Ridhwan amtukana baba yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ridhwan amtukana baba yake

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by KICHAKA, Jan 24, 2011.

 1. KICHAKA

  KICHAKA Member

  #1
  Jan 24, 2011
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 58
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Katika hali ya kutapatapa ama kutojua la kufanya kama sio kukosa makuzi mema gazeti la Majira Jumapili limechapisha mahojiano ya Ridhwani Kikwete akichambua serikali ya Baba yake na Chama chao. Katika mahojiano hayo, anasema bora CCM ya Mwalimu Nyerere huku pia akitoa vijembe kwa uongozi mzima wa CCM toka ngazi ya baba yake hadi chini na akifafanua pia kuwa serikali imejaa watu wasiotenda bali waongo na wasiokubali kusema ukweli. Wadau tafuteni habari hiyo muisome na mtafakari namna nchi ilipo kutokana na kuwa na vwatu visivyo kuwa na uwezo hata wa kuendesha familia.
   
 2. W

  We can JF-Expert Member

  #2
  Jan 24, 2011
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 681
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Who know the other side of the coin and who cares anyway!
   
 3. c

  carefree JF-Expert Member

  #3
  Jan 24, 2011
  Joined: Dec 19, 2010
  Messages: 265
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Tubandikie tuisome tuweze kujadili
   
 4. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #4
  Jan 24, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Alichokisema ni cha kweli kabisa na hata hasingesema, ukweli ungebaki pale pale(The truth shall prevail forever)
   
 5. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #5
  Jan 24, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  The CCM hour of RECKONING and realistic reality checks is here and now, out of sight of our honoured eyes!!

  Yes, Tanzanians, today, are by now a lot keener than any old-school politician around would imagine.
   
 6. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #6
  Jan 24, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Mdau asante kwa hii post ila ili kuepuka kumjadili mtu (Ridhiwan) naomba utuwekee copy ya hiyo habari hapa ili tujadili hoja.
   
 7. masharubu

  masharubu Senior Member

  #7
  Jan 24, 2011
  Joined: May 5, 2010
  Messages: 156
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Waswahili husema mchelea mwana kulia atalia yeye,kazi anayo jk
   
 8. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #8
  Jan 24, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  leo hii ridhiwani wakumgeuka babake kweli kazi ipo
   
 9. N

  Nasolwa JF-Expert Member

  #9
  Jan 24, 2011
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,830
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Hongera sana Ridhiwan kwa kusema ukweli juu ya ubabaishaji wa serikali ya baba yako. Huo ndio ukweli baba yako kikwete nchi imemshinda mshauri aachie ngazi
   
 10. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #10
  Jan 24, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Hii habari niliisoma kwenye gazeti ikanishangaza sana, nilijiulioza maswali mengi: kwa nini mahojiano ya RK yachukue main heading ya gazeti?, kwa nini nini azungumzie chama with such an authority?. Sijui baba yake anaposoma habari hizi anafikiria nini, natumai mathread atamjibu.
   
 11. Trustme

  Trustme JF-Expert Member

  #11
  Jan 24, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,172
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  kama kusema ukweli ni kumjeuka mtu Hata watoto wa Nyerere walimjeuka baba yao baada kuhamia upinzani ! Kwa mtazamo wangu hajalelewa vibaya , kusema ukweli siyo kulelewa vibaya hayo ndiyo malezi bora! siyo uogope kusema kwa vile ni baba! Sisi watanzania cjui tuna matatizo gani, hakuna jema kwetu, angesema viongozi CCM wanawajibika, mngesema anamfagilia baba yake! sasa kasema ukweli unasema hajalelewa vizuri!!!! Ulitaka asemeje ili uone amelelewa vizuri? kweli wewe ndiyo kichaka (ccm) kweli kweli!
   
 12. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #12
  Jan 24, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  There is a lack of sincerity kwenye dhamira yake na anajua kwamba anatuzuga. Tunamjua! Totally gimmick!
   
