Real Madrid (‎Los Blancos) | Special Thread

Iv Marco asensio mbna haijulikani kama ataondoka au laah?


Marco Asensio akitaka kucheza World Cup anatakiwa akafanye sprint za hatari na apige bao hata 5 hivi za haraka haraka kwenye timu yoyote Italy au England. Aking'ang'ania kucheza Real Madrid bench linamuhusu na timu ya taifa ataiona kwenye TV tu. Club iliwafungulia mlango baadhi ya wachezaji akiwemo Asensio, na kuna timu nyingi zilionyesha interest akakataa kuondoka. So he already knows what's going to happen to him. Timu imeshindwa kusajili striker kwasababu kuna watu hawataki kuondoka.
 
jamaa angeenda Arsenal pale angekiwasha kinoma!
 

Casemiro is considering Manchester United's offer​

Hasn't ruled out a move to the Premier League giants

Wakuu mnasemaje kuhusu hii ishu ya Casemiro., club imtoe!?

Imtoe tu mana hana maajabu, Ila replacement ni jambo la lazima, wale vijana wakifaransa sio wakuwaamini kabisa.
 
Imtoe tu mana hana maajabu, Ila replacement ni jambo la lazima, wale vijana wakifaransa sio wakuwaamini kabisa.
Akiondoka sasa hivi, ina maana vijana wetu wa Kifaransa ndio mbadala wake, sioni tukiingia sokoni kutafuta mbadala wake
 
Bila ya replacement itaigharimu timu sana kwa maana ya sana.
Uwezekano wa kupata mbadala wa uhakika ni mgumu sana, hapo labda Ancelotti awe anaenda na double pivot ya Camavinga na Valverde. Ama Kroos., ila kuingia sokoni kwa muda uliobaki sioni hilo likitokea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…