Reginald Mengi na Utawala wa Rais Magufuli

IppMedia ni kipimo halisia katika kufahamu ukweli wa mahusiano ya Reginald Mengi na watawala wa Tanzania.

Tarehe 3 Desemba 2015 ilikuwa ni siku ambayo ilibadilisha mahusiano ya Reginald Mengi na watawala wa Tanzania. Hii ilikuwa ni siku ambayo Rais Magufuli alikutana kwa mara ya kwanza na wadau kutoka Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) chini ya Mwenyekiti wake Reginald Mengi, jijini Dar es Salaam ambapo walijadili umuhimu wa sekta binafsi katika kukuza uchumi na wajibu wa Serikali kutengeneza mazingira wezeshi.

Ikumbukwe kuwa katika kampeni za Uchaguzi Mkuu 2015, IppMedia ilikuwa kwa uhalisia inapigia chapuo UKAWA.

Sifahamu ni masuala gani Rais Magufuli na Mzee Mengi waliongea na kukubaliana lakini ninachofahamu ni kuwa, siku hiyo ilikuwa ni mwanzo wa IppMedia kubadilisha mahusiano na mtazamo wa habari kuhusu serikali ya Awamu ya Tano.

Kwa sasa huwezi kusoma habari kutoka IppMedia ambayo ni hasi kuhusiana na serikali ya Awamu ya Tano.

Kwa sasa huwezi kuona habari ya mtu au mwanasiasa anayemponda Rais Magufuli ikiandikwa au kutangazwa kwenye IppMedia.

Mahusiano ya karibu kati ya Mzee Mengi na Rais Magufuli yamefanya hata Prof. Muhongo kubadilika. Ikumbukwe Mzee Mengi na Prof. Muhongo walikuwa mahasimu katika utawala wa awamu ya nne.

Mzee Mengi is putting his money where his mouth is by dissociating from Pres Magufuli’s critic, haters and losers.

Kama mazingira yataendelea kama yalivyo, kuna uwezekano mkubwa wa Mzee Mengi kunufaika sana na utawala wa Awamu ya Tano.

itv wameonyesha live gen. ulimwengu anaiponda serikali ya magufuli imeturudisha miaka 50 nyuma afu wewe unadanganya watu hapa habari mbaya za serikali hazituki ipp media!
 
Kwa mara ya kwanza nimeona itv leo ikiomba radhi kuhusu kipindi cha mahojiano na Msigwa.
 
IppMedia ni kipimo halisia katika kufahamu ukweli wa mahusiano ya Reginald Mengi na watawala wa Tanzania.

Tarehe 3 Desemba 2015 ilikuwa ni siku ambayo ilibadilisha mahusiano ya Reginald Mengi na watawala wa Tanzania. Hii ilikuwa ni siku ambayo Rais Magufuli alikutana kwa mara ya kwanza na wadau kutoka Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) chini ya Mwenyekiti wake Reginald Mengi, jijini Dar es Salaam ambapo walijadili umuhimu wa sekta binafsi katika kukuza uchumi na wajibu wa Serikali kutengeneza mazingira wezeshi.

Ikumbukwe kuwa katika kampeni za Uchaguzi Mkuu 2015, IppMedia ilikuwa kwa uhalisia inapigia chapuo UKAWA.

Sifahamu ni masuala gani Rais Magufuli na Mzee Mengi waliongea na kukubaliana lakini ninachofahamu ni kuwa, siku hiyo ilikuwa ni mwanzo wa IppMedia kubadilisha mahusiano na mtazamo wa habari kuhusu serikali ya Awamu ya Tano.

Kwa sasa huwezi kusoma habari kutoka IppMedia ambayo ni hasi kuhusiana na serikali ya Awamu ya Tano.

Kwa sasa huwezi kuona habari ya mtu au mwanasiasa anayemponda Rais Magufuli ikiandikwa au kutangazwa kwenye IppMedia.

Mahusiano ya karibu kati ya Mzee Mengi na Rais Magufuli yamefanya hata Prof. Muhongo kubadilika. Ikumbukwe Mzee Mengi na Prof. Muhongo walikuwa mahasimu katika utawala wa awamu ya nne.

Mzee Mengi is putting his money where his mouth is by dissociating from Pres Magufuli’s critic, haters and losers.

Kama mazingira yataendelea kama yalivyo, kuna uwezekano mkubwa wa Mzee Mengi kunufaika sana na utawala wa Awamu ya Tano.
Nimeshangazwa na huu uzi wako.
Mimi mtazamo wangu ni kwamba ITV inatangaza habari zote. Za wapinzani na za chama tawala.
Kwa mfano leo wame tangaza habari ya Tundu Lisu baada ya kutoka mahakamani vizuri sana. Sasa nashangaa unavyosema hawatangazi habari za watu wanaopinga chama tawala.
Fanya research yako vizuri. Nadhani huo ni mtazamo wako kuliko hali halisi ilivyo.
 
Back
Top Bottom