 13. KICHAKA

  KICHAKA Member

  #13
  Jan 24, 2011
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 58
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ridhwani: Viongozi wa CCM hawawajibiki
  *Asema tatizo ni kukwepa lawama
  *Atamani CCM ya Mwalimu Nyerere
  *Amsifu Mzee Msekwa kwa ukomavu
  *Azungumzia sakata la malipo ya Dowans

  Na John Daniel

  Miezi michache baada ya kumalizika uchaguzi mkuu Oktoba mwaka jana, Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja Wa Vijana CCM, Bw Ridhwani Kikwete, amesema hali ndani ya chama hicho si shwari kutokana na viongozi wake kushindwa kutim,iza wajibu wao kw akukwepa lawama.

  Akizungumza na gazeti hili wiki hii katika mahojiano maalum, Bw Ridhwani ambaye pia ni motto wa mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete alitaja mambo mengine yanayotishia mustakbali wa chama hicho kuwa ni ubinafsi na kushuka kwa nidhamu ndani ya chama.

  Alisema kutokana na hali ilivyo sasa ndani ya chama hicho anatamani CCM ingekuwa ile aliyoiacha Baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere. "Katika kampenmi za mwaka jana nilijifunza mambo mengi mazuri, lakini kikubwa zaidi ni kwamba chama CCM kinahitaji mabadiliko makubwa, nawaomba sana viongozi watusaidie wanapeleka wapi nchi? Watusaidie sisi vijana," alisema Bw Kikwete.

  Aliendelea; "Mfano rahisi wakati tunaanza kazi ya kuzunguka nchi nzima, yalikuwa ni mamauzi ya UVCCM na tulikuwa na makundi manne moja likiongozwa na Makamu wa UVCCM, Beno Malisa, lingine Katibu Martine Shigela na lingine bwana Mfaume. Lakini baadaye yalianza maneno oooh chama kimebinafsishwa, hakuna hata kiongozi mmoja aliyesimama kutoa ufafanuzi huo wa kweli, matokeo yake wananchi wakajenga dhana mbaya, sasa hii tunaelekea wapi?" alihoji.

  Ni ndefu na hawa jamaa hawajaweka mtandaoni nimebidi kuichapa upya na sina muda wa kuimaliza wengine saidieni
   
 14. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #14
  Jan 24, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Hee!
  Kumbe ukimwambia mtu ukweli umemtukana eeh?
   
 15. B

  Bruno David New Member

  #15
  Jan 24, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  2najua kabisa mwisho wa siku lazima watoleane macho!!!!!!!!!shame to mkwere...
   
 16. Wakumwitu

  Wakumwitu JF-Expert Member

  #16
  Jan 24, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 373
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Haya!! ukweli umesemwa. "Politically" ukitaka kujijenga kisiasa lazima uwe makini sana. Hapa anachojaribu kukifanya Ridwani ni kujipalilia aonekani yeye ni bora ndani ya wana CCM. Haya maneno anayoyasema sasa alifaa awaambie watanzania wakati wa kampeni kuwa CCM haiwajibiki. Kimtizamo hizi ni mbinu za mtu kutaka madaraka kwa kuponda wenzake wakati yeye mwenyewe yumo ndani. SIASA NI MCHEZO MCHAFU na KAMA HUWEZI hizo rafu hufiki popote. Pia ikumbukwe 2015 JK anastaafu kwa hiyo lazima aanze kujipalilia mapema ili awepo kwenye "system" siku za usoni.
   
 17. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #17
  Jan 24, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,626
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  KICHAKA nadhani unahitaji maombi sana pili unaonyesha wazi kuwa ni moja kt ya wana-CCM ambao katu hampendi kuelezwa ukweli juu ya matendo ya chama na serikali yake au si mtu constructive na unayependa drama tu.

