Richmond na Dowans ni mali ya nani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Richmond na Dowans ni mali ya nani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mshikachuma, Dec 11, 2010.

 1. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 11, 2010
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Jamani nimejaribu kufuatilia sana kwenye magazeti,TV,na hata Redioni! Lakini bado sijafanikiwa kuwapata wamiliki halali wa iliyokuwa RICHMOND na sasa DOWANS.

  Maana majina haya mawili kwa sasa yamekuwa masikioni kwenye kila media na wanachi wote kwa ujumla. kisa? wameshinda kesi na wanatakiwa kulipwa karibu Billion 184 kutoka kwenye pesa za kodi za watanzania.

  Jamani nauliza kulikoni? Ni nani wamiliki wa kampuni hii ya Dowans? Nitashukuru kama nitapata jibu sahihi kwa faida ya watanzania wote! Maana hizo pesa ni nyingi sana na anaeenda kulipwa hatumjui.

  Nawasilisha wandugu.
   
 2. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #2
  Dec 11, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  RA, akishirikiana na EL pamoja na Mwizi mkuu hao ndio wamiliki halali. Lakini ukienda Brela wamejificha nyuma ya pazia.
   
 3. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #3
  Dec 11, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  want to piss on those guyz parade? Hakuna aliye tayari kutaja full names, may be mwana halisi na W. Slaa (PhD) ndio wanaweza kuwataja moja kwa moja.:embarassed2::A S-devil1:
   
 4. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #4
  Dec 11, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Ungekuwa mfatiliaji ungesha wajua siku nyingi sana au unawajua ila unataka wao wenyewe wakuzibitishie kuwa wao ndiyo wamiliki RICHARD MODULI
   
 5. Not_Yet_Uhuru

  Not_Yet_Uhuru JF-Expert Member

  #5
  Dec 11, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hapo umelenga....Ila BRELA ni chama gani? Umoja wa kisiasa au? Mie nadhani hatuna taasisi ya manufaa inayoitwa BRELA ktk maslahi ya Taifa hili. Hilo ni pazia jekundu linalofunika makampuni ya wizi, na mafurushi ya wizi na za mafisadi wanaopitia kampuni zao maruhani 'ghost' na kulinyonya taifa hili na kuliangamiza.

  Kumbuka makampuni yote yaliyochota fedha za EPA, yooote hayakupatiwa majibu ya nani mmiliki halali toka BRELA. Sasa hiyo BRELA ni NGO au Chama cha Siasa au ndio nini? Maana hata yenyewe haiwezi kujipatia majibu. Wao watakuambia Dowans na Richmond 'hazina wamiliki'.
  Ni makampuni mangapi ndani ya Brela yamepewa tu majina kumbe ni mirija ya hao mafisadi??....Ni Hasira sana hii! ...Aibu tupu ya nchi!
   
 6. m

  mams JF-Expert Member

  #6
  Dec 11, 2010
  Joined: Jul 19, 2009
  Messages: 616
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Kazi kwelikweli,watu hawashibi pesa
   
 7. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #7
  Dec 11, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Mbona wamiliki wake wanajulikana!!
  Ni RA na swahiba wake EL aka mamvi.
   
 8. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #8
  Dec 11, 2010
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0

  Hivi wewe huna akili? ukitaka kujuwa kampuni inamilikiwa na nani unakwenda BRELA sio JF.

  Nenda BRELA utajuwa wamiliki wa Richmond na wa Dowans ni kina nani. Nyamaaf!
   
 9. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #9
  Dec 11, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Na hawa ndiyo vibaraka wao

   
 10. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #10
  Dec 11, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Ni Rostam Aziz na Edward Lowasa
  Na huyu hapa chini ni kibaraka wao

   
 11. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #11
  Dec 11, 2010
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Nashukuru kwa majibu yenu wandugu! na sasa nawatumia majibu
  watu wote waliokuwa wanaumiza kichwa kuhusiana na jambo hili.
  Ila huyu Dar es salaam naona ana matatizo ya ubongo wake
   
 12. Chifunanga

  Chifunanga JF-Expert Member

  #12
  Dec 11, 2010
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 291
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  kwa kweli hata mimi hii kitu inaniumiza kichwa kweli....sijui kwa nini wamiliki wake hawajulikani....hivi ni kweli ni EL na RA au ndio tetesi tu....wenye proofs waziweke basi.

  mi nimejaribu kufanya search kwenye website ya BRELA pale BRELA-Companies and Business Names ON-LINE SEARCH na haya ndio majibu niliyoyapata...hakuna majina lakini

  DOWANS: 58550 DOWANS TANZANIA LIMITED 06/12/2006 incorporation

  RICHMOND: (zipo richmond kama tano hivi, ila hii nadhani ndio yenyewe) : 57014 RICHMOND DEVELOPMENT COMPANY LIMITED 13/07/2006 incorporation

  Hizo namba za kwanza ni registration numbers, sasa sijui zinaweza saidia kutafuta majina au?
   
