Toka nimuone wakati wa kampeni sijamuona tena. Labda tunapishana kila akija mimi sipo. Kwa ujumla TMK lililobadilika zaidi ya huo ujenzi wa barabara ya tandika kupitia yombo dovya hadi jet. Hata hivyo hiyo barabara ni nguvu ya Magufuli baada ya kuingilia kati kukagua yeye mwenyewe nyumba hadi nyumba na kugundua nyumba feki zaidi ya 65 zilizochomekwa kwenye report ya fidia. Maana ilikuwa inasumbua kuwa pesa zilizotengwa za fidia hazitoshi sababu ya hizo nyumba feki. Baada ya hiyo survey ndio malipo yakafanyika jumatatu iliyofuata na wakazi wakaanza kubomoa nyumba zao wenyewe kwa hiari baad akuchukua mshiko wao na ujenzi ukaanza bila shida. Kuna taarifa zisizo rasmi huku mtaani zinasema kwamba mbunge alikuwa na nyumba zake katika hizo feki.