Recruitment agents zimeruhusiwa?

Recruitment agents zimeruhusiwa?

Kuna wakati serikali ilipiga marufuku recruitment agents lakini kila siku naona wanatangaza kazi , mfano HR solutions, jobmakini, cv people, radar n.k. Lile agizo la serikali vp?

recruitment agents zinaruhusiwa kufanya interviews kwa niaba ya mwajiri,kuitangaza kazi lakini sio kumiliki wafanyakazi
 
Watakuwa wameshatembeza rushwa wizarani sasa wameachiwa wapete tu na kuwanyonya na kuwakandamiza watafuta ajira. Wanaijua Tanzania ni nchi ambayo penye udhia tia rupia, mambo yako yanakunyookea.

Tamko la Jana tar 8/09/2014 kuhusu mawakala kuendelea kuajiri wafanyakazi wanaowatafutia kazi.
Msemaji wa Wizara hiyo Bw. Ridhiwani Wema, amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akitangaza uamuzi wa serikali wa kutoa leseni za usajili wa makampuni ya uwakala wa ajira.
Kutangazwa kwa usajili mpya wa kampuni za uwakala na huduma za ajira kunafuatia kuisha kwa zuio lililowekwa na serikali dhidi ya kampuni hizo ambazo baadhi yake zilikuwa zinatuhumiwa kukiuka taratibu za uwakala wa ajira.
Wema amesema makampuni ambayo yamepatiwa usajili wa kufanya kazi ya uwakala wa ajira, hayatakiwi kufanya kazi zilizo nje ya majukumu waliyopewa ikiwemo kupokea mishahara na stahiki nyingine za ajira kwa niaba ya watu waliowatafutia kazi kwani stahiki za ajira ni mkataba wa pande mbili na sio tatu kama baadhi ya makampuni yalivyokuwa yanafanya.
Akifafanua kipengele hicho, Wema amesema baadhi ya makampuni yamekuwa yakijitangaza kutafutia watu ajira lakini badala yake zimejigeuza kuwa waajiri kwa niaba ya kampuni hizo ambapo mishahara ya waliowatafutia kazi hupitia kwao na kuanza kuipunguza, kitendo alichodai kuwa ni kinyume na taratibu za ajira.
 
  • Thanks
Reactions: OMJ
Watakuwa wameshatembeza rushwa wizarani sasa wameachiwa wapete tu na kuwanyonya na kuwakandamiza watafuta ajira. Wanaijua Tanzania ni nchi ambayo penye udhia tia rupia, mambo yako yanakunyookea.

Waulize waliotafutiwa kazi na recruiment agency iliyona mifumo sahihi isiyo ya kinyonyaji watakuambia raha yake.
 
Hizo agencies si zinafanya kazi kama PSRS tu? Kwamba zinatoa matangazo na kufanya usaili kwaajili ya makampuni. Ila kumiliki wafanyakazi sio vizuri at all. Serikali itoe tangazo vizuri sio kutuficha ficha..
 
Sasa hao cha mtoto wapo Vipajilink pale maeneo ya victoria..............weeeee!!
 
"...ukitaka kula lazima ukubali kuliwa, japo kidogo..."
 
Back
Top Bottom