Richmond mpya wizara ya nishati | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Richmond mpya wizara ya nishati

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Jul 30, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 30, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,609
  Trophy Points: 280
  [​IMG]


  KATIBU Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi anakabiliwa na lundo la tuhuma ikiwa ni pamoja na kilichoitwa kujipa mamlaka ya kuendesha Shirika la Umeme la Taifa (Tanesco), imefahamika.Aidha, Maswi anatuhumiwa kushinikiza kusimamishwa kazi Mkurugenzi Mtendaji wa shirika

  hilo, William Mhando bila kufuata taratibu na kanuni za ajira yake.
  Katibu mkuu huyo anatuhumiwa pia kukiuka baadhi ya taratibu, ikiwamo kufanya manunuzi kinyume cha sheria na kuingiza shirika katika mikataba tata.Taarifa zinasema Maswi ndiye aliyeshinikiza Mhando kusimamishwa kazi kwa

  maslahi binafsi.
  Uchunguzi wa MwanaHALISI unaonyesha kuwa bodi ya wakurugenzi ya Tanesco haikutaka kumfukuza Mhando hadi ipate kwanza baraka za mamlaka ya uteuzi (rais); lakini shinikizo lilitoka kwa Maswi.Mwenyekiti wa bodi ya shirika hilo, Jenerali Robert Mboma amethibitisha kufanyika

  maamuzi hayo bila kufuata taratibu.
  “Ni kweli, kulikuwa na hoja ya kumsimamisha kazi Mhando, lakini nilisema uamuzi usitangazwe mpaka nimpe taarifa Mhe. Rais Jakaya Kikwete; naye anipe kibali kwa sababu yule ni mteuliwa wake…lakini ndiyo hivyo tena. Ikatangazwa kabla ya Jumatatu ya 16 Julai,”

  ameeleza.
  Lakini kiongozi mmoja ndani ya bodi ya Tanesco ameeleza, “Huyu bwana ndiye amekuwa mtendaji wa Tanesco. Jambo hili na mengine ambayo bado hayajafumuka, yamemuudhi sana mwenyekiti.”Akitaka kuthibitisha madai hayo, mtoa taarifa amesema Maswi ndiye anahusika na kuipa kazi kampuni

  ya BP (T) Ltd., ya kusambaza mafuta ya kuzalishia umeme wa IPTL, yenye thamani ya zaidi ya Sh. 28 bilioni.
  Taarifa zinasema ni Maswi aliyeagiza BP kuuza mafuta yake kwa Tanesco wakati kampuni hiyo ilienguliwa kwenye zabuni; jambo ambalo ni kinyume cha sheria ya manunuzi ya umma (PPRA) ya

  mwaka 2004.
  Sakata la Richmond ambalo linaendelea kuitesa serikali, lilitokana na kampuni hiyo kupewa mkataba wa kufua umeme kwa upendeleo baada ya kushindwa kwenye zabuni.Inadaiwa Maswi alifanya maamuzi kama hayo kwa BP, tena bila kushirikisha Mhando.Taarifa zinasema pia ni kwa “vitendo

  vya hatari vya aina hiyo, vya kuingiza shirika katika mgogoro wa kisheria,” Jenerali Mboma ameamua kuripoti kwa Rais Kikwete.
  Bali Maswi aliwaambia waandishi wa habari juzi Jumatatu, ofisini kwake, Dar es Salaam kuwa hahusiki na tuhuma hizo kwa vile alipoingia wizarani hapo mchakato huo ulikuwa

  tayari umeanza.
  Lakini alipoulizwa na MwanaHALISI, aligoma kuzungumzia suala hilo, badala yake alitaka mwandishi kwenda ofisini kwake kuchukua taarifa aliyosambaza kwenye vyombo vya habari.Hata hivyo, nyaraka zilizopo zinathibitisha jinsi Maswi alivyokuwa wakala wa BP, mratibu, msimamizi,

  mlipaji na mnunuzi wa mafuta hayo yaliyonunuliwa kwa fedha za umma.
  “Ndugu yangu, katika mazingira haya, ni nani anayepaswa kuchunguzwa kati ya katibu mkuu wizara ya nishati na madini, Eliakim Maswi na Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, William Mhando,” amehoji mjumbe mmoja wa bodi ya

