Redio Free ondoeni masafa yenu Dodoma

Stayfar

JF-Expert Member
Jan 11, 2016
1,066
2,214
Redio Free Africa mnakera sana, huku Dodoma. Yaani redio yenu kila siku ni kwikwi. Hakuna msikilizaji anapenda tena kuwasikiliza japo kuwa baadhi ya vipindi vyenu ni vizuri, lakini imekuwa kero. Matangazo hayasikiki kwa sababu sauti za watangazaji hazina tofauti na mtu mwenye kwikwi.

Bora mfunge masafa yenu huku Dodoma, mkabaki na sehemu ambazo mnasikika vizuri. Sielewi TCRA kwa nini wanawafumbia macho badala ya kuwanyang'anya masafa na kugaia Redio zingine zenye uhitaji. Huku mnapatikana kwenye FM 89.0, Bora namba hiyo wakapewa hata Wasafi FM, nyie mmeshindwa kuboresha.

Fungasheni muende zenu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Radio Free kitu pekee walibaki nacho sasa ni hazina ya nyimbo mbalimbali ambazo wametunza kwenye computer zao.
 
Pitia hapa pia...
 
Stayfar,
Yaani RFA katika Jiji hilo ni kama imekufa. Ina kwikwi isiyopona na hakuna juhudi zozote zinazochukuliwa kukabilina na hali hii. Tatizo jingine ni kuwa imesongwa na radio nyingine za FM ambazo zimeibuka kama uyoga katika Jiji hilo. Wahusika wa ugawaji wa masafa ya FM nao wanahusika katika hili.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom