Renatus Mkinga live ITV, malumbano ya hoja

Sijaona kosa na sio kila mpinga Serikali ya CCM avae Magwanda ya khaki anaweza kuwa humohumo au CUF hata TLP
 
Kwani unashangaa nini? Mbona hata Dr.Lwaitama ni CCM memba ijapo anaichana mwanzo mwisho?mbona Mzee Sabodo anadai yeye ni kada wa Tanu na CCM na bado anaichana CCM?

Mbona Filikunjombe anaichana CCM na yy ni mwanachama wao?Tafakari,chukua hatua.
dr rwaitama ni ccm 'mfu': maneno yake mwenyewe.
 
Sasa wewe unataka Tanzania iwe chadema,kila mtu anayo haki ya kujiunga na chama chochote cha siasa,anachofikiri kinao uwezo wa kuongoza
 
Ningependa kutoa ushauri kwa huyu mchambuzi asiye mchambuzi maarufu wa ITV.
Kwanza, ni vema afahamu kuwa katika kanuni za kuzungumza na kadamnasi,'public speaking skills'ni muhimu kutumia 'tone' inayo badilika-badilika kutegemea na muktadha.Kwa mfano sauti inayotumika kutoa mfano,itakuwa chini kidogo na kamwe haiwezi kuwa sawa na ile itakayotumika kuweka msisitizo ambayo aghalabu huweza kupanda kidogo.Yeye akiamini sauti ndio kila kitu,huanza na makele mwanzo hadi mwisho.Hali hii haiwezi kuvutia usikivu na umakini wa hadhira asilani.
Pili,hadhira makini,haipendi wazungumzaji wanaolazimisha masuala mahali pasipohusika.Kwa mfano,kwa kuzingatia mada iliyokuwa inajadiliwa, hapakuwa na umuhimu wala sababu kwa yeye kuanza kijinasibu kama mmoja wana CCM 'asilia' na kukandia wana CCM anaowaita 'maslahi'.
Otherwise ninamchukulia kama mtu dhaifu kifikra kwa hulka yake ya kukariri masuala ambayo hata hivyo juhudi zake hizo hazizai matunda ...kuwa na taarifa kichwani ni suala moja na kuzichanganua ni suala tofauti kabisa. Kwa hulka yake hiyo huishia kubwabwaja tu bila kuacha uchambuzi wowote wa maana unaongeza maarifa kwa hadhira.
Hoja zangu hapo juu hazina uhusiano wowote na chuki dhidi ya Chama atokacho muhusika.
 
Huyu kaka alikuwa na matatizo juzi juzi, na alihitaji msaada, fadhira hurudiswa kwa aina na kiasi tofauti.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom