Reli ya SGR ifike Zambia

Reli ya SGR ifike Zambia

davedas

Senior Member
Joined
Feb 18, 2015
Posts
173
Reaction score
130
Nchi ya Zambia ni moja ya mtumiaji mkubwa sana wa bandari ya Tz mwaka huu pekee amepitisha zaid ya ton 2M kweny bandar yetu ya Dar na hii ni pamoja na changamoto zote za bandari na umbali kutoka Dar hadi tunduma kwanjia ya barabara

Ningependa kuona tunampango wa kupeleka sgr uko sababu mizigo ipo mingi tu na wako na shauku kubwa sana na wao kuwa na reli ya kisasa ivyo kupelekea hata mwitikio wa kuunganisha reli yetu na zao kuwa rahis.
Ikumbukwe kuwa 2021 zambia walisaini mkataba na railnet kujenga sgr kutoka copper belt mpaka livingstone lakini ukicheck reli hii bado haina port connection ivyo kuifanya hata morali ya kujenga kupungua https://www.railwaysafrica.com/news/mosetse-kazungula-livingstone-railway-project-to-cost-us-1-5-billion sasa badala ya kusubiri mpaka S.A na Mozambique wamchukue kwanini TRC wasikae nao kujua wanawezaje kuunganisha na yetu ili kuokoa biashara ya bandari zetu maana mpaka sasa kuna mizigo mingi sana ya zambia inaenda S.A na mizigo mingi sana ya south drc ina pita uko wakati percent kubwa ilitakiwa kupita kwetu kama vile kenya anatufanya kwa Uganda..

Sasa siwezi kulaumu sana kwasababu bandari yenyewe ya Dar bado ni changamoto ila sababu tunaenda kujenga Bagamoyo port yenye uwezo wa kuingiza meli kubwa ambazo Dar haziwezi kuja ni bora kufikiria kupeleka sgr Zambia mpaka south Drc hii itapelekea hadi nchi kama zimbabwe na botswana kupitisha hata mizigo kidogo kwenye bandari zetu.

Najua kuna mazungumzo ili kuboresha Tazara (cape gauge) lakini Tazara limit yake mpaka sasa ni 5 M ton. kwa mizigo tu ya sasa iyo Tazara imeshazidiwa maana kwa DRC tunafika hadi 4M ton na hapo kuna mizigo mingi inaenda South..
IMG_3599.jpeg

Sasa kama kweli tunataka kuwa competitive na kufikia ule uchumi wa trillion 1 usd 2050 bhasi sgr ya kisasa itakayotoa foreni ya pale Tunduma ndo inatakiwa na sio kupanua barabara au kugharamia tena ujenzi wa kuitoa Tazara toka Dar mpaka bagamoyo wakati sgr /reli ya kisasa ishafika mpaka Dodoma karibu kabisa na mpaka wa Iringa kwenda mbeya mpaka Zambia

Uboreshaji wa Tazara wala sio kitu kibaya tena me naona tumechelewa sana kufanya hayo maboresho lakini kwa jinsi uchumi wa hizo nchi mbili zinakuwa ni dhairi kabisa mzigo hautatosha tunahitaji reli ambayo itapokea ongezeko la mizigo miaka mingi mbele ili kuwa competitive zaidi kwa bandari za S.A na Mozambique.
Ukitoa kuhudumia Zambia na South drc kufikisha sgr mikoa iyo itatusaidia kuweka urahisi wa kuunganisha sgr ya central corridor na ile ya mtwara to mbambabay na kufanya sekta ya uchukuzi Tz kuwa ya viwango vya juu maana

Mtu wa mwanza au Arusha anaweza kupanda train mpaka mtwara bila kushuka shuka, viwanda vya mtwara viwanaweza kuuza bidhaa zake kanda ya ziwa,uganda,kenya,burundi rwanda hadi south sudan uko..
Hata kukitokea shida kwenye bandari moja bhasi bandari nyingine zote zina support au hata foreni kwenye bandari moja nyingne zinaingia kusupport, hii itafanya itaongeza security kwenye sekta ya uchukuzi ivyo ivyo kuongeza ufanisi kwa nchi zinazotutegemea.

Uchumi wa 1 trillion usd tukifika 2050 unawezekana mungu ametupa vyote ni sisi tu kuamua na kuanza kuumiza ubongo..​
 
Back
Top Bottom