendi popote. Lakini katiba mpya endelevu, itawalinda jamii ya Kikwete sasa na vizazi vijavyo na hata jamii za wale walioathirika na mabadiliko aliyoyaruhusu Rais Kikwete. Ridhwani akitaka kugombea urais atahukumiwa kama mtanzania mwingine yeyote na siyo kwa dhambi ya kufikirika ya Baba yake ama Mama yake. Tuliona huko nyuma jinsi Makamba alivyotaka kumkomoa Nnape Mnauye lakini akaokolewa na Rais Kikwete. Bahati mbaya labda huko tuendako kwa katiba hii Ridhwani hata kuwa na mtu wa kumuokoa. Tudai katika mpya endelevu ili maisha ya Ridhwani yasitegemee kuokolewa na mtu ila sheria na taratibu.
 
Tubandikie tuisome tuweze kujadili


Ridhiwani: Viongozi
CCM hawawajibiki

*Asema tatizo lao ni kukwepa lawama
*Atamani CCM ya Mwalimu Nyerere
*Amsifu Mzee Msekwa kwa ukomavu
*Azungumzia sakata la malipo Dowans

Na John Daniel

MIEZI michache baada kumalizika Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka jana, Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bw. Ridhiwani Kikwete, amesema hali ndani ya chama hicho si shwari kutokana na viongozi wake kushindwa kutimiza wajibu wao kwa kukwepa lawama.

Akizungumza na gazeti hili wiki hii katika mahojiano maalumu Bw. Ridhiwani ambaye pia ni mtoto wa Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete alitaja mambo mengine yanayotishia mustakabali wachama hicho kuwa ni ubinafsi na kushuka kwa nidhamu ndani ya chama.

Alisema kutoka na hali ilivyo sasa ndani ya chama hicho anatamani CCM ingekuwa ile aliyoiacha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.

"Katika kampeni za mwaka jana nilijifunza mambo mengi mazuri, lakini kikubwa zaidi ni kwamba chama (CCM) kinahitajia mabadiliko makubwa, nawaomba sana viongozi watusaidie wanapeleka wapi nchi? Watusaidie sisi vijana,"alisema Bw. Kikwete.

Aliendelea,"Mfano rahisi wakati tunaanza kazi ya kuzunguka nchi nzima, yalikuwa ni maamuzi ya UVCCM na tulikuwa na makundi manne moja likiongozwa na Makamu Mwenyekiti, Beno Malisa, Nyingine Katibu Mkuu Martin Shigela na nyingine Bw. Mfaume.

Lakini baadaye yalianza maneno mara ooh! chama kimebinafsishwa, hakuna hata kiongozi aliyesimama kutoa ufafanuzi huo wa kweli, matokeo yake wanachi wakajenga dhana mbaya, sasa hii tunaelekea wapi? Alihoji.

Alisema kutokana na hilo alijifunza kwamba viongozi wa CCM wanakwepa majukumu yao na wanaogopa aidha kulaumiwa kwa kusema ukweli.

Alitaja jambo la pili alilojifunza kuwa ni viongozi wengi kushindwa kueleza mazuri yaliyofanywa na serikali katika kipindi cha miaka mitano hivyo kuwafanya wananchi kuelewa kwa usahihi matunda ya utawala.

"Mfano barabara nyingi zimetengenezwa, mikopo imetolewa, ruzuku ya mbolea na zana mbalimbali za kilimo pamoja na mbegu bora zimetolewa kwa fedha nyingi lakini vijana wamekaa vijiweni wanasema hawana ajira.

Kilichotakiwa ni viongozi kuwaelimisha kuwa serikali imefanya hayo ili sasa wao wenyewe sasa waongeze uzalishaji na kujiajiri, kama mtu alikuwa akizalisha tani moja na kuuza kwa bei ya chini sasa azalishe tani 10 na kusafirisha na kuuza kwa bei ya juu maana miundombinu imeimarishwa,"alisema .

Alisema kutokana na viongozi kushindwa kuwaelimisha wananchi mambo yaliyofanywa na serikali na kutoa mwanga wa jinsi wanavyoweza kujinasua katika umasikini, vijana wengi wamebaki na wimbo wa kukosa ajira.

Alisema amesikitishwa na kitendo cha baadhi ya viongozi kugongana kauli katika tukio la maandamano yaliyozuiliwa Arusha huku akimwagia sifa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Bw. Pius Msekwa kwamba majibu yake ndiyo yaliyoonesha ukomavu wa uongozi katika suala hilo.

"Mimi ni kijana niliyekulia ndani ya CCM, nimeanza kushiriki mambo ya chama nikiwa shule ya msingi kama chipukizi, mtu asije akadhani nimeanza jana wala leo.

"Siku zote CCM inatoa kauli kupitia vikao, Mzee Msekwa peke yake ndiye aliyejibu vizuri kuhusu sakata la Arusha kuwa 'tusubiri kikao kitatoa kauli' wengine walitoa kauli za ajabu ajabu huku wakipingana wao kwa wao, natamani sana CCM aliyoacha Mwalimu Nyerere, kwani wakati huo kila kitu kilisemwa kupitia vikao,"alisema

Alitaja changamoto nyingine aliyojifunza katika uchaguzi wa mwaka jana kuwa ni wagombea kushindwa kuvunja makundi yao na kuyahamishia kujenga uadui ndani ya chama.