  Tanesco.
  Taarifa zinamuonyesha Maswi akipokea hati ya kabla ya malipo – Profoma Invoice – iliyoambata na ujumbe wa barua pepe kutoka meneja masoko ya BP (sasa Puma Ltd), Machumani Shebe uliosema, “…itakuwa ni vema zaidi kama utaweza kutupatia nyaraka rasmi za jambo hili

  kiofisi.”
  Anasema, “Naomba tupate barua ya uthibitisho wa malipo kutoka wizarani kwako ili kuwa na uhakika wa malipo. Tunataka pia utupatie LPO (ankara ya malipo) ya kiwango cha mafuta kitakachosambazwa.”Akiandika kwa njia ya kushukuru, Shebe anasema, “Tunakushukuru kwa kutupatia biashara hii na tunatarajia kusikia kinachoendelea kutoka kwako hivi mapema iwezekanavyo.”Mara baada ya kupata ujumbe huo kutoka BP, Maswi

  alimwandikia ujumbe naibu mkurugenzi mtendaji wa Tanesco anayeshughulikia uzalishaji, Boniface Njombe, tarehe 12 Julai 2012 kumwamuru kuandaa malipo hayo haraka iwezekanavyo.
  Barua ya Maswi kwenda kwa Njombe, ilinakiliwa kwa Mhando na Decklan Mhaiki, ambaye ni naibu mkurugenzi wa

  shirika anayeshughulikia usambazaji umeme.
  Kwa kasi ya aina yake, siku hiyohiyo ya 12 Julai, Njombe alimwagiza Anetha Chengula wa idara ya uhasibu, kuandaa malipo kwa kile alichoita, “Utekelezaji wa maelekezo ya Maswi.”“Bila shaka unakumbuka juu ya jambo hili. Tupo wizarani hapa na tumepokea hati

  malipo kutoka kwa katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini iliyotoka Puma (BP) watakaosambaza HFO kwa ajili ya mitambo ya IPTL,” ameeleza Njombe katika barua yake kwa Chengula.
  Amesema, “Malipo hayo yatafanywa na wizara ya nishati na madini kama ambavyo tulikubaliana. Hivyo unatakiwa kuandaa malipo ya mafuta hayo haraka kwa msambazaji na unijulishe.”MwanaHALISI lilipomuuza Mboma kuhusu madai hayo, alikiri kuwa

  shirika lake halijawahi kuipa kazi kampuni ya BP.
  Alisema, “Mimi ninachofahamu ni kwamba TANESCO ina-deal (inashughulika) na makampuni yale matatu yaliyokuwa na sifa. Sifahamu jingine nje ya hapo.”Mbali na kulazimisha kulipwa fedha hizo, Maswi amedaiwa kuzuia Sh. 36 milioni kutoka Wizara

  ya Fedha (Hazina) ambazo ni sehemu ya fedha zilizoombwa na Tanesco serikalini.
  Tanesco iliomba, tarehe 22 Septemba 2011, Sh. 136 bilioni kwa ajili ya gharama za kuendesha mitambo ya dharura ya umeme. Ilitarajia kuzirejesha baada ya kupata mkopo wake mkubwa wa Sh. 408 bilioni ambazo shirika hilo

  liliahidiwa.
  Akiwa kaimu katibu mkuu wa wizara hiyo, Maswi anadaiwa kukata Sh. 36 bilioni na kuipa Tanesco Sh. 100 bilioni. Inadaiwa alitoa maelezo kuwa kiasi kilichokatwa kitafuta mkopo wa Sh. 20 bilioni katika benki ya CRDB.Katika barua yake ya 28 Septemba 2011 yenye kumb. Na.

  AB.88/286/01/15 kwenda kwa mkurugenzi mtendaji wa Tanesco, Maswi anaeleza kuwa kiasi kilichobaki cha Sh. 16 bilioni kingetumika kununulia mafuta mazito kwa mitambo ya IPTL kwa mwezi Oktoba 2011 kutoka Puma/BP.
  Mhandisi Mhando alisimamishwa kazi 13 Julai 2012 pamoja na maofisa watatu

  waandamizi – Naibu Mkurugenzi, Huduma za Shirika, Robert Shemhilu, Ofisa Mkuu wa Fedha, Lusekelo Kassanga na Meneja Mwandamizi Manunuzi, Harun Mattambo kwa kilichoitwa “madai ya matumizi mabaya ya madaraka na ubadhilifu.”
   
