Siempre Hechos
JF-Expert Member
- Dec 9, 2016
- 1,231
- 1,537
Ni kweli mkuu, ila tofauti ya Rais wa Madrid na Club nyingine ni Kwamba, Florentino Perez kuvunja kibubu hashindwi, akimtaka mchezaji yeyote atampata, akimshindwa ujue yeye kaamua tu kuachana naye!kwa sisi mashabiki wa manchester tunaamini ya kwamba sir alex ferguson ameleta mafanikio makubwa sana alipokuwa manchester united baada ya kujenga emperor zaidi ya goguryeo ndani ya miaka 26 ya utawala wake lakini moja kati ya uamuzi ambao haukunifurahisha ni kitendo chake cha kuwaruhusu real madrid watuzidi kete kwenye dili la usajili wa luka modric.
bado nashindwa kuelewa kama aliweza kupambana na daniel levy kwenye dili la usajili wa dimitar berbatov kwa nini hakutumia nguvu kubwa sana kwa ajili ya luka modric?
ukimuondoa andres iniesta na xavi hernandez sijawahi kumuona kiungo mwengine yeyote akimzidi kimpira mchawi huyu wa croatia asiyepewa heshima yake inayostahili.
kumuangalia luca modric akicheza mpira ni burudani zaidi kwa mwanamme kuliko kuangalia video za beyonce akionyesha maungo yake ya mwili.
kwa sisi mashabiki wa manchester tunaamini ya kwamba sir alex ferguson ameleta mafanikio makubwa sana alipokuwa manchester united baada ya kujenga emperor zaidi ya goguryeo ndani ya miaka 26 ya utawala wake lakini moja kati ya uamuzi ambao haukunifurahisha ni kitendo chake cha kuwaruhusu real madrid watuzidi kete kwenye dili la usajili wa luka modric.
bado nashindwa kuelewa kama aliweza kupambana na daniel levy kwenye dili la usajili wa dimitar berbatov kwa nini hakutumia nguvu kubwa sana kwa ajili ya luka modric?
ukimuondoa andres iniesta na xavi hernandez sijawahi kumuona kiungo mwengine yeyote akimzidi kimpira mchawi huyu wa croatia asiyepewa heshima yake inayostahili.
kumuangalia luca modric akicheza mpira ni burudani zaidi kwa mwanamme kuliko kuangalia video za beyonce akionyesha maungo yake ya mwili.
Hivi hilo kombe original linachukuliwa mojakwamoja?
Kama kawaida, asanteee!Cristiano Ronaldo has admitted he may have spoken out of turn in suggesting that his Real Madrid days were numbered after the Champions League final.
Having starred for Madrid throughout the competition, this year's top scorer drew a blank against Liverpool in Kiev.
Substitute Gareth Bale stepped up to seal a third straight title as the Blancos prevailed 3-1, with Karim Benzema also getting his name on the scoresheet.
Ronaldo, however, stole the headlines when he referred to his sparkling Madrid career in the past tense to reporters.
That statement caused an instant reaction, with both Madrid president Florentino Perez and coach Zinedine Zidane speaking out to deny his exit.
And while he later claimed he was taken out of context, the Portugal striker seemed to regret the storm his comments had caused.
"It takes away from a beautiful, historic moment for us that is winning three Champions Leagues in a row, obviously it is a special moment," he told Fox Sports.
It's always great to win the Champions League because I know how important that competition is, I have had a great Champions League from start to finish so I'm very happy.
"A player's personal things aren't the most important thing now, it might have been taken out of context but maybe I shouldn't have said what I said."
Ronaldo finished the 2017-18 Champions League with 15 goals in 13 starts, and now boasts no less than five winner's medals in the competition with Manchester United and Madrid.
Swahili version sass! asante!Mshambuliaji wa Real Madrid Gareth Bale alifunga bao la pili kupitia "mbilimbili" kwa guu lake la kushoto na bao lake la pili kupitia mkwaju alioupiga pia kwa guu lake la kushoto na kuipa timu yake ushindi wa mabao 3-1 katika fainali ya kombe la mabingwa Ulaya, Champions League. Huu ni ushindi wa tatu mfululizo wa Real Madrid.
Bale, ambaye ametokea katika mbao ndefu, na ambaye pia alifunga bao wakati wa fainali ya mwaka 2014 kati ya Real na Atletico Madrid, alikuwa amekaa uwanjani kwa dakika tatu hivi wakati aliporuka juu mbilimbili na kuupiga mpira kufuatia pasi maridadi majimaji kutoka kwa Marcelo, nje kidogo na eneo la hatari la lango la Liverpool. Mpira ukautikisa wavu wa Liverpool na kuiwezesha Real kuongoza kwa mabao 2-1 dakika ya 64 katika uwanja wa Olympic Stadium mjini Kiev nchini Ukraine.
Kipindi cha pili kilianza kwa kisa cha kushangaza ambapo Karim Benzema aliipatia timu yake ya Real bao la kwanza baada ya kosa kubwa lililofanywa na mlinda lango wa Liverpool, Loris Karius. Sadio Mane alisawazisha dakika chache baadaye, lakini Bale akaiweka tena Real kifua mbele.
Cristiano Ronaldo sasa ameshinda mataji matano ya ligi ya mabingwa wa Ulaya katika maisha yake ya kusakata soka, lakini hata yeye hawezi kuhoji kwamba usiku wa leo ulikuwa wake Gareth Bale. Mchezaji huyo kutoka Wales alitarajiwa kucheza katika kikosi cha kwanza cha Real lakini akaachwa nje na nafasi yake ikachukuliwa na Isco.
