Record Label ya Ali Kiba

Habibu B. Anga

JF-Expert Member
May 7, 2013
6,557
25,716
Naona kama watu wamezidi kumuandama msanii wetu pendwa na self proclaimed king of bongo fleva Mr. Aki kiba.. Watu wanamzonga zonga kisa tu Dee lebo yake inapaa kwa mwendo kasi wakati Ali eti (narudia 'eti') hana lebo.. Inaonekana watu wameanza kufuatilia mambo juzi juzi hawajui tulikotoka.. Kwa wasiofahamu Ali ndio moja ya wasanii wa mwanzo kabisa kuwa na lebo yake, iliitwa AFTER THE MIDDLE FINGER INC.. nakumbuka alishirikiana na mtanzania fulani hivi anaishi marekani wakaianzisha pamoja.. Hii ilikuwa ni 2010.!

Bado sijafahamu ni nini hasa kiliikumba hii lebo lakini nahisi ilishakufa hata kaburi lake halijulikani lilipo.. Ninachotaka kusema ni kwamba muacheni Ali apumzike sio kumzonga aanzishe lebo kitu ambacho kilishamshinda na akaamua kuachana nacho.. Yeye ni msanii anajua kuimba suala la kuwa na lebo inahitaji uwe na management skills, sasa kama mwenzenu hana management skills mnataka afanyaje??? Dee ni dhahili amejaliwa kipaji cha kuimba na pia amejaliwa akili ya biashara.. Ali hajajaliwa akili ya biashara kwahiyo hebu acheni kumuandama eti aanzishe lebo! Alishashindwa huko, AFTER THE MIDDLE FINGER INC. ilishazikwa..

Acheni kumuandama eti anajivunia kusainiwa kwenye lebo ya Sony wakati mwenzie ana lebo ambayo iko mbioni ku-take over Africa.. Ali amefuata ushauri alioutoa Dee juzi kwenye kipindi cha XXL, Dee alisema, nanukuu "... Mfano Sallam hapa labda ana mpango wa kununua Prado, lakini Harominse hapa yeye amenunua Mark X na kwake hiyo ni hatua kubwa, so kila mtu ana level yake ya mafanikio..."
Hizo level za kuwa na lebo za mwendo kasi Ali alishazishindwa na ndio maana hataki mumpotoshe tena aanzishe lebo... Hebu muacheni na "Mark X" yake (kusainiwa Sony) na mwacheni Dee na "Prado" yake (WCB ya mwendi kasi)

Yote maisha tu.. Ali kaza mwanangu!!

f27187228f260cca230a3205c5a83af9.jpg
 
This dude Kiba is Overstated...... his influence currently in the game is too weeeeaaakkkkk.....

only that his fans are blind....
Ndi uwezo wake huo kiongozi!! Juhudi hazizidi kudra.. Mnampa stress sana kumtaka ashindane na wasanii wakubwa afrika wakati hajafikia huko bado..
 
Eti kwa mfano hapa "sallam anataka kununua Prado,lakini Harmo kanunua Mark x ni mafanikio kwake kila mtu ana levo zake za mafanikio" Huyu kweli wa Tandale kashindikana.
 
Eti kwa mfano hapa "sallam anataka kununua Prado,lakini Harmo kanunua Mark x ni mafanikio kwake kila mtu ana levo zake za mafanikio" Huyu kweli wa Tandale kashindikana.
Hahahahahh!! Falsafa za kitaa
 
Hahahah!! Heshima yako kiongozi.. Inawezekana wewe umenielewa zaidi
kama nakuona vile ambapo imekubidi ukaitafute hiyo video youtube, kisha ukasubiria hiyo sehemu uka-screenshot then ukaja tena jf ukai-paste, si mchezo mkuu safi sana!
 
kama nakuona vile ambapo imekubidi ukaitafute hiyo video youtube, kisha ukasubiria hiyo sehemu uka-screenshot then ukaja tena jf ukai-paste, si mchezo mkuu safi sana!
Asante sana mkuu!! Juhudi zote hizo ni katika kuhakikisha raia wanafahamu uwezo wa kingi..
 
Back
Top Bottom