Zakayo Chacha Wangwe
Member
- Jul 6, 2014
- 5
- 6
- Thread starter
- #41
CHACHA WANGWE/ CHACHA RASTA
Ni miaka 6 imepita tokea ulipotutoka usiku ule wa tarehe 28/7/2008. Bado jina lako linakumbukwa na watanzania wengi ilihali ipo wazi kuwa, wabunge waliotukoka katika bunge lile la tisa walikuwa wengi lakini jina lako ni miongoni mwa majina machache ambayo bado yako vichwani mwa watanzania.
Hii ni kutokana na matendo yenu, misimama, ujasiri na umahiri wenu wa ujengaji na usimamiaji kuntu wa hoja kwa maslahi ya taifa letu.
Mzee, unakumbukwa sana na wanatarime waliokuamini na kukutunuku nafasi mbili za uongozi (Udiwani na Ubunge) na hatimaye na watanzania wengine kukufahamu.
Kumbukumbu hii hutokea hasa wanapokumbwa na mambo magumu yanayogusa maisha yao moja kwa moja. Hii ni kutokana na kutopata viongozi ambao hawako tayari kutetea maslahi yao (wananchi) kwa hali yoyote ile na hata kutokuwa tayari kuweka maisha yao rehani kwa maslahi ya wanyonge wa Tarime na Tanzania kwa ujumla. Wanatarime tumeendelea kukuso viongozi Wa kaliba yako.
Viongozi wengi ambao tumewapa ridhaa ya kututumikia ni wale ambao wanadhani kujipendekeza, kugawa watu katika makundi ili wakose umoja wa kusimamia uwajibikaji na mstakabali chanya wa maendeleo ya Tarime ndio mbinu mbadala ya utumishi. Viongozi wafyata mikia pale ujasiri wao unapohitajika, halikadhalika viongozi ambao wamekosa kabisa weledi wa ujengaji wa hoja na ushawishi wawapo ndani ya vyombo vya uwakilishi. HIVI NIVIKWAZO VINGINE VYA MAENDELEO.
Nyamongo kumegeuka kuwa dead zone ( sehemu ya kifo)
Vijana wetu wameendelea kuawa kama kuku kwa makusudi na polisi wasiokuwa na uzalendo, sio tu kwamba serikali yetu imeweka rehani maisha na utu wa watanzania kwa anasa za mtu mweupe, lakini pia imeendelea kuhatarisha maisha ya mifugo na mimea kwa maji yenye kemikali hatari za sumu yanayo tiririka kwenye makazi ya watu. Hata fedha ambazo Mgodi ulikuwa unatoa kwa halimashauri ya Tarime kwajili ya vijana wetu kusoma bure, leo zimekuwa ni ndoto. HAKUNA FEDHA TENA. Nina asilimia zote chini ya uongizi wako usingekubali kufyata mkia katika hili. HII NI FEDHEHA KWA TAIFA LETU.
Mzee, CHADEMA uliyoiacha Tarime siyo iliyopo kwa sasa. Hata vikao vilivyokuwa vinatumika kujadili mikakati jadidi namna gani ya kukabiliana na wadhalimu na wahujumu maendeleo ya Wanatarime, leo vimegeuka kuwa sehemu ya ndondi na kutupiana maneno kwa faida, anasa na fuaha ya watu wachache ambao wameendelea kuendeleza uhasimu ndani ya chama.
Hii dhambi ya makundi ya mahasimu imeendelea kudhorotesha ustawi wa chama na hatimae kutoa mianya hata watu wenye uwezo kiduchu kushinda uchaguzi. HII NI DHAMBI AMBAYO INAENDELEA KUKITAFUNA CHAMA licha ya jitihada za makusudi ambazo wanachama tusio amini kwenye dhambi hiyo kuendelea kukiunganisha Chama kwa maslahi ya kujenga demokrasia shindani (competitive democracy) kwa maslahi ya jimbo letu.
TUTAENDELEA KUKUENZI,
TUTAENDELEA KUKUMBUKA .
MUNGU AKULAZE MAHALA PEMA PEPONI,
Amen.