Platnam
JF-Expert Member
- Mar 1, 2011
- 769
- 1,239
Hili ndio la msingi. Wachezaji wengi kwa sasa umri umesogea. Vijana wageni hawana experience ya kutosha na soko la wachezaji limekua na ushindani mkubwa kwa sasa. Kuunda timu kunaitaji utulivu.
Nimekusoma vyema Mkuu, ila tunapishana kwenye mambo kadhaa, Moja ni uundwaji wa team, kwa upande wangu sijaona kama Zidane ameshindwa kuunda team sababu asingeweza kuuza karibia kikosi kizima kisha akasajili wapya, uundwaji wa team ni kitu cha hatua, usishangae team ikawa inaundwa hata misimu matatu.,
Unaposema kuwa Zidane alikuta team.imeundwa tayar usisahau kabla yake alikuwepo Benitez akafukuzwa kwa kushindwa kuleta matokeo chanya, swali la kujiuliza ni Vp Zidane alifanikiwa na team ile ile na Benitez akashindwa!? Hapo utagundua kuifundisha Real Madrid inahitaji kitu cha ziada.
Kwa makocha uliowataja wapo vizur kwenye team zao japokuwa hawana cv kubwa, anayeweza kuhimili Real Madrid labda Pochettino kwanza apewe muda wa kutosha, ila tukisema kuwa aondoke Zidane kwasasa aletwe Kocha mwingine hakuna wa kutuvusha kwasasa! Ile team inahitaji Kocha anayewafahamu wachezaji , kwasababu si kwamba hatuna team nzuri bali ni kwamba hawana tena ile hari ya kushinda unaweza kuona hilo kwenye game dhidi ya Sevilla, kikosi kile kile kasoro Ramos walitoka kufungwa kule Paris lakin wakapata matokeo La liga, hakuna mbinu mpya iliyotumika bali ni wachezaji waliamua kucheza kama team, ina maana performance kama ile ikiwa inajirudia mara.kwa mara tuna uwezo wa kupata.kikombe msimu huu.

