Reginald Munisi akataa uteuzi wa CHAUMMA

Reginald Munisi akataa uteuzi wa CHAUMMA

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
26,662
Reaction score
59,100
IMG-20250526-WA0012(1).jpg

"Nashukuru kwa heshima ya kuteuliwa kuwa mtaalamu CHAUMMA. Ingawa nathamini sana imani yenu, majukumu yangu ya sasa yananilazimu kuchukua "Back Seat" kisiasa kwa wakati huu. Nawatakia Sekretarieti mpya na Chaumma utendaji uliotukuka!"

Awali John Mrema alitangaza kuteuliwa kwake
IMG-20250526-WA0016.jpg
IMG-20250526-WA0011.jpg
 
Nashukuru kwa heshima ya kuteuliwa kuwa mtaalamu CHAUMMA. Ingawa nathamini sana imani yenu, majukumu yangu ya sasa yananilazimu kuchukua "Back Seat" kisiasa kwa wakati huu. Nawatakia Sekretarieti mpya na Chaumma utendaji uliotukuka!
Huyo Mushi ni nani? Jee hataki kufanya kazi na Wachaga wenzake waliotoka Chadema?
 
97d88d81-98ce-4431-95d2-b7ca59829634.jpg

Aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Mikakati na Uchaguzi wa Chadema, Reginald Munisi amekataa uteuzi wa mtaalamu wa mikakati katika Chama cha Ukombozi wa umma (Chaumma), baada ya kutangazwa Mei 24, 2025.
Taarifa ya uteuzi huo uliofanywa na Kamati Kuu ya Chaumma ilitolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Mawasiliano na Uenezi wa Taifa, John Mrema.

Hata hivyo, Munisi ameandika katika ukurasa wake wa X (zamani Twitter) akisema atabaki mstari wa nyuma katika siasa.

“Nashukuru kwa heshima ya kuteuliwa kuwa mtaalamu CHAUMMA. Ingawa nathamini sana imani yenu, majukumu yangu ya sasa yananilazimu kuchukua "Back Seat" kisiasa kwa wakati huu. Nawatakia Sekretarieti mpya na Chaumma utendaji uliotukuka!”

Munisi alitangaza kujiondoa kwenye nafasi yake aliyokuwa akishika Chadema mara baada ya uongozi mpya wa Mwenyekiti Tundu Lissu, baada ya uchaguzi wa chama hicho uliomwondoa Freeman Mbowe aliyekuiongoza chama hicho kwa Zaidi ya miaka 20.

Tofauti na waliokuwa makada wa Chadema maarufu G55 waliotangaza kujiunga na Chadema, haijafahamika kama Munisi naye amejiunga na chama hicho.
 
Nashukuru kwa heshima ya kuteuliwa kuwa mtaalamu CHAUMMA. Ingawa nathamini sana imani yenu, majukumu yangu ya sasa yananilazimu kuchukua "Back Seat" kisiasa kwa wakati huu. Nawatakia Sekretarieti mpya na Chaumma utendaji uliotukuka!
Amekataa au ameona njia ya kutoboa hakuna
 
Amekataa kubariki ujambazi, najisi na dhambi kwa moyo wake wote huku akiwasupport kwa vijineno vya kinafiki. He did well.
 
Back
Top Bottom