Richmond na Dowans ni mali ya nani?

wadau kwanza niwape hongera japo kwa kufikia siku ya leo na pia naomba muungane nami tumuombe mwenyezi mungu atuoneshe mwaka 2011.

Kulikuwa kumetulia ila jambo jipya (jipya kwa nje ila ukweli ni kuukuu) linaongoza vichwa vya habari na linamgusa kila mtanzania, kupitia waandishi john daniel na suleman abeid (majira) nimeona nanyi msome alafu tupate mtazamo wenu wana jf kwani huo ni mtazamo wa walioandika, nanukuu, nawasilisha.

'mwenye dowans atajwe kabla ya kulipwa'

na waandishi wetu

sakata la malipo ya sh. Bilioni 185 kwa kampuni ya dowans iliyorithi mikoba ya kampuni hewa ya richmond imezidi kuchafua hali ya hewa baada ya wananchi kumtaka rais jakaya kikwete kumtaja hadharani mmiliki wa kampuni hiyo
kabla ya kulipwa mabilioni ya fedha za walipa kodi.

Wakizungumza na majira kwa nyakati tofauti kutoka mikoa mbalimbali, wananchi hao wamesema wanasikitishwa na kauli ya serikali kukubali kuheshimu sheria kulipa dowans fedha hizo wakati mmiliki wake hajulikani hadi sasa.

tunataka serikali, hasa rais kikwete, atuonyeshe mmiliki wa dowans, ajitokeze hadharani mbele ya vyombo vya habari tumfahamu. Haiwezekani nchi ikashindwa kesi na hewa, maana hadi leo hatujui mmiliki wa dowans ni nani.

"pia tunataka hiyo hukumu ipelekwe kwa jaji mkuu ili baadaye ilitolewe hadharani kwa vyombo vya habari tujue inasemaje,” alisema bi. Catherine maliwa wa kigogo dar es salaam.

Alisema katika historia ya taifa la tanzania haijawai kutokea nchi ikashindwa kesi na mtu asiyejulikana na kuonya viongozi wa serikali wanaohusika kutothubutu kutoa hata senti kulipa dowans bila wamikiki wake kujulikana na kujitokeza hadharani.

“jambo linalotusikitisha ni kuwa richmond ni kampuni feki na wamiliki wake hawajulikani, iweje kampuni feki ambaye mmiliki wake hajulikani kuuzwa kwa dowans, mtalipa pesa mashetani?” alihoji bi. Maliwa.

Alisema hivi sasa watanzania wamechoshwa na viongozi wazembe wanaowabebesha mzigo wajane na maskini huku wahusika wakibaki salama na kufurahia maisha ya anasa kwa jasho lao.

Alisema baada ya hatua ya rais kikwete kumtangaza mmiliki wa dowans na mwenye kampuni hiyo kujitokeza hadharani na nakala ya hukumu kukwekwa hadharani kwenye vyombo vya habari wahusika wote wachukuliwe hatua za kisheria suala la kulipa fedha hizo liwe la mwisho.

Mkoani shinyanya wananchi walisema licha ya mahakama ya kimataifa ya kusuluhisha migogoro ya kibiashara (icc) kuipa ushindi dowand, utekelezaji hauwezekani hadi mmiliki wake ajulikane kwa watanzania wote.

Walisema ni ajabu na mshangao kwa shirika la serikali kupelekwa mahakamani na mtu asiyejulikana huku baadhi ya viongozi waandamamizi wakionesha kwa haraka dalili ya kutaka kulipa adhabu hiyo kwa mtu asiyefahamika.

“umefika wakati kwa rais kikwete abebe jukumu la kuwafahamisha rasmi watanzania mmiliki halisi wa dowans, itakuwa ni miujiza na aibu kwake kulipa fedha hizo kwa mtu asiyejulikana. Watanzania hatujawa wajinga kiasi hicho, kila mara serikali imekuwa ikieleza wazi kutomfahamu mmiliki wa dowans,” alisema bw. Fredy mmassy.

Wananchi hao walihoji kauli iliyotolewa na waziri mkuu mizengo pinda kuwa serikali inaheshimu sheria na kwamba ikibidi haina ujanja zaidi ya kulipa mabilioni hayo kwa dowans.

Rais atueleze na amtaje huyo mtu, vinginevyo watanzania hatutokubali fedha hiyo ilipwe, na hata ikilipwa kwa nguvu waelewe iko siku tutaidai kwao, alisisitiza bw. Mmassy.