 13. mchonga

  mchonga JF-Expert Member

  #13
  Dec 11, 2010
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,250
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Dowans ni mali ya CCM, Kampuni hii ilianzishwa kwa ajili ya chama kujipatia fedha kwa ajili ya uchaguzi. WANACHUKUA SERIKALINI KAMA MKOPO ukifuatilia utagundua kuwa CCM walitumia fedha nyingi ktk uchaguzi wa mwaka huu. Je unafikiri walipata wapi? ndiyo maana walihakikisha kwa udi na uvumba lazima wakae madarakani ili siri yao isitoke. Sasa njia rahisi kwao CCM ya kulipa zile pesa ni kutumia serikali kulipa Dawson ili pesa hizo ziende CCM na wao wazirudishe Serikalini ili ku-balance mahesabu kabla ya kikao kijacho cha bunge .
   
 14. mchonga

  mchonga JF-Expert Member

  #14
  Dec 11, 2010
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,250
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135


  Jaribu na hapa: BRELA-Companies and Business Names ON-LINE SEARCH
   
 15. kakuruvi

  kakuruvi JF-Expert Member

  #15
  Dec 31, 2010
  Joined: Sep 2, 2009
  Messages: 645
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Wadau kwanza niwape hongera japo kwa kufikia siku ya leo na pia naomba muungane nami tumuombe Mwenyezi Mungu atuoneshe mwaka 2011.

  Kulikuwa kumetulia ila jambo jipya (jipya kwa nje ila ukweli ni kuukuu) linaongoza vichwa vya habari na linamgusa kila mtanzania, kupitia Waandishi John Daniel na Suleman Abeid (MAJIRA) nimeona nanyi msome alafu tupate mtazamo wenu wana JF kwani huo ni mtazamo wa walioandika, nanukuu, nawasilisha.

  'Mwenye Dowans atajwe kabla ya kulipwa'  Na Waandishi Wetu

  SAKATA la malipo ya sh. bilioni 185 kwa Kampuni ya DOWANS iliyorithi mikoba ya kampuni hewa ya Richmond imezidi kuchafua hali ya hewa baada ya wananchi kumtaka Rais Jakaya Kikwete kumtaja hadharani mmiliki wa kampuni hiyo
  kabla ya kulipwa mabilioni ya fedha za walipa kodi.

  Wakizungumza na Majira kwa nyakati tofauti kutoka mikoa mbalimbali, wananchi hao wamesema wanasikitishwa na kauli ya serikali kukubali kuheshimu sheria kulipa Dowans fedha hizo wakati mmiliki wake hajulikani hadi sasa.

  Tunataka serikali, hasa Rais Kikwete, atuonyeshe mmiliki wa Dowans, ajitokeze hadharani mbele ya vyombo vya habari tumfahamu. Haiwezekani nchi ikashindwa kesi na hewa, maana hadi leo hatujui mmiliki wa Dowans ni nani.

  "Pia tunataka hiyo hukumu ipelekwe kwa Jaji Mkuu ili baadaye ilitolewe hadharani kwa vyombo vya habari tujue inasemaje,” alisema Bi. Catherine Maliwa wa Kigogo Dar es Salaam.

  Alisema katika historia ya Taifa la Tanzania haijawai kutokea nchi ikashindwa kesi na mtu asiyejulikana na kuonya viongozi wa Serikali wanaohusika kutothubutu kutoa hata senti kulipa Dowans bila wamikiki wake kujulikana na kujitokeza hadharani.

  “Jambo linalotusikitisha ni kuwa Richmond ni Kampuni feki na wamiliki wake hawajulikani, iweje Kampuni feki ambaye mmiliki wake hajulikani kuuzwa kwa Dowans, mtalipa pesa mashetani?” alihoji Bi. Maliwa.

  Alisema hivi sasa Watanzania wamechoshwa na viongozi wazembe wanaowabebesha mzigo wajane na maskini huku wahusika wakibaki salama na kufurahia maisha ya anasa kwa jasho lao.

  Alisema baada ya hatua ya Rais Kikwete kumtangaza mmiliki wa Dowans na mwenye kampuni hiyo kujitokeza hadharani na nakala ya hukumu kukwekwa hadharani kwenye vyombo vya habari wahusika wote wachukuliwe hatua za kisheria suala la kulipa fedha hizo liwe la mwisho.

