Real Madrid (‎Los Blancos) | Special Thread


Ata uelewi mlengo wa timu. Bossy unakua kama mashabiki wa timu za bongo
 
Nasikia fununu kwamba MILTAO atakuwa nje ana majereha. Twafaaaa
Sio fununu man, ni Ukweli, tutamkosa msimu mzima pamoja na Courtois.,
Wakati huo huo Arda Guler amefanyiwa upasuaji leo na yeye atakaa nje kwa muda, japokuwa inategemewa kuwa atarudi mapema uwanjani., hao wote wanaungana na Dani Ceballos kwenye kujiuguza majeraha.
 

Official Announcement: Kepa​

14/08/2023

Real Madrid C. F. and Chelsea FC have reached an agreement to sign Kepa Arrizabalaga on loan, seeing him sign for the club for this season until 30 June 2024.
Kepa will be presented as a new Real Madrid player tomorrow, Tuesday 15 August, at 1.30pm at Real Madrid City.
 
Juzi niliangalia game ila sikutoa recommendation hapa. Ukweli tulishinda ila mpira wetu bado si tishio kabisa. Hatuna structure ya kushambulia, build up pia haipo.

Kidogo alivyongezeka modric ndio nikaona kiasi chake tunauwezo ata wa kuzunguka 18 ya mchezaji.

Timu bado sana
 
Binafsi, sikufanikiwa kuangalia game yetu, niliangalia highlight tu kidogo, hata hivyo sikuridhishwa na nilichokiona, kuna shida niliiona, na ni hii ya kutokuwa na kiongozi, kwa muda mrefu sana tumekuwa na tendency ya kumtengenezea mfungaji wetu nafasi za ufungaji, ila nilichokiona pre season hatuna huyo mtu kwa sasa., imekuwa ni vurugu tu mtu anapofika na mpira ndani ya eneo la hatari ya team pinzani.
Vinicius akifika anapiga, haangalii kama kuna mwenzie aliye sehemu nzuri zaidi ama laa, Bellingham na yeye anataka kuonyesha umwamba., Rodrygo pekee ninaona anajaribu hata kucheck wenzie.

Sasa ni muda sasa wa Ancelloti kuamua ni nani atakuwa mfungaji wetu, ili sasa team ifocus kumtengenezea nafasi kama tulivyofanya kwa akina Cristiano na wenzie huko nyuma., hapo ndipo tutaona uelekeo wa team, laa sivyo hizi vurugu pale mbele hazitaisha.
 

Kwa jude nakupinga, kiasi ndio mchezaji aliyeonesha uhai na umakini, alikua anafanya tackle,ana hold mpira ana beba mpira kwenda mbele. Ufanisi wake ulikua 80% ya game.

Kweli vini hana utulivu wenge ni jingi. Nafikiri bado ana ule woga na haraka ya kufikia alichokifanya msimu ulioisha.

Wala hatukuua na tendecy ya kumtengenezea mfungaji mmoja. Kila game ina approach yake unapokua na joseleu mbele huwezi cheza kama ukiwa na vin au rodrygo. Utaitaji zaidi upige mipira ya juu maana height na efficiency vinambeba.

Changamoto bado iko kwenye coaching staff. Kinaitajika kufanyika kitu kikubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…