Wananchi hao walisema mbali na rais kikwete kumtaja mmiliki wa kampuni hiyo pia awaeleze watanzania mwakilishi wa serikali aliyeiwakilisha tanesco katika mahakama ya icc.

Walisema imefika wakati wa serikali kuweka wazi mkataba kati yake na kampuni hewa ya richmond pamoja na ule wa dowans ili kila kitu kifahamike na watanzania wajionee wenyewe ni wapi tanesco inapotiwa hatiani kabla ya fedha hizo kulipwa.

Katika hatua nyingine wananchi hao walimtaka rais kikwete kuangalia upya maamuzi ya tanesco kupandisha bei ya umeme na kuweka wazi kuwa hali hiyo haiendani na maisha yao duni na umasikini uliokithiri.

Tunaomba rais kikwete kama kweli anawathamini watanzania waliomchagua kwa moyo mmoja basi, azuie ongezeko la bei mpya za umeme, viongozi wetu wameonesha wazi kutokuwa na huruma na watu wao, wanakubali kulipa sh. Bilioni 185 na kuongeza bei ya umeme,” alisema bw. Masunga jilaba, mkazi wa kitongoji cha ndembezi mjini shinyanga.

Hawa wana haki ya kufanya hivyo kwa sababu hawatoi hata chapa moja mifukoni mwao kwa ajili ya kulipia umeme, uchungu wataupata wapi? Ni watanzania masikini wanaohangaikia hata mlo wao wa siku ndiyo watapaswa kulipa deni hilo la dowans kupitia ankara za kila mwezi za matumizi ya umeme,” alisema bw. Jilaba.

Wananchi hao walisema ongezeko la bei ya umeme kwa asilimia 18.5 ni dalili ya wazi kuwa wateja wa tanesco ndiyo wanaopaswa kuilipa dowand na kwamba hilo halihitaji mtu kuwa na elimu ya chuo kikuu kufahamu kuwa kampuni hiyo ni ya mfukoni na kuna watu wanafaidika nayo kwa njia moja au nyingine.

Katika hatua nyingine wanachi hao wamehoji kauli iliyotolewa na waziri mkuu aliyejiuzulu bw. Edward lowassa, kwamba wananchi watangulize upendo kudai katiba mpya na kumtaka atafute kwanza upendo na huruma kwa watanzania.

“najiuliza ni upendo gani anaounzungumzia, yeye anajua upendo tumeumizwa na mengi ikiwemo mikataba mibovu, kama angejua upendo nchi isingeingia katika mkataba wa aibu wa richmond wakati akiwa madarakani,” alisema bi. Maliwa.

Alisema bw. Lowassa anapaswa kuwaomba radhi watanzania kwanza ili kuonesha upendo badala ya kujifunika shuka nyeupe wakati ndani kuchafu.

Wakati huo huo serikali imeshauriwa kuangalia uwezekano wa kusitisha mikataba yote na makampuni ya uzalishaji umeme ikiwemo iptl na songas ili fedha zinazotumika kulipa capacity charge zitumike kununulia mitambo itakayomilikiwa na serikali.

Umefika wakati wa serikali kukatisha mikataba mibovu inayowakamua watanzania katika uzalishaji umeme hata kama ni kulipa fidia basi fidia ilipwe ili fedha zinazolipwa kila siku kwa makampuni hayo zielekezwe katika kununua mitambo yetu sisi wenyewe,

kwa hii watanzania tutakuwa radhi hata kama nchi itaingia gizani kwa miezi miwili mfululizo ni bora iwe hivyo, na katika kipindi hicho umeme kidogo unaozalishwa na tanesco yenyewe uelekezwe katika maeneo nyeti tu ya uzalishaji, ili mradi tu baada ya muda mfupi tuwe na mitambo yetu wenyewe,” alisema bw. Juma shukuru.

Imeandaliwa na john daniel dar na suleiman abeid, shinyanga

mkuu maombi yako usiyasimamishe tu baada ya kutajwa endelea kumuomba mungu awaondoe kabisa duniani..swala lakujulikana labda nikuabalishe ndilo linaumiza vichwa cvvyao na hata ukisikia serikali sijui italipa wanasubiri kusajiliwa kesi wazame na huyo atakae kaa mkao wa kula .....ila ukweli ni aibu kubwa na mbaya zaidi na mkulu atakuwa amevuliwa nguo zote karibu na nusu
mwaga sala mwagaaa
 
mmiliki atachakachuliwa na tutaambiwa muda si mrefu na watanzania tutaona ni sawa tu RA ,EL na mkuu JK wapo busy sijui hata JK km ameandaliwa hotuba ya kuisoma mwisho wa mwaka maana mambo yako sivyo.

