Real Madrid (‎Los Blancos) | Special Thread

Game imeisha tumeua...

Urejeo wa Camavinga unaleta tija pale kati kati.
Nilifanikiwa kuangalia kipindi cha kwanza tu jana., kidogo vijana wanaonyesha jitihada., ni kama wanajua walipokwama, so kila mtu anajitahidi ili kumpunguzia Kocha lawama., ila kuna ishu bado inaendelea., tukiwa tunashambulia tunakuwa sana wachache mbele, ama wanachelewa kwenda mbele wakati wa kushambulia, itabidi Mwalimu alifanyie kazi hili suala.
Camavinga kama akiendelea hivi tutakuwa tumepunguza tatizo kwenye eneo la kati., ninapenda anavyopokea mipira na kuitoa.,ile ndio kiungo anatakiwa kufanya, sio mtu ana pokea mpira hata hawezi kugeuka nao., kitendo cha kuweza kugeuka inasaidia sana team kufunguka.
 
Siku hizo hatuna game rahis yaan kila game kwetu ningumu asee!!
Mimi ninaona Ancelloti ndio anayezungua, huwa ni muoga sana kufanya mabadiliko., jana tulikuwa na viungo Wanne uwanjani ila jamaa walishika dimba, shida ni kuwa hao viungo wote watatu wana uchezaji unaofanana., Modric na Ceballos walivyoingia ndio game ilibadilika, niliona tunacheza mpira mzuri tu unaoeleweka.
Kama atakuja Kocha mwingine msimu ujao ni lazima afumue midfield yetu.
 

Ton kroos na Modric walikuwa wanarahisisha sana game kutokana na brain yao hawa watu naona itakuwa ngumu sana kupata replacement yao
 
Ton kroos na Modric walikuwa wanarahisisha sana game kutokana na brain yao hawa watu naona itakuwa ngumu sana kupata replacement yao
Ni kweli kabisa, ila wakati wao umepita hatuna budi kukubali hilo, kinachotakiwa sasa ni Mwalimu aumize kichwa ni namna gani atawapanga vijana waliopo tupate matokeo chanya.
Ila kwa namna vijana walivyokuwa wanacheza hana haswa kipindi cha kwanza, kiukweli bado sana, kwasababu hata kwenye safu ya usashambukiaji kila mtu anacheza kivyake., mbaya zaidi sasa tukienda kushambulia unakuta una wachezaji wawili ama watatu tu mbele, sasa sijui shida ipo wapi kiukweli., na maelekezo ya Mwalimu ama ni vijana tu wamekuwa wazito.
 

Alicheza
Mwanzo tulikua na viungo wanne wa sifa moja ila majukumu yao yalikua tofauti.

Kipindi cha kwanza Madrid walicheza mfumo wa 3-4-2-1.

Yaani Camavinga na Federico Valverde walisimma kati kati kama 6 na 8.

Miltao alibana kulia huku Vasquez akisogea Eneo la kiungo.

Rudiga alibana kushoto huku Garcia nae akipanda Eneo la kiungo.

Beki ya kati alisimama Aurelian Tchouameni.

Attacking midfielders walisimaa Vini na Jude.

Foward akasimama mbappe.

Lengo lilikua ni kuushika mchezo na kwa Plan hii ilikua nzuri sema haikulipa kwa sababu kuna maeneo waliwekwa watu sio sahihi.

Ndiomana Kipindi cha pili Carlo hakubadili tu wachezaji Bali na mfumo mzima wa uchezaji wa timu kwa ujumla.

Mimi sipendezwi na kuchelewa kwake kufanya mabadiliko tu wakati mapema tu timu inashikwa na Anaona kabisa mchezaji flan kapwaya ila anaacha tu.

Mfano Hii Mechi Federico Valverde alipaswa kupunzika kusubiri El classico kijana katumika sana
 

tatizo kuu la timu lipo kati, midfield zote ni za style moja amabazo sio rafiki kwa mazingira ya timu, Camavinga, Valverde na Belingham lazima wawili wakae nje modric na Rodrygo wachukue nafasi.
 
Valverde kuanzia game inaanza hakuwepo kabisa uwanjani, na Ancelloti ni kama amekariri kuwa Valverde ni lazima acheze., una Ceballos nje na Arda Güler unamforce vipi mtu kucheza wakati unaona kabisa amechoka., halafu ile game hata haikutaka mambo mengi, ila sasa kwa plan ya Kocha akajikuta anaufanya mchezo uwe mgumu.
Kama kwenye El classico ataenda na plan ile, tusitarajie makubwa., yaani team haikueleweka kama inashambulia ama inajilinda, kwasababu kote tulipwaya.
 
Mi nilishangaa alivyomtupa Bellingham pembeni nilichoka sana,afu kati viungo wagumu wote.kama vipi arda awe anaanza afu jude ajichange ila ndo hivo kocha ni kama ana uwoga flani ivi.
 
Mpangilio ni huh hapa.

Kabla ya mechi kuanza atoke nani aingie nani?
 

Attachments

  • FB_IMG_1729619230272.jpg
    103.5 KB · Views: 20
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…