TANZIA Rest In Peace Tanzania One (T.O), Elias Kihombo

Leo tunavyozungumza Elias Kihombo hatunaye tena duniani. Inasemekana kifo chake ni kutokana na maradhi yaliyokuwa yakimkabili.

Tunahitaji kuwa Karibu na Mungu wakati wote kwani safari yetu ipo mikononi mwake.

Bwana ametoa na bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe!

I will never forget you My brother.

You will be missed forever and always. The beautiful moments you shared with me will always speak of a great person that you were. Rest in peace up in heaven.

-----
Pia soma




ALAMA ALIZOACHA ELIAS KIHOMBO


Imepita miaka takribani miaka 14 sasa, tangia Tanzania ilipopata kumshuhudia mwanafunzi alieshindikana katika masuala ya Elimu hapa namzungumzia,Tanzania One (2006) Elias Kihombo katika matokeo ya Kidato cha Sita mwaka 2006 akitokea shule ya sekondari Tosamaganga wengi wanapenda kuiita Tosa Boy's

Mwaka 2006, Necta ilimtangaza mwanafunzi Elias Kihombo kutoka Tosamaganga Secondary School kuwa ndo kipanga wa mwaka huo akiwapita wanafunzi wenye akili zaidi waliovuma toka shule kongwe na special schools kama Kibaha, Ilboru, Mzumbe, Kilakala, Tabora Boys etc ukweli ni kwamba Elias Kihombo hakuwa maarufu kwa kipindi hiko na wengi walisikia tu story zake haswa kwa Wanafunzi wa Mzumbe Boys ambao Mara nyingi walipata kumuona katika mazingira yao.

Kumbuka kwamba Elias Kihombo hakupewa Priority kubwa sana ya kuwa T.O wa Advance Level kutokana pia na matokeo yake ya Kidato cha Nne (4) kuonekana kuwa ya kawaida sana, Kihombo alifanikiwa kupata Division One (1.14) akiwa na Physics-A Chemisrty-A Biology na Mathematics-B, Ndipo mwaka huo 2003 alipata kuchaguliwa Tanga Technical school iliyopo mkoa wa Tanga (tetesi), lakini baadae aliamua kurudi tena katika shule yake ya zamani yaani Tosamaganga Secondary kuendelea na masomo yake ya Advance Level. Alimaliza hapo hapo akifanikiwa kuwa mwanafunzi wa kwanza toka Tosamaganga kwa Advance Level kuwa mwanafunzi bora kitaifa, Alifanikiwa kupata maksi za juu sana na kupata Division One (1.3)

Physics-A
Chemistry-A
Advanced Mathematics-A

October 2006 Alichaguliwa kujiunga na University of Dar Es Salaam (UDSM) akiwa kama T.O kusoma Bachelor of Science In Telecommunication Engineering (4years) na tetesi zinasema alifanikiwa kupata ufadhili wa masomo yake chini ya kampuni ya Airtel.

Siku zilienda na alikuwa karibu kumaliza Elimu yake ya chuo kikuu, huku akipata madili mengi ya kufundisha Tuition maeneo mbalimbali ya mkoa wa Dar Es Salaam na shule nyingi za sekondari ndani ya Tanzania, hasa shule za Advance.

Lakini baada ya Miaka 4 kupita ikiwa miezi michache tu imebaki ya kumaliza chuo, Tanzania One Kihombo alidisco chuo na hivyo kumfanya asifanikiwe kupata degree yake ya kwanza mwaka huo 2010, lakini wengi wanasema hakupaswa kudisco chuo lakini ndivyo ambavyo Hatima yake ilipoishia hapo (tetesi )

Moja kati ya maneno ambayo wengi wanamnukuu aliyopata kuyasema ndani ya Miaka hiyo, alisema "Duniani walionipita kwa akili ni watu wawili tu wa kwanza Mola, wa pili ni Mzungu" hapa ndipo hatima yake inavyosemekana ikafungwa na wakuu wake lakini wengine wanasema vingine.

Elias hakutaka kwenda chuo chochote kile na ndani ya Miaka hiyo mitatu baada ya kudisco chuo, yaani 2011, 2012 na 2013 alikuwa anazunguka shule mbalimbali za sekondari Tanzania kupiga mapindi ya Physics na Chemistry na kwelii huyu jamaa alikuwa ni Invisible katika masomo hayo mawili, Japo Pure Mathematics alikuwa hafundishi kabisa kwasababu alikuwa anasema "Siwezi kufundisha Somo rahisi duniani kama Pure Mathematics, Mimi nafundisha Physics na Chemistry tu"

Ndipo baada ya Miaka mitatu kupita (3) T.O aliyetukuka zaidi katika vinywa vingi vya wanafunzi wa Tanzania, kutokana na ufundishaji wake na kuwaita wanafunzi wake Nyumbu na kuwa na Jeuri zaidi ya Akili zaidi ya watu wengine, alifanikiwa kurudi tena ndani ya University of Dar Es Salaam safari hii akiwa ameamua na amezamilia kuchagua kozi nyingine Mpya kabisa iliyoanzishwa mwaka huo 2013 hapohapo Udsm iliyoitwa (Bachelor of Science In Petroleum Engineering). Hii kozi ilikuwa inachukua wanafunzi 20 pekee Tanzania nzima tena wale waliosoma PCM tu (Physics, Chemistry na Advanced Mathematics) na waliopata Marks za juu kabisaa.

Baada ya Miaka 4 kupita, ndipo July 2017, T.O Elias Kihombo alifanikiwa kumaliza Degree yake ya kwanza (Bachelor of Science In Petroleum Engineering) na mnamo November 2017 Elias Kihombo alifanikiwa kutunukiwa Degree yake ya kwanza akiwa ndani ya University of Dar Es salaam baada ya Miaka 11 kupita.

Hapa imepita Miaka mingi tangia, 2006 Engineer Elias Kihombo alivyotangazwa kuwa Tanzania One lakini ilimchukua Miaka mingine 11 mpaka kutunukiwa Degree yake ya kwanza. Huyu ndiye The Best Of The Best, Eng Elias Kihombo Mwanafunzi aliyepata kutokea Tanzania kuwa na uwezo mkubwa darasani. Nlsikia jinsi ambayo eng elias alikuwa na kipaji cha kufundisha kuanzia asubuhi mpk jioni na kusitokee hata swali moja liliomtolea nje .siku ambayo alisolve maswali kuanzia saa moja hadi saa nne hakuna swali lililo msumbua saa tano hadi saa nane hakuna swali lililo msumbua saa tisa hadi saa kum na mbili hakukua na swali lililo msumbua tuliendelea na mwendo huo kwa muda wa wiki moja . Itabaki historia ktk maisha ya wanafunzi na elimu ya Tanzania kwa ujumla.

Lakin leo tunavyozungumza Elias Kihombo hatunaye tena duniani. Inasemekana kifo chake ni kutokana na maradhi yaliyokuwa yakimkabili. Tunahitaji kuwa Karbu na Mungu wakati wote kwan safari yetu ipo mikononi mwake. Bwana ametoa na bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe!

I will never Forget you My brother

You will be missed forever and always. The beautiful moments you shared with me will always speak of a great person that you were.

Rest in peace up in the heaven

View attachment 1630262
View attachment 1630283
Kafa na ukimwi tetesi zinahakikisha 😒
 
Back
Top Bottom