 2. Msalagambwe

  Msalagambwe JF-Expert Member

  #2
  Jul 30, 2012
  Joined: Jul 11, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Huu ni wizi wa mchana kweupe,
  Siamini mjeshi Mboma anachezeshwa Joyce wowowo na kijana mdogo?
  Kuna haja 2015 kuwa na wabunge 75% ya wabunge kutoka CDM tu,
  ili kumaliza ujinga huu once and for all.
   
 3. Kiona

  Kiona JF-Expert Member

  #3
  Jul 30, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 936
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mtoto wa jirani ama kweli mbebe akiwa kalala akiwa macho atamlilia mamake. Bado hamjaamka sawa sawa
   
 4. Nyenyere

  Nyenyere JF-Expert Member

  #4
  Jul 30, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,567
  Likes Received: 1,930
  Trophy Points: 280
  Ndo ujue kwamba hii ngoma ni nzito. B.M. Mkapa vs Mike Tyson!
   
 5. Msalagambwe

  Msalagambwe JF-Expert Member

  #5
  Jul 30, 2012
  Joined: Jul 11, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Niliwahi kusikia kwenye radio, moja hapa USA, ya Coast to Coast kwamba, kuna race moja ya Alien, ambao Umbo lao ni mijusi, lakini wana uwezo wa, kuchaange shape zao na kuonekana watu, kwamba ndiyo asili ya vurumai, za kiuchumi, kisiasa, na kidini hapa duniani.

  Inanifanya niamini hili, kuna mambo yanafanywa, na watendaji wa serikali ya CCM, yanaonyesha wazi kwamba, wako under control,
  ya race hii ya Alien, ambao nia na madhumini yao, ni kutawala uchumi wa dunia nzima, na kugeuza binadamu wote, kuwa watumwa wao, kama ilivyokuwa awali, wao walipokuwa mabwana, huko Egypt na Mesopotamia.

  Biashara yao kubwa duniani, ni dhahabu na vito vya thamani, nyingine ni usafiiri wa anga meli na viwanda. Sasa hivi wamejiingiza ipasavyo, katika biashara ya anga za juu, ndiyo maana hata serikali ya Marekani, imenyoosha mikono, na kukabidhi utafiti wa anga za juu, mikononi mwa watu binafsi.

  Maelezo haya yanabezwa na watu wengi, lakini yana ukweli fulani ndani yake.

  Mijusi hawa wakikubana kisawasawa, kisha wakakukata mjengo wa nyuma, na kukupa oda uzifuate bila maswali, ukigoma unapigwa mjengo tena, naambiwa huwezi kukataa, mijusi hao hawafai. ukibali unakua tajiri na si rahisi, kwenda jela kwa makosa uliyofanya,
  ukiamua kuanika hadharani, yaliyokukuta, kila mtu atadai umedata, tangu lini mijusi wana akili, sembuke kumkata mjengo mtu??
   
 6. Osaka

  Osaka JF-Expert Member

  #6
  Jul 30, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 1,766
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Wabongo bwana, kila ngoma inayopigwa wanacheza tu!
   
 7. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #7
  Jul 30, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Ninyi ndiyo wale wle mliohongwa ili kuwatetea akina MHANDO siyo?
   
 8. m

  mams JF-Expert Member

  #8
  Jul 30, 2012
  Joined: Jul 19, 2009
  Messages: 616
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Waziri na Katibu Mkuu wa hii Wizara ni wasomi wasio shaka na maamuzi yao hayakufanyika kwa pupa. Inasikitisha kuona wazawa wanajitokea kutukomboa toka gizani tunaanzisha usanii kwa kuwabeza!
   
 9. m

  mharakati JF-Expert Member

  #9
  Jul 30, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  maswi na Prof Muhongo ni outsiders kwenye wizara nyeti ya ulaji na kwa hilo wanapata wakati mgumu sana hawa wazalendo. hawa waandishi habari wa mifukoni watatupeleka pabaya na hizi tuhumua na counter tuhuma.
   
Loading...