Richmond mpya nayo tunasubiri kamati teule | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Richmond mpya nayo tunasubiri kamati teule

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MADORO, Nov 24, 2011.

 1. M

  MADORO Senior Member

  #1
  Nov 24, 2011
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 199
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Wadau tunauliza, yawezekana siku hizi bila kamati teule hata kama kitu kinasemwa kibaya kwa taifa serikali inakaa kimya mpaka ibanwe bungeni ndo inaunda kamati teule. Tunasema kuna richmond inapikwa singida.na tunasema kuwa tangu tarehe 25 august 2008 kituo cha taifa cha uwekezaji (tic) ilitoa cheti cha motisha na kuifutia kampuni ya wind east africa na kuifutia kodi, kampuni imesajiliwa 12 august 2008, cheti kilitolewa na kifanye kazi kati ya august 2008 hadi july 2011. Leseni hiyo inaonyesha kampuni ilipewa eneo, lakini yenyewe imekuja na eneo tofauti la lile lililloidhinishwa na serikali. Hata hivyo mpaka 20/10/2011 kampuni hiyo ilikuwa haina eneo singida, pamoja na kuwa ilikuwa tayari . Imeshajichotea mipesa toka ubalozi wa uingereza, na kupata ahadi ya kupata mikopo world benk, hatujajua za ndani zimechotwa kiasi gani. Lakini ieleweke kwanza kuwa utaratibu wa kampuni kupewa cheti wakati haina eneo, kuna mengi ya kuuliza. Je tunasubiri yawe makubwa tukaunde kamati teule..... Wajukuu hawatalaani tulivyouzwa, watalaani tulivyoangalia wakati tunauzwa
   
 2. I

  Isango R I P

  #2
  Nov 24, 2011
  Joined: Jul 23, 2008
  Messages: 295
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kwa utamaduni wa kulindana wa kitanzania, sitegemei kama kuna mtu atafuatilia sakata hili. Kama dodoma ambapo mafisadi walitajwa hawakusumbuliwa katika kikao, sembuse mradi ambao kwanza ndo unaanza. Kweli tunasubiri tume.
   
Loading...