"Katika maeneo yote tulioshindwa mfano Mwanza, Arusha mjini, Iringa Mjini,Maswa na maeneo mengine CCM ndio ina wanachama wengi zaidi, kilichotokea ni mgawanyiko ndani ya chama,maeneo mengine tulikuta Kamati za siasa zenyewe zimegawanyika.

"Maeneo mengine tuliambiwa kuwa waliochaguliwa ni chaguo la viongozi wa wilaya si wanachama, hali kama hii ni hatari kwa chama, mimi kama kijana nasema tunahitaji mabadiliko makubwa, "alisema.

Alisema angependa kuundwa kikosi maalum cha uchunguzi ambacho kitapita kila eneo kutathmini hali halisi ya wanaoomba kuteuliwa kugombea ili kuhakikisha kila anayeteuliwa ndiye changuo la wananchi.

"Uchunguzi wetu kama UVCCM na hata mimi mwenyewe unaonesha wazi kuwa Watanzania wanaipenda sana CCM, tatizo ni mabadiliko tu,"alisema na kuongeza.

"Mimi tangu nizaliwe sijaona CCM ikitikiswa kama kipindi hiki, ni lazima tukae chini tujiulize tunakwenda wapi, dira na malengo ya chama chochote ni kuongoza, ni lazima tukubali kubadilika,"alisema

Alisema chanzo cha matatizo mengi ni ubinafsi ndani ya viongozi badala ya kufikiria kwanza wananchi.

Alisema licha ya Serikali ya Awamu ya Nne kujitahidi kuboresha maisha ya wananchi wake bado kunahitajika juhudi kubwa za kuelimisha wananchi kuboresha makazi yao kwa kutumia fursa zilizopo.

Bw. Ridhiwani ambaye aliweka wazi kutotaka cheo chochote kikubwa ndani ya chama hicho au serikali kwa maelezo kuwa anapenda kujifunza, alisema vijana wengi wa kitanzania wanahitaji kubadilika kifikra ili kuondokana na umasikini.

Alisema hata serikali kuu ikitoa matrekta madogo (power tillers) kwa ajili ya wakulima iwapo vijana hawatatambua kuwa hiyo ni fursa ya kujiendeleza bado umasikini utaendelea.

Kuhuusu malipo ya sh. bilioni 94 kwa Kampuni ya Dowans, alisema yeye kama mwanasheria anawaomba viongozi kuacha kufanya suala hilo ajenda ya kisiasa, badala yake waisaidie serikali kulimaliza.

"Sisi wanasheria taratibu zetu zinaanza baada ya mahakama kutamka hukumu, sasa katika hili serikali inapaswa kuangalia nafasi yake kama ni kukata rufaa au kulipa, lakini si watu kulifanya la kisiasa,"alisema.

Hata hivyo alisema hatua yoyote ya serikali inaweza kuanza baada ya Dowans kukazia hukumu hiyo Mahakama Kuu ya Tanzania.
 
Ridhiwani ni mnafiki.
Kama sio mnafiki kwa nini yeye binafsi haishi maisha ya hayati Mwalimu Nyerere?
kwanini ana mali nyingi kuliko mapato yake halali?
Aache unafiki na arudi kwa baba yake akamuombe msamaha.
Kamwe Nyoka hawezi kuzaa njiwa.
Kikwete ni Mwizi na ridhwani pia ni mwizi

Hapo wanena! Kama watu wanayoyasema ni ya kweli kuhusu mali anazomiliki huyu dogo! lazima atakua mwizi akimfuata kwa karibu white hair!
 
Hii habari ilikuwa kwenye gazeti la majira gazeti huru la kila siku majira jumapili,ni kweli kijana anatamani ccm ya nyerere ambayo kila kitu kilikuwa kinajadiliwa kwenye vikao, jambo ambalo naliiunga mkono,chukua majira ya jana utaiona hii habari
 
Ridhiwani ni mnafiki.
Kama sio mnafiki kwa nini yeye binafsi haishi maisha ya hayati Mwalimu Nyerere?
kwanini ana mali nyingi kuliko mapato yake halali?
Aache unafiki na arudi kwa baba yake akamuombe msamaha.
Kamwe Nyoka hawezi kuzaa njiwa.
Kikwete ni Mwizi na ridhwani pia ni mwizi
Si kweli we unaushahidi yakwamba ana mali nyingi?au ni hizi porojo za mtaani! na hili ameliongelea kwamba mtu anatunga kitu, kwa kuogopana hakuna anaye mjibu mfano kipindi cha kampeni watu walisema chama kimetelekezwa kwa familia kitu ambacho si kweli watu waligawana majukumu nani aende wapi na akafenye nini,lkn tuhuma zilipo tolewa hakuna aliye jibu ikaonekana ni kweli,
 
Back
Top Bottom