  Mkoani Shinyanya wananchi walisema licha ya Mahakama ya Kimataifa ya kusuluhisha migogoro ya kibiashara (ICC) kuipa ushindi Dowand, utekelezaji hauwezekani hadi mmiliki wake ajulikane kwa Watanzania wote.

  Walisema ni ajabu na mshangao kwa shirika la serikali kupelekwa mahakamani na mtu asiyejulikana huku baadhi ya viongozi waandamamizi wakionesha kwa haraka dalili ya kutaka kulipa adhabu hiyo kwa mtu asiyefahamika.

  “Umefika wakati kwa Rais Kikwete abebe jukumu la kuwafahamisha rasmi Watanzania mmiliki halisi wa Dowans, itakuwa ni miujiza na aibu kwake kulipa fedha hizo kwa mtu asiyejulikana. Watanzania hatujawa wajinga kiasi hicho, kila mara serikali imekuwa ikieleza wazi kutomfahamu mmiliki wa Dowans,” alisema Bw. Fredy Mmassy.

  Wananchi hao walihoji kauli iliyotolewa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuwa serikali inaheshimu sheria na kwamba ikibidi haina ujanja zaidi ya kulipa mabilioni hayo kwa Dowans.

  Rais atueleze na amtaje huyo mtu, vinginevyo Watanzania hatutokubali fedha hiyo ilipwe, na hata ikilipwa kwa nguvu waelewe iko siku tutaidai kwao, alisisitiza Bw. Mmassy.

  Wananchi hao walisema mbali na Rais Kikwete kumtaja mmiliki wa kampuni hiyo pia awaeleze Watanzania mwakilishi wa serikali aliyeiwakilisha TANESCO katika mahakama ya ICC.

  Walisema imefika wakati wa serikali kuweka wazi mkataba kati yake na kampuni hewa ya Richmond pamoja na ule wa Dowans ili kila kitu kifahamike na Watanzania wajionee wenyewe ni wapi TANESCO inapotiwa hatiani kabla ya fedha hizo kulipwa.

  Katika hatua nyingine wananchi hao walimtaka Rais Kikwete kuangalia upya maamuzi ya TANESCO kupandisha bei ya umeme na kuweka wazi kuwa hali hiyo haiendani na maisha yao duni na umasikini uliokithiri.


  Tunaomba Rais Kikwete kama kweli anawathamini Watanzania waliomchagua kwa moyo mmoja basi, azuie ongezeko la bei mpya za umeme, viongozi wetu wameonesha wazi kutokuwa na huruma na watu wao, wanakubali kulipa sh. bilioni 185 na kuongeza bei ya umeme,” alisema Bw. Masunga Jilaba, mkazi wa kitongoji cha Ndembezi mjini Shinyanga.

  Hawa wana haki ya kufanya hivyo kwa sababu hawatoi hata chapa moja mifukoni mwao kwa ajili ya kulipia umeme, uchungu wataupata wapi? Ni Watanzania masikini wanaohangaikia hata mlo wao wa siku ndiyo watapaswa kulipa deni hilo la Dowans kupitia ankara za kila mwezi za matumizi ya umeme,” alisema Bw. Jilaba.

  Wananchi hao walisema ongezeko la bei ya umeme kwa asilimia 18.5 ni dalili ya wazi kuwa wateja wa TANESCO ndiyo wanaopaswa kuilipa Dowand na kwamba hilo halihitaji mtu kuwa na elimu ya chuo kikuu kufahamu kuwa kampuni hiyo ni ya mfukoni na kuna watu wanafaidika nayo kwa njia moja au nyingine.

  Katika hatua nyingine wanachi hao wamehoji kauli iliyotolewa na Waziri Mkuu aliyejiuzulu Bw. Edward Lowassa, kwamba wananchi watangulize upendo kudai katiba mpya na kumtaka atafute kwanza upendo na huruma kwa Watanzania.

  “Najiuliza ni upendo gani anaounzungumzia, yeye anajua upendo tumeumizwa na mengi ikiwemo mikataba mibovu, kama angejua upendo nchi isingeingia katika mkataba wa aibu wa Richmond wakati akiwa madarakani,” alisema Bi. Maliwa.

  Alisema Bw. Lowassa anapaswa kuwaomba radhi Watanzania kwanza ili kuonesha upendo badala ya kujifunika shuka nyeupe wakati ndani kuchafu.

  Wakati huo huo serikali imeshauriwa kuangalia uwezekano wa kusitisha mikataba yote na makampuni ya uzalishaji umeme ikiwemo IPTL na Songas ili fedha zinazotumika kulipa capacity charge zitumike kununulia mitambo itakayomilikiwa na serikali.

