Real Madrid (‎Los Blancos) | Special Thread

Atletico Madrid anafata nadhani, Ukweli jana ilipendeza kuona tumeweka vijana pale katikati ya dimba. Nasubiri ujio wa tchouameni uongezee nguvu
Vijana walijitahid kiukweli, sio mbaya sana, ningependa kuona wanajitahidi kukaa na mpira zaidi na kutengeneza nafasi kutokea kati kati, kwasababu kwasasa hatuna full back wa kufanya hiyo kazi.,

Kituo kinachofuata ni Kombe la Mfalme dhidi ya Atletico Madrid pale Bernabéu., halafu Jumapili tena hapo hapo tunawakaribisha Real Sociedad., yaani ni bampa to bampa
 
Ancelotti bado anawaamini Modrić na Kroos, ila kiukweli kwasasa wapo slow sana., yaani licha ya kuwa na Valverde kama ziada katika kiungo ila jamaa bado wanacheza vizuri kati kati ya uwanja., shida nyingine tuliyonayo ni kuwa na watu wachache wakati tunashambulia.!
Ceballos ameingia acha tuone kama atafanya mabadiliko yoyote pale kati kati.
 
Naangalia game timu yetu inatia huruma
Tunahitaji vijana wenye kasi kwenye kiungo., hii itatusaidia wakati wa kushambulia kuwa tutakuwa na wachezaji wengi eneo la Atletico., so option zinakuwa nyingi pia., ila hii ya kuwa wa watu wawili ama watatu wakati tunashambulia wakati huo wao wakiwa wengi itatuwia ngumu sana kupata goli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…