Ridhiwani Kikwete: Fedha za maendeleo zinasuasua, serikali inasema Makusanyo hayajakaa vizuri

iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,437
14,927
Akihojiwa na mwandishi wa Gazeti la Mwananchi,toleo la tarehe 18/2/2017.

Ridhiwani anakiri kwamba kilio kikubwa cha wabunge ni kucheleweshwa (sema kutopelekwa) kwa fedha za maendeleo.

Anasema miradi mingi imekwama,na kwamba akiuliza serikali ni anaambiwa "MAKUSANYO HAYAJAKAA VIZURi"

Nadhani sasa ni wakati muafaka kwa serikali kutuambia hali ya makusanyo ya TRA na uwezo wa nchi kuhimili bills zake.

Hawa watu wamekuwa wakijigamba kwamba serikali ni tajiri na ina mahela mengi,huku pembeni wanawaambia wabunge kuwa hali ya makusanyo si nzuri.

Bora tuqmbiane mapema tujua kwamba mwaka huu hakuna kupanda madaraja,hakuna uhamisho,kodi zitaongezeka,na miradi ya maendeleo haitafanyika.

Zile barabara za maghorofa hakuna,badala yake inajengwa ya lusekelo,

Ni wakati wa kuambiana ukweli sasa
 
Kwani January makusanyo yalikuwaje? Trilioni ngapi?

Mh Riziwani vipi kuhusu Tanzania ya viwanda Ni hivyo Tu 52,000 alivyosema Waziri? Je milioni 50 kila kijiji inatoka lini?
 
Back
Top Bottom