Ushauri tuendelee na maombi kwa sana majibu yapo karibu tena
 
mkuu maombi yako usiyasimamishe tu baada ya kutajwa endelea kumuomba mungu awaondoe kabisa duniani..swala lakujulikana labda nikuabalishe ndilo linaumiza vichwa cvvyao na hata ukisikia serikali sijui italipa wanasubiri kusajiliwa kesi wazame na huyo atakae kaa mkao wa kula .....ila ukweli ni aibu kubwa na mbaya zaidi na mkulu atakuwa amevuliwa nguo zote karibu na nusu
mwaga sala mwagaaa

WanaJF, Watanzania Sala zisikike Mungu atazisikia Sala/Ibada,Sala/Ibada,Sala/Ibada,Sala/Ibada,Sala/Ibada,Sala/Ibada,Sala/Ibada,Sala/Ibada
Sala/IbadaSala/IbadaSala/Ibada,
 
katika hotuba ya JK jana usiku nilitegemea kabisa atafafanua suala la Dowans na hukumu tata. Lakini hilo sikulisikia. Je kuna aliyesikia akilitaja wakati akizungumzia namna ya kumaliza kero za umeme?
 
Richmond ilikuwa ya nani? Kama richmond iliasisiwa na Lowassa mbona iliendelea baada ya Lowassa kujiuzulu. Ilikuwa richmond ikawa dowans na sasa symbion. Halafu Mh. Mwakyembe aeleze ni nini walibakiza katiba ripoti yake. Kuweka hii wazi itakata mzizi wa vitna maana inaonekana richmond ililengeshwa Lowassa ili kuwaokoa wengine lakini tofauti ya utekeleza ilionekana kwenye kashfa ya Escrow kwa waliovurunda kutetewa kwa gharama kubwa. Karibu wadau kwa mjadala na mods msiunganishe hii na zingine.
 
Mbona alishamrudishia mwenye gamba lake la Richmond!? Mmiliki wa Richmond ni yule anayeishi kule Kivukoni!
 
Jamani nimejaribu kufatilia sana kwenye magazeti,TV,na hata Redioni! Lakini
bado sijafanikiwa kuwapata wamiliki halali wa iliyokuwa RICHMOND na sasa
DOWANS. Maana majina haya mawili kwa sasa yamekuwa masikioni kwenye
kila media na wanachi wote kwa ujumla. kisa? wameshinda kesi na wanatakiwa
kulipwa karibu Billion 184 kutoka kwenye pesa za kodi za watanzania. Jamani
nauliza kulikoni? Ni nani wamiliki wa kampuni hii ya Dowans? Nitashukuru kama nita
pata jibu sahihi kwa faida ya watanzania wote! Maana hizo pesa ni nyingi sana na anae
enda kulipwa hatumjui

Nawasilisha wandugu.
Richmond hafahamiki lakini Dowans alikuwa Rostam na Dowans yenyewe imeuzwa tayari tena Kwa Dola million 120 na Serikali walishawalipa dola Milion 100 , Hii dili ilipigwa kimya kimya na Rostam kwa Msaada wa Mzee Mengi ambaye alimsaidia kukwepa kodi na kuhamisha mapesa yote toka Tz kwenda Dubai na ulaya.
 
Richmond ilikuwa ya nani? Kama richmond iliasisiwa na Lowassa mbona iliendelea baada ya Lowassa kujiuzulu. Ilikuwa richmond ikawa dowans na sasa symbion. Halafu Mh. Mwakyembe aeleze ni nini walibakiza katiba ripoti yake. Kuweka hii wazi itakata mzizi wa vitna maana inaonekana richmond ililengeshwa Lowassa ili kuwaokoa wengine lakini tofauti ya utekeleza ilionekana kwenye kashfa ya Escrow kwa waliovurunda kutetewa kwa gharama kubwa. Karibu wadau kwa mjadala na mods msiunganishe hii na zingine.
Ni hivi hilo Dili lote lilikuwa la Rostam Lakini mwanzoni hakujulikana, alikuja kufahamika kuanzia Dowans kuuzwa kwa Symbion ambapo aliuza kwa dola million 120 na Serikali ikalipa fidia million 100 , pesa zote akakomba Rostam akamugawia Mengi ili amsaidie kukwepa kodi na kutunza siri.
 
