Reginald Mengi amwaga Bilioni kwa WAMA

Reginald Mengi amwaga Bilioni kwa WAMA

IsangulaKG

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2010
Posts
706
Reaction score
386
Katika hali iliyowashangaza wengi akiwamo Rais Kikwete na Mkewe Mama Salma ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA, Mzalendo na mmiliki wa makampuni ya IPP Bwana Reginald Mengi ameahidi kutoa Tshs Bilioni moja kwa kutoa mil 200 kila mwaka kwa miaka mitano ili kuipa support shule ya WAMA Nakayama iliyopo Rufiji.

Shule hiyo ambayo imefanya mahafari yake ya kwanza kwa kidato cha nne leo hutoa full scholarship kwa wasichana waliotoka katika mazingira magumu na hatarishi.

Akiongea kumshujuru Mengi,Rais Kikwete alisema anamfahamu Mengi na wameshrikiana kwa mambo mengi hata kabla hajawa Rais. Mengi pia aameelezea kukunwa na Mama Salma Kikwete na Taasisi ya WAMA kwa kuwajali mabinti masikini kwani naye amekulia katika umasiki na anaufahamu vilivyo.

Mimi si mshabiki wa Serikali hii lakini kwa hili la WAMA kuwasaidia mabinti wenye mazingira magumu mama huyu anastahili pongezi

.Kwa mara ya kwanza nimesikiliza hotuba ya shule ambayo haijatoa ombi kubwa kwa Rais na waziri wa elimu ya kwamba changamoto zilizopo shule imejipanga kukabiliana nazo.

Hivi ndivyo shule zote zilitakiwa kuwa...zimejitoshelesha ili kutoa fursa sawa kwa wote kwani imebainika baadhi ya wilaya zinafanya udanganyifu na kuwachomeka watoto wa wakubwa hivyo kuwanyima fursa mabinti masikini na mayatima.
 
milioni 200x5 = 1 billion ambayo ni sawa na ile bei ya tender doc za vitalu vya gesi

Inaonekana washauri wa Mengi nao sio makini maana after 2 years JK atakuwa nje na pale white house atakuwepo mtu mwingine. sasa cha kujiuliza kama kweli Mengi angekuwa anajua kucheza Chess angetoa hiyo cheque ya Bilioni 1 leo leo halafu halafu anyamaze kimyaaaa....najua ikifika jioni Muhongo mwenyewe atampigia ili wafanye ''private conversation'' on vitalu na mengineyo.
 
Mmmmmmh ! Kwa nini asitoe zote kabsa yaishe
 
isije ikawa ni hongo apewe vitalu vya mafuta na gesi

just thinking outside the box

wachaga ni watu wapenda maendeleo sana, pamoja na kudhalilishwa na kuitwa masikini huku wakidhaminiwa wageni, bado ameendelea kuwatumikia na kuwasaidia wapiga kura wa kikwete! wauziwa vitalu vya gesi wapo wapi? poor my government! HONGERA MZEE MENGI!
 
Mwenyekiti wa makampuni ya Ipp bwana Reginal Mengi leo akihudhuria ktk mahafali ya kidato cha nne ktk shule ya Wasichana iitwayo Mama Salma Kikwete Mkoani pwani,ametoa ahadi ya sh bilion 1km mchango.

Akizungumza na Wanafunzi wa shule hiyo amesema kuwa kwa kumuunga mkono Mama Salma Kikwete atakuwa akichangia kila mwaka sh milioni 200 kwa muda wa miaka 5!!

Chanzo;Itv habari saa 2
 
Ha ha haaaa jamaa anawagawia hela ya kuuza matunda! Yaani Maswi saa hii hoooi! Muuza matunda bana!
 
Elimu ya Tanzania sasa imeingia katika mtizamo wa kimakundi.
Leo ITV wametuonesha mama Salma akiungwa mkono na Mengi kuchangia shule moja, moja tu Bilioni 5. Akimaanisha Milioni 200 kwa Mwaka.
Chanel 10 wao saa 1 wameonesha Lowasa katika harambee ya shule za kata na akatoa Mil 10, na jumla ya pesa yote ni takriban Mil 200 si kwa shule moja, kama 7 hivi za Kigamboni.
Wadau kama nimekosea nisaidieni.
Hoja yangu ni kuwa hivi hiyo shule ya Mama Salma itachukua wakina Kayumba wote tz wafaidi hayo mahela ya Mengi?
Kikwete amemsifia Mengi anahuruma na wa tz, je angezitoa hizo kama madawati kusambaza Tz nzima hiyo huruma si tungeiona?
Mama Salma, tumeona hizo pesa, vp usaili wa watoto wetu kuja shule ya WAWAMA si fomu mtatuuzia Mil 1? Sisi hatuna ela, jiandae tunaleta watoto na pesa ni za Mengi.
Kwako Lowasa...pole kwa kusimama kuchangisha sh mia tano tano hadi kufikia Mil 200..nimeona wananchi wakipita kuchangia.
Hoja ya tatu, nimesubiri ITV mtangaze Lowasa nae kachangisha pesa kusaidia shule za kata kama 7 hivi..labda sikuona. Ni kwa nini wakati ni kawaida yenu.
Enyi Matajiri na Enyi Masikini Mlizaliwa uchi na mtarudi mavumbini uchi.
 
Mengi atakumbukwa kwa mengi... Matajiri wengine sijui misaada yao wanatoaga wapi...
 
Hawa vijisent hatuwasikii ktk haya. Pesa zao zinafanya nini? any way kutoa ni moyo...Mengi atazidishiwa mara mia, biblia yangu inaniambia apandacho mtu ndicho atakacho vuna. Anapamda wema, ufadhiri....
 
Wanaowajali yatima na wajane watapendwa na Mungu... Wale watoto wanaosoma Wama ni yatima.. Hivyo ni jambo jema,,,
 
Hela za muuza juice na soda hizo? Mengi bwana kweli ana mengi....hongera zake maana kasaidia jamii kwa mda mrefu sana japo yule waziri anamdharau utadhani ana beef nae kama lile la marsha
 
Ul-Masjid al-harkat al-mujahideen.

Niulize kwa nini matajiri wetu wengi hatuwaoni wakijitolea kusaidi mayatima na maskini kama afanyavyo Mengi? Hivi tungekuwa na wazawa wa 5 dizaini ya Mengi tungekuwa wapi? Hivi hawa wengine si wazawa?
 
Niulize kwa nini matajiri wetu wengi hatuwaoni wakijitolea kusaidi mayatima na maskini kama afanyavyo Mengi? Hivi tungekuwa na wazawa wa 5 dizaini ya Mengi tungekuwa wapi? Hivi hawa wengine si wazawa?


Sijui ila nasikia SSB hutoa misaada yake kila Ijumaa na vigezo anavijua yeye mwenyewe.
 
Ni kawaida ya freemason. Secret societies ni kawaida yao kwenye masuala ya kijamii.
 
Enyi Matajiri na Enyi Masikini Mlizaliwa uchi na mtarudi mavumbini uchi.
 
Back
Top Bottom