  Umefika wakati wa serikali kukatisha mikataba mibovu inayowakamua Watanzania katika uzalishaji umeme hata kama ni kulipa fidia basi fidia ilipwe ili fedha zinazolipwa kila siku kwa makampuni hayo zielekezwe katika kununua mitambo yetu sisi wenyewe,

  Kwa hii Watanzania tutakuwa radhi hata kama nchi itaingia gizani kwa miezi miwili mfululizo ni bora iwe hivyo, na katika kipindi hicho umeme kidogo unaozalishwa na TANESCO yenyewe uelekezwe katika maeneo nyeti tu ya uzalishaji, ili mradi tu baada ya muda mfupi tuwe na mitambo yetu wenyewe,” alisema Bw. Juma Shukuru.

  Imeandaliwa na John Daniel Dar na Suleiman Abeid, Shinyanga
   
 16. Nchi Kavu

  Nchi Kavu JF-Expert Member

  #16
  Dec 31, 2010
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 3,520
  Likes Received: 1,041
  Trophy Points: 280
  Japo sijasoma habari hiyo ndefu nimeona mantiki kwenye title. Nashangaa hii nchi. Yaani tunataka kumlipa jini? Tumjue kwanza huyo Dowans ndio tuidhinishe malipo
   
 17. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #17
  Dec 31, 2010
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Sitaki kusema neno maana nina hasira na hawa watu..wametugeuzwa mbumbumbu vyakutosha!..watawala wasiojua kusoma alama za nyakati...wababe...wenye kiburi na wezi wa wazi wazi!
   
 18. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #18
  Dec 31, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Atatajwa mara ngapi jamani mlisha ambiwa Dowans dada ake ni Richmond sasa mchanganye akili za kuambiwa na zenu
   
 19. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #19
  Dec 31, 2010
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Mkurugenzi wa Tanesco anasema Mmiliki wa Dowans ni siri mpaka pale hukumu ya kesi ya Dowans itakaposajiliwa hapa nchini ndio mmiliki atafahamika. Haya ni maajabu, hivi kweli tangu lini wamiliki wa makampuni wakawa siri? au ndio anatafutwa/anachakachuliwa mmiliki ili baadae tuambiwe mmiliki wake? Kwa nini anafichwa?
  RA, EL na washirika wenu mnatajwa tajwa kama wamiliki..sijasikia mkikataa au kukubali, kanusheni basi au mkubali na muombe msamaha na muachane na hayo madai yenu ya kulipwa fidia, kwa nini hamna huruma nyinyi? Kila siku kanisani na misikitini hamna hata aibu, kwa dhambi hizi mnajisumbua kwenda makanisani au misikitini.
  Hatuna haki ya kuhukumu wengine lakini kwa haya mnayowafanyia watanzania......RA, EL,JK na wengine wanaila nchi hii bila huruma......yenu ni Jehanum. Jehanum inaanzia hapa hapa duniani, siku si nyingi mtaona yatakayowapata kwa kuwasababishia mahangaiko watanzania wasio na hatia. Hata maisha yenu sijui kama mna'enjoy' na hizo hela za wizi, kila mnachofanya mwanyooshewa vidole. Hata muwe na maghorofa mia mbili kama hamna peace of mind hayakusaidii chochote. Tafadhali wamiliki jitokezeni na mtubu mkiwa hai, hakutakuwa na nafasi nyingine ya kutubu mkishakufa. Kwenda kuhiji Isarael hakusaidii bila kutubu mbele ya watanzania na kuacha ujambazi mnaoufanyia watz. Mungu Inususuru nchi yetu, wape mapigo kumi (sio saba) wale wote wanasababisha mateso kwa watu wako. Amen.
   
 20. r

  rushasha JF-Expert Member

  #20
  Dec 31, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 732
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  MUNGU si mwanadamu, na hakuna mwanadamu atakayejilinganisha na MUNGU! MUNGU anayaona haya yote, na Watanzania tuzidi kumuomba MUNGU ili wahusika wa haya ashughulike nao yeye mwenyewe. MUNGU amesikia kilio cha Watanzania na nina amini kuwa hatakaa kimya, atafanya kitu! Sisi kama wanadamu tuna mapungufu yetu lakini kwa kweli hili la kuwasababishia wengine maumivu ya jinsi hii kwa kweli halivumiliki! MUNGU tunakuomba ukaonekane HARAKA katika hili! Wewe ni MUNGU Mkuu, waweza yote hakuna tena MUNGU kama wewe!
   
Loading...