MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,997
IppMedia ni kipimo halisia katika kufahamu ukweli wa mahusiano ya Reginald Mengi na watawala wa Tanzania.
Tarehe 3 Desemba 2015 ilikuwa ni siku ambayo ilibadilisha mahusiano ya Reginald Mengi na watawala wa Tanzania. Hii ilikuwa ni siku ambayo Rais Magufuli alikutana kwa mara ya kwanza na wadau kutoka Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) chini ya Mwenyekiti wake Reginald Mengi, jijini Dar es Salaam ambapo walijadili umuhimu wa sekta binafsi katika kukuza uchumi na wajibu wa Serikali kutengeneza mazingira wezeshi.
Ikumbukwe kuwa katika kampeni za Uchaguzi Mkuu 2015, IppMedia ilikuwa kwa uhalisia inapigia chapuo UKAWA.
Sifahamu ni masuala gani Rais Magufuli na Mzee Mengi waliongea na kukubaliana lakini ninachofahamu ni kuwa, siku hiyo ilikuwa ni mwanzo wa IppMedia kubadilisha mahusiano na mtazamo wa habari kuhusu serikali ya Awamu ya Tano.
Kwa sasa huwezi kusoma habari kutoka IppMedia ambayo ni hasi kuhusiana na serikali ya Awamu ya Tano.
Kwa sasa huwezi kuona habari ya mtu au mwanasiasa anayemponda Rais Magufuli ikiandikwa au kutangazwa kwenye IppMedia.
Mahusiano ya karibu kati ya Mzee Mengi na Rais Magufuli yamefanya hata Prof. Muhongo kubadilika. Ikumbukwe Mzee Mengi na Prof. Muhongo walikuwa mahasimu katika utawala wa awamu ya nne.
Mzee Mengi is putting his money where his mouth is by dissociating from Pres Magufuli’s critic, haters and losers.
Kama mazingira yataendelea kama yalivyo, kuna uwezekano mkubwa wa Mzee Mengi kunufaika sana na utawala wa Awamu ya Tano.