‘Riba kubwa kikwazo cha kukopa’ benki


kbm

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Messages
5,144
Likes
268
Points
180
kbm

kbm

JF-Expert Member
Joined Oct 5, 2012
5,144 268 180
Dodoma. Changamoto zinazowakabili wakopaji wadogo katika taasisi za fedha nchini, ni riba kubwa inayotozwa na mabenki na taasisi zake, Bunge lilielezwa jana.
Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi, wakati akijibu swali la Cynthia Ngoye (Viti Maalumu-CCM).
Mbunge huyo alitaka kujua ni lini Serikali itawapatia mafunzo ya ujasiriamali wanawake wa Mkoa wa Mbeya na kama Serikali itakuwa tayari kuhamasisha benki mbalimbali kusogeza huduma karibu na wananchi ili kukidhi azma yao ya kuwapatia mikopo na kujiwekea akiba.
Waziri alisema kuwa Serikali kupitia Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) ilifanya utafiti katika Mkoa wa Mbeya na kubaini kuwa wananchi wengi wakiwamo wanawake wameanzisha vikundi vya uzalishaji.
“Kutokana na juhudi hizo, Baraza kwa kutumia Mfuko wa Uwezeshaji Mwananchi Kiuchumi imeanza kutoa udhamini kwa mikopo kwa wananchi wa Mbeya hususani Chimala Saccos,” alisema Lukuvi.
Alisema utaratibu wa kutoa mafunzo umeandaliwa na kwamba mafunzo yataanza kutolewa mwanzoni mwa mwaka wa fedha wa 2013/14.
Alibainisha kuwa mafunzo hayo yatalingana na mafunzo ambayo yalishatolewa na Serikali katika Mikoa ya Dodoma, Ruvuma, Tanga, Manyara na Dar es Salaam.
Lukuvi alisema kuwa Serikali itaendelea kuzihamasisha benki na taasisi za fedha kupunguza riba na masharti mengine ya mikopo ili wananchi wengi zaidi wenye mitaji midogo waweze kunufaika na fursa hiyo na kujiongezea kipato.
Malalamiko ya kuwapo kwa riba kubwa kwenye mikopo ya mabenki yanatolewa wakati wiki iliyopota Mbunge wa Viti Maalumu Zakia Meghji alishangaa kuona mabenki yanatoza riba kubwa badala ya asilimia nane ambayo Serikali kupitia benki kuu iliidhinisha.

CHANZO: Mwananchi
 
Nyani Ngabu

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Messages
82,401
Likes
50,137
Points
280
Age
29
Nyani Ngabu

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined May 15, 2006
82,401 50,137 280
Sasa hiyo riba kubwa haina namba? Ni asilimia 9 ama 25?

Hizi habari zingine bana.
 
Kiranga

Kiranga

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2009
Messages
43,026
Likes
18,242
Points
280
Kiranga

Kiranga

JF-Expert Member
Joined Jan 29, 2009
43,026 18,242 280
Sasa hiyo riba kubwa haina namba? Ni asilimia 9 ama 25?

Hizi habari zingine bana.
Wabongo nine times out of ten ukitaka matatizo nao tafuta exactitude na specificity.

Habari ya finance namba pekee unazoziona ni miaka 2013/14.
 
H

halikela82

Senior Member
Joined
May 14, 2013
Messages
187
Likes
2
Points
0
H

halikela82

Senior Member
Joined May 14, 2013
187 2 0
Sina ham na hizi bank za bongo me kuna 1 nilienda kutaka m2 wakanambia niweke nyumba sikuaga hahahahaha.
 

Forum statistics

Threads 1,273,538
Members 490,428
Posts 30,484,489