tutafikatu
JF-Expert Member
- Dec 17, 2011
- 3,307
- 4,585
Huwa najiuliza mtu anapogawa vitabu shule za msingi na sekondari, huwa ni vile vya kiada na ziada? Nimejitahidi kuvitambua vitabu alivyogawa Ridhiwani jimboni kwake, sijavitambua. Vingine kama vya mapishi vile. Hongera kaka.
FRIDAY, FEBRUARY 19, 2016
MBUNGE WA CHALINZE ATOA VITABU 3438 KWA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI JIMBONI KWAKE
Mbunge wa Jimbo la Chalinze,Mh. Ridhiwani Kikwete akikabidhi vitabu 3438 vya shule za Msingi 105 na Sekondari 17 vyenye thamani ya Shilingi Milioni 68,760,000, kwa Afisa Elimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, Mkoani Pwani. Makabidhiani hayo yamefanyika mapema leo asubuhi kwenye Shule ya Sekondari ya Mdaula.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze,Mh. Ridhiwani Kikwete akizungumza mara baada ya kukabidhi vitabu hivyo. kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mdaula, Mwalimu Komba.
Mratibu wa Taasisi ya Kulea Village, Bw. Kombo (wa pili kulia) akizungumza machache wakati wa hafla ya kukabidhiwa Vitabu kwa Shule za Msingi na Sekondari, vilivyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Chalinze,Mh. Ridhiwani Kikwete (mwenye skafu shingoni).
FRIDAY, FEBRUARY 19, 2016 ~ COPYRIGHT: MICHUZI BLOG