  Kutokana na title uliyotumia ktk hii post, naomba kukuuliza yafuatayo je aliyosema Ridhiwani ni uwongo au ni kweli tupu.Je kama ni kweli, mtu anaposema ukweli ni kutukana? Au ulitegemea asifie tu kwa kuwa Baba yake ni raisi wa nchi. Mimi nakushauri kuwa mwangalifu unapowasilisha ujumbe si vuziri kukurupuka. Vile vile ningependa kukufahamisha kuwa raisi wa nchi ni taasisi na si mtu binafsi kama unavyofikiri ww. Kwa hili Ridhiwani yuko sahihi sana.
   
 18. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #18
  Jan 24, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Kichaka asante kwa jitihada.

  Ingawa anachokisema RK ni ukweli unaojulikana swali watakalojiuliza baadhi ya watu ni "nini kimetokea"????

  Gazeti la Mwanahalisi wamewahi kufungiwa kwa kusema "RK anatumika kudhoofisha uongozi wa JK" sasa sijui haya mahojiano yanaimarisha uongozi wa JK kwa kiasi gani!!!
  RK kahusika kikamilifu ktk kumbwaga Masauni (M/kiti wa UVccm) na alikuwa injinia mzuri wa mweleka wa Bashe (nzega).
  Ktk matukio haya mawili M/kiti wa CCM alihusika kuyafanikisha jambo lililoonyesha RK ana ushawishi wa kutosha kwa M/kiti wa chama who happens to be his father.

  Ningetamani atumie ushawishi huo kumfanya M/kiti wa chama asafishe safu ya uongozi wake ndani ya chama na serikali.

  Otherwise mimi naamini RK kapata publicity ya haraka sana tena on a silver platter kiasi kwamba hawezi kuhandle!

  Minyukano ndani ya CCM na iendelee tu maana madhila yetu yanatokana na wao!!!!!
   
 19. KICHAKA

  KICHAKA Member

  #19
  Jan 24, 2011
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 58
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mo-Town! Hongera sana kwa mawazo yako! Kama ningekua na muda wa kuichapa sori ile ungeona kuwa alichokisema hakina ukweli. Tatizo la CCM kwanza ni Baba yake tatizo la pili ni mama yake na la tatu ni yeye! Hawa familia wametaifisha taasisi ya serikali na chama. wamevigeuza kuwa BMW sasa mmoja katika hao anataka kuonyesha kuwa yeye ni safi ila baba ndiye mchafu? Kisha anamsifu Msekwa kuwa anatumia vikao, mbona yeye karopoka magazetini ilihali anajidai kazaliwa katika chama? Anataka CCM ya mwalimu Nyerere, je anajua kuwa Mwalimu hakutaka baba yake kuongoza baada ya kutambua uwezo wake? Mbona hajatamka kuwa kukosekana kwa Nyerere kumesababisha baba yake kuingia madarakani wakati hana uwezo? Juzi alikacha mkutano wa waandishi wa habari kutoa taarifa za UVCCM. Baada ya kuona vijana wale wamepokelewa vema katika jamii sasa anaona ni wakati wake kutafuta kutoka? Matatizo yote yaliyopo UVCCM nani hajui kuwa chanzo ni yeye? Hata kuporomoka kwa morari ya vijana nchini nani hafahamu kunachangiwa na yeye kuweka maslahi yake binafsi kwanza badala ya kuacha taasisi hiyo kufanya kazi? Nitazidi kushuka nondo hapa kama utachangia kwa busara na hekima
   
 20. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #20
  Jan 24, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,132
  Trophy Points: 280
  Ridhiwani ni mnafiki.
  Kama sio mnafiki kwa nini yeye binafsi haishi maisha ya hayati Mwalimu Nyerere?
  kwanini ana mali nyingi kuliko mapato yake halali?
  Aache unafiki na arudi kwa baba yake akamuombe msamaha.
  Kamwe Nyoka hawezi kuzaa njiwa.
  Kikwete ni Mwizi na ridhwani pia ni mwizi
   
Loading...