Real Madrid (‎Los Blancos) | Special Thread

Mi nilishangaa alivyomtupa Bellingham pembeni nilichoka sana,afu kati viungo wagumu wote.kama vipi arda awe anaanza afu jude ajichange ila ndo hivo kocha ni kama ana uwoga flani ivi.
 
Mpangilio ni huh hapa.

Kabla ya mechi kuanza atoke nani aingie nani?
 

Attachments

  • FB_IMG_1729619230272.jpg
    103.5 KB · Views: 20
Usengerema huu maninaaa...yale yale ya miaka ya Lewando yanajirudia...Miltao anangalia mpira unampita mbele maninaa....hii timu tulisema ipo siku tutapata aibu ya mwaka,ngoja El clasico uone vile tutapigwa kama ngoma😡😡🤬...timu inacheza utasema haina kocha.
 
Hakuna timu hapa. Toka msimu umeanza hii timu mbovu hakuna improvement yeyote ile. Ujio wa Mbappe na kustaafu kwa Kroos kumeondoa balance ya timu. Tunatoka kapa msimu huu. Hakuna timu hapa.
 
HT: Tumecheza hovyo,timu utasema haijafanya mazoezi ya pamoja,kila eneo kila mtu anacheza kivyake,watu wanajipigoa cross mradi tu mpira utoke mguuni,tumeshindwa kupangua kabisa ngome za hawa jamaa kwa sababu tunacheza kibinafsi mnooo..
Hili suala lipo tokea tuanza msimu na sioni Ancelloti alibadilisha hii hali., kwasababu ni muoga wa mabadiliko, team ina shida ya kutengeneza nafasi kwa washambuliaji, viungo wanaocheza huo uwezo hawana., kwasababu Valverde hana hizo skills, Bellingham nae ni mfungaji mzuri ila hana mipango., Modric anaweza ila umri umemtupa mkono, ila ana option ya kumchezesha Arda Güler, huo uwezo anao ila sasa Mzee Ancelloti anaogopa kujaribu kitu kipya.,

Anaweza kuanza na Camavinga, ubavu mmoja akampa Modric/Valverde/Ceballos na Mwingine Bellingham., juu ya hao akampa Arda kazi moja tu ya kutengeneza mipango kisha kule mbele aamue kuanza na Vinicius na Mbappe ama Rodrygo, wawili hapo.
Kwenye beki hatuna option zaidi ya wale wawili, ama ampe nafasi Tchouamen acheze na Rudiger., kwasababu Militão bado akili haijakaa sawa.,
 

Timu haina creative players kama walivyokuwa Kroos na Modric. Hawa kina Tchou, Camavinga na Jude ni nguvu nyingi creativity hawana. Hiyo ni changamoto itatusumbua msimu wote. Defense tuombe Alaba arudi ASAP ana utulivu wa kutosha. Mbappe is not up to speed yet.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…