Reposted

nakumbuka msimu wa kanda imeliwa basi sasa lazima uwe na kalamu ya biki ni mwendo wa kuanza kurudisha nyuzi za kanda huku unaipiga piga eti imekuwa nzito haipigi vizuri kweli kitambo
 
nakumbuka msimu wa kanda imeliwa basi sasa lazima uwe na kalamu ya biki ni mwendo wa kuanza kurudisha nyuzi za kanda huku unaipiga piga eti imekuwa nzito haipigi vizuri kweli kitambo
Radio zenye auto reverse ndio zilikuwa fasheni
 
Umenikumbusha mbali, natafuta picha yangu ya darasa la I, chini nimekula raba ya "Moroshuu"
 
Hahahhhh ni wachache sana hapa JF tutachangia hili. Enzi za utoto wetu. Moroshoe ilikuwa mkifungua shule kila mtu ana moroshoe na raba za Bata dah! Miaka imesonga. Kuna duka la viatu vya bata lilikuwa samora avenue.
 
Teh teh! Umenikumbusha enzi zile kuna baba yangu mdogo alikua kazitinga hzo laizoni afu kabeba kabox ka sabuni anatoka home kwetu anaenda kwa bibi kijijini,sasa si akakutana na mgambo enzi za uhujumu uchumi,akapatwa na hofu akalianzisha mbio kurudi pale home na mgambo wakalala nae mbele kumfukuza,yaani hata kusimlia sijui nisemeje maana sina mbavu nikikumbuka[emoji2] [emoji3] [emoji3] [emoji2] [emoji3]
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Mie nna urithi wa radio,ni model hii hii but nadhani ya nyuma kidogo na kulingana na maelezo ya bimkubwa father aliinunua 1980 me sijazaliwa bado.nikiendaga chaka sometimes natia battery nasikiliza huwa nafanya hivi kujifariji maana mzee wangu sikufanikiwa kumuona.
 
Betri za national deal kama kifurushi cha internet enzi hizo...

Ha ha haa kulikua na taaluma ya kuzichemsha ili kuzi bust zikianza kuishiwa nguvu. Finale ilikua kuzibonda bonda kidogo, baada ya kuzianika juani. Wahandisi wengine kama akuna mshana jr walikua wana njia ya kuzining'iniza kwenye choo ili ziendelee kupata chaji. I am seriously missing those days
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…