Dowans inamilikiwa na JAKAYA MRISHO KIKWETE, ROSTAM AZIZ NA EDWARD LOWASA.

Dowans ilikuwa ya Rostam Lakini ilishauzwa kwa Symbion kitambo na Rostam wakagawana pesa na Mengi kimya kimya ndiyo maana Mengi hakupaza Sauti.
 
Mengi katokea wapi huko kwenye dowans?

Mengi ndiye alimsaidia Rostam kuondoka na pesa pasipo kulipa kodi, yaani badala ya kulipa kodi pesa akapewa Mengi akafanya yake na kumaliza Ugonvi wao na Rostam, na kama Mengi asingepewa mgao lazima angepakaza sana, hapo ndipo Mengi alipoingilia.
 
UKWELI KUHUSU SAKATA LA RICHMOND

Hii ni hoja ambayo kila uchao yeyote ambae atakua anampinga Edward Lowassa basi ndio funguo ya kuanzia popote atakapo simama

hii kashfa kwa Lowassa ilianza muembe Yanga na Dr. Slaa aliopo toa orodha ya kwanza ya mafisadi hadi katika magazeti na watu kukaa hadi vikao wakitaka jina la Lowassa na bahati mbaya jina la Lowassa halikuwemo wakilenga atajwe katika scandal ya DAWASCO na kizuri zaidi serikali ilishinda katika kesi ile kwa maamuzi magumu ya Lowassa mpaka akahoji katika kikao cha ndani NEC mbele ya mwenyekiti kipi nilikifanya usicho kijua? Na huu ndio muendelezo wa mashambulizi hadi katika scandal iliyoitwa Richmond. Baada ya kujiuzulu kwa -kiongozi huyu 2008 nilifuatilia sinema ile kwa umakini na nilishangazwa kuona kesi iliyofunguliwa dhidi ya Richmond na kuelezwa kuwa kampuni hii haipo na wala haijawahi kuwepo inashindaje kesi na mashauri yake -yote yaliyo funguliwa dhidi yake ?, pili inakuwaje serikali inakubali -mitambo inauzwa kwa DOWANS na baadae SYMBION kwa baraka za baraza la mawaziri?, inakuwaje mitambo hiyo inagharimu pesa za wamarekani ambao tunaamini wapo makini -kwa waziri wao wa mambo ya nje H. Clinton na Rais wa Dunia- Barack Obama wanaikagua kwa ziara ya gharama za fedha za Wamarekani?. Jibu hapa vita dhidi yake na mipango ilikwama na wanaposema fisadi alifisadi nini ? au ndio trolling mitandaoni dhidi yake?.
 
hii kashfa kwa Lowassa ilianza muembe Yanga na Dr. Slaa aliopo toa orodha ya kwanza ya mafisadi hadi katika magazeti na watu kukaa hadi vikao wakitaka jina la Lowassa na bahati mbaya jina la Lowassa halikuwemo wakilenga atajwe katika scandal ya DAWASCO na kizuri zaidi serikali ilishinda katika kesi ile kwa maamuzi magumu ya Lowassa mpaka akahoji katika kikao cha ndani NEC mbele ya mwenyekiti kipi nilikifanya usicho kijua?

Na huu ndio muendelezo wa mashambulizi hadi katika scandal iliyoitwa Richmond. Baada ya kujiuzulu kwa -kiongozi huyu 2008 nilifuatilia sinema ile kwa umakini na nilishangazwa kuona kesi iliyofunguliwa dhidi ya Richmond na kuelezwa kuwa kampuni hii haipo na wala haijawahi kuwepo inashindaje kesi na mashauri yake -yote yaliyo funguliwa dhidi yake ?

Pili inakuwaje serikali inakubali -mitambo inauzwa kwa DOWANS na baadae SYMBION kwa baraka za baraza la mawaziri?, inakuwaje mitambo hiyo inagharimu pesa za wamarekani ambao tunaamini wapo makini -kwa waziri wao wa mambo ya nje H. Clinton na Rais wa Dunia- Barack Obama wanaikagua kwa ziara ya gharama za fedha za Wamarekani?.

Jibu hapa vita dhidi yake na mipango ilikwama na wanaposema fisadi alifisadi nini ? Au ndio trolling mitandaoni dhidi yake?.
 
Back
Top Bottom