Republican sasa rasmi ni chama cha makahaba? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Republican sasa rasmi ni chama cha makahaba?

Discussion in 'International Forum' started by Malafyale, Jun 25, 2009.

 1. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #1
  Jun 25, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,207
  Likes Received: 3,622
  Trophy Points: 280
  Week iliyopita gavana mwenye nguvu sana kiutendaji ndani ya chama cha Republican kutoka Nevada John Ensign alikubali hadharani na kuomba msamaha ka wamerkani wote kuwa alikuwa na uhusiano wa nje ya ndoa na mja wa wafanyakazi wake waliomsaidia kufanya kampeni ili kushinda tena U-seneta wa USA.Gavana Ensign alikuwa anachukuliwa kama mmoja kati ya watu nguli ndani ya Republican wenye uwezo wa kumuangusha Rais wa sasa Barack Obama;kwa kupatikana na kashfa ya ngono seneta Ensign sio tu hawezi kufukiria kuwania Urais wa USA bali hata ukisha muda wake wa useneta hawezi tena kufikiria kugombea,kiufupi ndiyo mwissho wake kisiasa!
  Leo tena yamezuka mapya,Mark Sanford ambaye ni gavana wa South Carolina kupitia tiketi ya Republican nae amekili sasa hivi kuwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamke mwingine aitwaye Maria anayeishi nchini Argentina.Sanford amekubali kuwa hata habari ya safari yake aliyo aga ofisini na nyumbani kwake week iliyopita kuwa anakwenda kwenye milima ya Appalachian kuwinda haina ukweli wowote bali alikuwa nchini Argentina kwa msichana wake huyo.Sanford amewataka wamerekani hasa familia yake imsamehe!
  Kukiri kwa gavana Sanford na seneta Ensign kujihusisha na ngono kunafanya idadi ya wana Republican vigogo kujihusisha na ngono kuwa watatu,kwani mwaka juzi seneta wa Idaho mzee Larry Craig alikamatwa na polisi kwenye vyoo vya uwanja wa ndege wa Minnepolis akidaiwa kutaka kufanya mapenzi kwa njia ya ulawiti.Craig akajiuzuru useneta wa Idaho na bado ana mashtaka ya kujibu mahakamani kosa la ulawiti!
  Kama ilivyo ada,wana harakati wamekwisha mtaka gavana Sanford ajiuzuru haraka nafasi zote alizonazo ikiwa na ile yenye nguvu kimaauzi ya uenyekiti wa magavana wa Republican hapa USA
  Ukumbuke tu ni kuwa Sanford alikuwa anachukuliwa pia kama mtu mwenye nguvu za ushawishi kiasi cha kuanza kushawishiwa kugombea Urasi mwaka 2012.kwa kukubali kuwa alikuwa anafanya mapenzi nje ya ndoa ndiyo mwisho wa safari ya gavana Sanford kisiasa!
  Bado ninajiuiliza na sipati jibu;kujihusisha na ngono kwa wanasiasa 3 mashuhuri sana kwa sasa ndani ya Republican ndiyo kusema chama hiki kilichowahi kutamba sana kwenye siasa za USA ndiyo kimejingiza rasmi na kujitangaza kama chama cha makahaba?Nini mwelekeo wa chama hiki kikongwe kabida duniani kilichoa asisiwa na mzee Abraham Lincoln karibu miaka 150 iliyopita?
   
 2. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #2
  Jun 25, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Na Democrats nao wamo. Kuna Clinton miaka ya tisini. Mwaka huu tu John Edwards nae alishikwa na kashfa ya uzinzi pia. Eliot Spitzer nae aliyekuwa govenor wa New York alikubwa na kashfa ya kutumia maelfu ya madollar kwa kulipia ngono iliyo pelekea ajiuzuru. Hii ilitokea mwaka 2007. Kwa hiyo sidhani kama this is a republican issue mkuu. Mimi nadhani uzinzi ni kitu kinacho fanywa na watu wengi sema kwa vile hawa wanasiasa ni public figures ndiyo maana soo zao zikitokea zinakuwa highly publicized.
   
 3. StaffordKibona

  StaffordKibona JF-Expert Member

  #3
  Jun 25, 2009
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 671
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ahasnte Mwanafalsafa; Ngono haina chama ni pepo la mtu mwenyewe
   
Loading...