Recruitment agents zimeruhusiwa?

Recruitment agents zimeruhusiwa?

mambucha

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2013
Posts
279
Reaction score
160
Kuna wakati serikali ilipiga marufuku recruitment agents lakini kila siku naona wanatangaza kazi , mfano HR solutions, jobmakini, cv people, radar n.k. Lile agizo la serikali vp?
 
Kuna wakati serikali ilipiga marufuku recruitment agents lakini kila siku naona wanatangaza kazi , mfano HR solutions, jobmakini, cv people, radar n.k. Lile agizo la serikali vp?

mambucha; Umewasahau Vipaji Link yaani Mmmh sina la kusema kuhusu Ndugu zangu wale.Mungu awasamehe kusema ukweli.
 
Last edited by a moderator:
mie kuna hawa Genius consultancy walinipigia simu baada ya salam ananiuliza natakilipwa kiasi gan,nlopo mjibu kati ya laki 4 mpaka 7 akakata simu,cjui alitegemea nmjibu laki na nusuuu au niseme pesa yoyote walio nayo???unyonyaji ufike mwisho sasa hata kama ajira n ngumu
 
Ni kweli serikali ipo kimya kuhusu hii issue,hivi hakuna wanasheria ili tuwashitaki hawA wanyonyaji
 
Kiukweli tanzania inakuwa kwani hazikuwepo ila kuwepo kwao kunaleta mabadiliko chanya ba hasi pia ila naam tutambue kuwa hata nchi za wenzetu hizi kampuni zipo ila tu sisi wananchi wenyewe tunahitaji kuwa makini katika mapokeo ya vitu vigeniiiiiiiii.......................................
 
Kuna wakati serikali ilipiga marufuku recruitment agents lakini kila siku naona wanatangaza kazi , mfano HR solutions, jobmakini, cv people, radar n.k. Lile agizo la serikali vp?

Ww hii serikali ipo mifukoni mwa watu
 
Waziri Kabaka alikuja na mikakati ya nguvu ya kuzuia hawa mawakala wanaotafutia watu ajira na kuendelea kuwaajiri. Sasa naona kimya hadi bunge la budget limepita kimya tu na mawakala bado wapo tu. Kama Erolink wameganda tu VODA lakini airtel nasikia wapo kwenye mchakato wa kuwahamisha wafanyakazi toka kwa mawakala kwenda kwa airtel japo wamepunguza watu kazini kwa kuwaachisha kazi kwa lazima. Mama Kabaka aliangalie hili ni unyonyaji au ndo mpaka uchaguzi ukaribie.
 
The thing ni zsisi vijana tunaonyonywa nguvu zetu tuandamane mpaka kwa wazir wa kazi tujue nini hatma yetu,maana hao agents wanachezea maisha yetu,tusome kwa tabu halafu bado tunyonye Na wachache hili halivumiliki,tupange mkakati wa kuhamasishana tuandamane
 
Kiukweli tanzania inakuwa kwani hazikuwepo ila kuwepo kwao kunaleta mabadiliko chanya ba hasi pia ila naam tutambue kuwa hata nchi za wenzetu hizi kampuni zipo ila tu sisi wananchi wenyewe tunahitaji kuwa makini katika mapokeo ya vitu vigeniiiiiiiii.......................................

ndugu Mwananchi, kila jamii inahitaji mabadiliko, yes serikali kwa kutambua hilo ililuhusu kuwapo kwa makampuni ya namna hiyo kuwasaidia job seekers kupata kazi. the problems came, hayo makampuni yalianza kuwanyanyasa watu yanaowapa kazi, mishahara to some company halipwi na mwajili bali analipwa na haya makampuni kama dalali vile. take MAKAMPUNI YA ULINZI KWA MFANO, MWAJILI ANALIPA LAKI 6 (600,000) KWA MFANO, BUT MLINZI ANAKUJA PATA ELFU 80/90/ KWA MWEZI KULINDA USIKU.
hata haya makampuni yamekuwa hivo hivo, halafu hata some haki nying waajiliwa hawapati, na wengine wanafanyishwa kazi kwa mikataba mifupi wakati mwajili anahitaji long employment.
IT WAS VERY NICE FOR SERIKALI KUZUIA HIZI COMPUNI
 
Mimi kuna watu wanaitwa Neema rec ruitment agency walininiibia sana, I hate them...
 
Ziendelee kuwepo zinasaidia sana upatikanaji wa ajira big up agency zinazosaidia vijana tumepata ajira
 
  • Thanks
Reactions: OMJ
Tamko la Jana tar 8/09/2014 kuhusu mawakala kuendelea kuajiri wafanyakazi wanaowatafutia kazi.
Msemaji wa Wizara hiyo Bw. Ridhiwani Wema, amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akitangaza uamuzi wa serikali wa kutoa leseni za usajili wa makampuni ya uwakala wa ajira.
Kutangazwa kwa usajili mpya wa kampuni za uwakala na huduma za ajira kunafuatia kuisha kwa zuio lililowekwa na serikali dhidi ya kampuni hizo ambazo baadhi yake zilikuwa zinatuhumiwa kukiuka taratibu za uwakala wa ajira.
Wema amesema makampuni ambayo yamepatiwa usajili wa kufanya kazi ya uwakala wa ajira, hayatakiwi kufanya kazi zilizo nje ya majukumu waliyopewa ikiwemo kupokea mishahara na stahiki nyingine za ajira kwa niaba ya watu waliowatafutia kazi kwani stahiki za ajira ni mkataba wa pande mbili na sio tatu kama baadhi ya makampuni yalivyokuwa yanafanya.
Akifafanua kipengele hicho, Wema amesema baadhi ya makampuni yamekuwa yakijitangaza kutafutia watu ajira lakini badala yake zimejigeuza kuwa waajiri kwa niaba ya kampuni hizo ambapo mishahara ya waliowatafutia kazi hupitia kwao na kuanza kuipunguza, kitendo alichodai kuwa ni kinyume na taratibu za ajira.
 
:moony:Ni kweli ndugu yangu kampuni hizi zimechangia sana katika uhaba wa ajira na kwa kiasi kikubwa sekta binafsi imeajiri watu wengi wasiokuwa na sifa na kulipwa mishahara mizuri huku ufanisi wa kazi ukipungua na kuasili hali ya uchumi.Nazani kuna haja ya wizara ya kazi kuweka sera nzuri kwani sekta ndio inachasngia ajira kwa kiasdi kikubwa kuliko serikali kama ikiangaliwa vizuri nazani tatizo la ajira litapungua kwa kwa 50%.
 
Mi acha tu niendelee kuwa mtazamaji
Im tied mwaka wa 4 huu kitaa
 
Back
Top Bottom