Rebeca Gyumi unaninyima usingizi

Malingumu

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
616
429
Acha tu niseme jamani..huyu Dada kwa kweli moyo wangu unamsumbukia sana. Nimefaiti kukutana naye lakini mpaka sasa sijafanikiwa..Rebecca naomba ujue kuwa Mimi nakosa usingizi kwa ajili yako. Huko uliko naamini hujui,na wala mi sijui kama unapanga nini katika idara hii ila tu niseme toka moyoni na toka katika uvungu kabisa wa mtima wangu..nakukubali sana! You are a kind of a woman I want..yani huwa nikiangalia picha zako nabaki tu na 'I can only imagine'.

969409_10152340360110278_2084266052_n.jpg


Naamini kupenda siyo dhambi maana upendo ndiyo amri kuu tuliyopewa wanadamu. Nakupenda si kwa sababu wewe ni maarufu,nakupenda si kwa sababu wewe ni mwanaharaki ,nakupenda si kwa sababu ya mwonekano wako(though wakati mwingine swaga zako hunivuruga). Nakupenda zaidi ya hivyo vyote 'mama'.
Naomba mmwambie Rebecca huko aliko kama atapata muda angalau apite huku asome tu hii thread na akiweza akomenti hata kwa neno moja tu nami moyo utatulia kidogo.

Wahenga walisema huba mwanzowe jicho, nakubali kabisa maana tangu nimekuona pale Ubungo Plaza kwenye event ya "Kijana komaa na katiba" moto wa kukupenda ulichocheka zaidi moyoni mwangu,nami sasa ninakubali kabisa kuwa unaniunguza (my heart is on fire).

REBECCA.jpeg


Rebecca ninayo mengi ya kusema ila nitayasemea wapi na sijakuona..ni kama samaki majini...
jamani mwambieni aje angalau asome hata ajue kuwa kuna kijana ANAYEJIELEWA ambaye hasinzii wala halali sababu yake...
da!!! huwa nauzuia moyo kupenda ila kwa Rebecca nimechemka.
Rebeca umeniteka.!!!!!
 
Sijawah Hata Kuwaza Kma Nitafikia Steji Yako Mkuu, Hongera But Jikaze Kiume...Mtafute Mmayamalize.
Kma Vip Weka Na Kapicha Me Simjui Bhaanaa...Ila Nina Kismati Naweza Kukusaidia.
 
Ukiona vyaelea baba ujue vimeundwa, tafuta na wewe mkulima wako mfanyie setting zote atatoka kuliko Rebeca, mpaka umuone Rebeca hivyo kuna watu wamechakaa akili mpaka mifuko, wewe unataka kucheza na ngonjera na mashairi yakutoe!! Utalalapo.
 
kwani huna namna nyingine ya kuwasiliana naye mpaka utangaze humu...?
 
Ukiona vyaelea baba ujue vimeundwa, tafuta na wewe mkulima wako mfanyie setting zote atatoka kuliko Rebeca, mpaka umuone Rebeca hivyo kuna watu wamechakaa akili mpaka mifuko, wewe unataka kucheza na ngonjera na mashairi yakutoe!! Utalalapo.

Kwani Kete Ngumu ni lazima kila saa ufanye mambo yawe magumu?
 
Ni changamoto tu mkuu, hatuwezi kukushauti jambo moja wote, wengine tunajaribu kukuandalia plan B usije ukajinyonga ndugu yangu.
 
Huu utongozaji mwingine wa kibaya sana aiseeee.....
Yaani unataka kusema if you really love her, unashindwa kumtafuta...!?
Ebu ngoja kwanza niwaze kwa akili kubwa.....
Kwa mfano mimi nimejikuta moyo wangu umempenda mdada yeyote, kweli nitashindwa kumtafuta na kumueleza haja ya moyo wangu kweli ....?
Agghhhh.....
Hizi sim zimetuharibia watoto wa kiume kabisa kwa kusababisha ongezeko la madomo zege na nilio vya wavulana
 
Sura ya huyu mwanadada nahisi nimeshaiona pale Law Collection.

Hadi anakukataa alikua na sababu zake, kwahiyo mpotezee tu. Hujui Mungu anakuepushia nini au anamuepushia nini dada wa watu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom