Mkoa mzima wa Singida tangu asubuhi ya leo umegubikwa na vigelele na vifijo. Kijani na njano vikiwa rangi Tawala kila kona. Barabara zimefungwa kwa bashasha na nderemo za vijana wenye sura zilizojaa furaha, na ari ya kujenga Nchi yao.
Haikuwa mechi ya Simba na Yanga, wala kombe la dunia la Qatar Singida, bali ni mapokezi ya Binti yetu lulu tuliyemzaa, kumlea na kumkuza Singida, si mwingine bali Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana wa Chama cha Mapinduzi Taifa (UVCCM), Rehema Sombi Omary.
Kwa msiojua, Bi. Rehema kwenye Uchaguzi wa Chama cha Mapinduzi uliofanyika ngazi zote nchini mwaka huu, alishinda kwa zaidi ya 80% ya kura zote katika nafasi ya Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Singida, hivohivyo kwa asilimia hizo alipogombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti UVCCM Taifa, huko nako aliwatoa kimasomaso washindani wake.
Bi. Sombi wakati wa mapokezi ya leo Singida hakuja peke yake. Aliambatana na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa ndugu Mohamed Ali Mohamed (KAWAIDA), Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa, Kenani Kihongosi pamoja na viongozi mbalimbali wa Chama Taifa.
Binafsi nilipofika Ukumbini majira ya adhuhuri nilijionea vijana wa rika mbalimbali, chipukizi, akina mama, na Wazee wakiburudika huku hata nafasi hata ya kukanyaga wala kuketi ikikosekana. Hii ilinipa salam moyoni kwamba Bi. Sombi ni nuru ing'aayo gizani na kwa hakika ametuheshimisha sana wana Singida.
Ukiachana na Viongozi wengi wa Chama na Serikali wa Mkoa Singida waliohudhuria; nilishangazwa kuona viongozi wa UVCCM kutoka miaka zaidi ya 10 ikiwemo Arusha, Mwanza, Manyara, Dodoma, Dar es Salaam, Iringa, Kigoma, Geita, Tabora (to mention a few) wamehudhuria huku wamebeba zawadi mbalimbali.
Hakika Rehema ametufana.
Katika hali isiyo ya kawaida, nimejikuta nikihemewa na kitendo cha mimi KUAGIZWA kuhama kutoka kwenye viti vya kawaida nilipoketi na mamia tuliohudhuria na kwenda kuketi "high table". Nawashukuru sana Mwenyekiti Kawaida, Makamu Mwenyekiti Dada yangu Rehema, Katibu Mkuu Kenani, pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Bi Sophia Mfaume. Asanteni sana.
Nawashukuru mno kwa kuniita high table na kunipa pongezi na kutia moyo kwa kutetea agenda za Chama na Serikali, kupambania Chama na kumsemea mema Mwenyekiti wetu Dkt Samia Suluhu Hassan bila kukata tamaa katika mitandao ya Jamii licha ya matusi na kila aina ya karaha ninayopatiwa na watesi wetu.
Aidha nikiri kufurahishwa na Hotuba zikizojaa ujasiri, ari mpya, na mwelekeo mpya wa UVCCM za Mwenyekiti Kawaida, Makamu Mwenyekiti Rehema na Katibu Mkuu Kenani. Hakika nyie ndiye nyuki na walinzi wakuu wa Chama chetu cha Mapinduzi.
Kama mlivyosema wazi wazi leo kwamba hamtakubali yeyote akishambulie Chama chetu na Viongozi wetu hususani Rais wetu Dkt Samia kama ambavyo Mwenyekiti Kawaida alivyorejea wale wanaozodoa ziara za nje, so be it. Binafsi nitawaunga mkono sana kwa vitendo popote nilipo, hususani kwa kujibu hoja mujarabu mitandaoni.
Ahsante Mwenyekiti wetu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Singida Mama Martha Mlata kwa kuhakikisha Chama Mkoa na Jumuiya zake zimewapokea vijana wetu hawa wa UVCCM kwa hadhi inayostahili. Mama umetoa Hotuba iliyojaa Ujumbe mzito kwa sisi vijana kujiamini na kusimamia ndoto zetu.
Mwenyekiti Mlata, shukrani pia kwa kumpatia jina jipya la Kinyaturu Mwenyekiti wa UVCCM, Ndugu Kawaida liitwalo "Majengo" likibeba tafsiri ya "Mjenzi", na isitoshe mkapatia na kiwanja cha kujenga ndugu Majengo hapa Singida Manispaa. Umetuheshimisha sana.
Kwa ujumla nikipongeze sana Chama changu cha Mapinduzi Mkoa wa Singida na Jumuiya zake hususani UVCCM kwa kuhakikisha shughuli ya kumpokea Rehema wetu imefanyika kwa kiwango cha kimataifa. Hakika mmeifanya CCM kisiwa cha raha na matumaini Makuu kwa kila MwanaCCM na Mtanzania.
Mdogo wangu Rehema, wana Singida hatuna cha kukulipa kwa heshima hii isiyomithilika uliyotuzawadia, mbwembwe na fahari yetu leo ni kwasababu yako. Umeheshimisha Chama, Umeheshimisha MKOA na Umeheshimisha wanawake na mabinti wote nchini. Hatuna zaidi cha kukupa zaidi ya kukushuru na kukuombea kila la kheri, uzidi kutung'arisha daima. TUNAKUPENDA SANA.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.
Suphian Juma Nkuwi,
MwanaCCM,
Desemba 18, 2022.
Singida.
Phone: 0717027973
Email :
yessuphian@gmail.comView attachment 2451271View attachment 2451272View attachment 2451273View attachment 2451274