Heparin
JF-Expert Member
- Sep 24, 2021
- 440
- 3,211
Ridhiwani Kikwete umesema vyema kabisa, na sisi tumekuelewa. Ujumbe huu wapelekee pia mabosi wako, Samia Suluhu Hassan na Mwigulu Nchemba ambao hadi sasa wanatuona watanzania ni mazuzu, kwamba hawaelewi watu walikuwa wanalalamikia nini kiasi cha kuandamana.
Nakunukuu
"Malalamiko juu ya maadili ya viongozi yamekuwa mengi sana... Nyie wenyewe mnaona mfano maandamano yaliyotokea juzi hapa, malalamiko yalikuwepo makubwa juu ya maadili ya viongozi, au nyie hamjasikia?... "
Najua umejenga hoja hii ukitana kujinasua kwenye kashfa ya Lake Oil ambayo umekana kuhusika kwake, na umebainisha upo tayari kuhojiwa. Lakini, hii si pointi ya muhimu sana kwangu.
Mimi ninakusihi, najua wote serikalini mnajua sababu za watu kuandamana, lakini wenzio wameamua kujifanya hamnazo kwa kuamua kusingizia foreign influence, waambie pia wenzako sababu hii ili wasiwe na kisingizio tena.
Hilo la maadili ya viongozi ni moja tu kati ya mambo mengi tunayolalamikia.