Jeraha la Salah pigo kwa Liverpool
Jurgen Klopp na Liverpool walipata pigo wakati Mohamed Salah alipoumia katika kipindi cha kwanza, na kulazimika kutoka nje ya uwanja baada ya dakika 30 alipojiumiza katika bega lake.
Huu haukuwa usiku wa Salah, huku Real wakimuwezesha Zinedine Zidane kuwa kocha wa kwanza kuwahi kushinda kombe la mabingwa wa Ulaya miaka mitatu mfululizo. Madrid ni timu ya kwanza kufaulu kufanya hivyo tangu Bayern Munich mnamo mwaka 1976. Hili ni taji lao la nne katika kipindi cha miaka mitano, na ni la 13.
Kwa upande wa Liverpool, mechi hii itakumbukwa kwa janga lililomkuta mlinda lango Loris Karius katika kipindi cha pili, na kwa machozi ya Salah wakati alipokuwa akitoka uwanjani Olympic Stadium. Raia huyo wa Misri ambaye ameifungia Liverpool mabao 44 msimu huu, alijiumiza bega lake alipokuwa akianguka chini baada ya kukabiliana na Sergio Ramos dakika ya 25. Dakika tano baadaye akampisha Adam Lallana.
Uwezekano wa Salah kushiriki mashindano ya kuwania kombe la dunia nchini Urusi umeingia mashakani, pamoja na Dani Carvajal, beki wa kulia wa Real aliyetoka nje ya uwanja baada ya kupata jeraha katika misuli kabla kipindi cha mapumziko. Majeaha hayo yaliifanya kasi ya mchezo kupwaya na kupoteza utamu uliokuwepo tangia mwanzo, huku Liverpool ikidhibiti mchezo.
Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amedokeza kwamba jerah ala Mohamed Salah ni baya. "Ni jeraha baya. Yuko hospitalini akifanyiwa vipimo na kupigwa picha ya X-ray. Huenda ameumia mfupa unaoiunganisha shingo na bega au bega lenyewe," alisema Klopp baada ya kupoteza mechi ya fainali na Real Madrid.
Real walitiwa tumbo joto na kutolewa kijasho, lakini baada ya Salah kutoka, wakahisi wana fursa ya kushinda. Walifaulu kushinda bao dakika ya 43, lakini halikukubaliwa baada ya kuonekana walikuwa wameotea.
Beki wa Real Madrid, Sergio Ramos amejutia kitendo cha kumsababishia majeraha ya bega nyota wa Liverpool, Mo Salah na kumtumia ujumbe akimuomba radhi kuwa hakudhamiria kufanya hivyo.
Salah alilazimika kutoka uwanjani kipIndi cha kwanza kwenye mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati Liverpool ikitifuana na Real Madrid.
Mchezo huo ambao ulibadilika baada ya Salah kutoka nje, uliisha kwa Real Madrid kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 na kunyakua taji la ubingwa kwa mara ya tatu mfululizo na ikiwa ni mara ya 13 katika historia ya mashindano hayo.
Machozi ya Salah yaliwafanya mashabiki waliokuwa uwanjani hapo kushika tama, huku wengine wakishika vichwa kwa hofu majaraha aliyopata huenda yakamsababisha kushindwa kuichezea timu ake ya Misri katika mashidano ya Kombe la Dunia.
Mashabiki wa Liverpool wamemtupia lawama Ramos kwenye mitandao ya kijamii kutokana na kumsababishia majeraha makubwa Salah katika bega.
kwa sisi mashabiki wa manchester tunaamini ya kwamba sir alex ferguson ameleta mafanikio makubwa sana alipokuwa manchester united baada ya kujenga emperor zaidi ya goguryeo ndani ya miaka 26 ya utawala wake lakini moja kati ya uamuzi ambao haukunifurahisha ni kitendo chake cha kuwaruhusu real madrid watuzidi kete kwenye dili la usajili wa luka modric.
bado nashindwa kuelewa kama aliweza kupambana na daniel levy kwenye dili la usajili wa dimitar berbatov kwa nini hakutumia nguvu kubwa sana kwa ajili ya luka modric?
ukimuondoa andres iniesta na xavi hernandez sijawahi kumuona kiungo mwengine yeyote akimzidi kimpira mchawi huyu wa croatia asiyepewa heshima yake inayostahili.
kumuangalia luca modric akicheza mpira ni burudani zaidi kwa mwanamme kuliko kuangalia video za beyonce akionyesha maungo yake ya mwili.
What Ramos has said.JINA la Sergio Ramos si geni masikioni mwa mashabiki wa soka, hasa wa La Liga. Mbali na sifa nyingine ikiwamo uwezo wake wa kutupia mabao, nahodha huyo wa Real Madrid anawavutia wengi kutokana na aina yake ya uchezaji wa kujitoa anapokuwa uwanjani.
Ramos aliweka rekodi ya kuwa mchezaji mwenye kadi nyekundu nyingi La Liga akiwazidi wakongwe, Pablo Alfaro na Xavi Aguado, waliokuwa wamekutana na adhabu hiyo mara 18 kila mmoja.
Je, ukiachana na hilo, uliyajua haya kuhusu nyota huyo ambaye pia ni nahodha wa timu ya Taifa ya Hispania?
Ramos mwenye umri wa miaka 31, ni mume wa mwandishi wa habari maarufu wa Hispania, Pilar Rubio, ambaye amezaa naye watoto wawili; Sergio na Marco. Wawili hao walianza kuripotiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi mwaka 2012.
Akiwa na umri wa miaka 19, Ramos aliitwa kwa mara ya kwanza kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Hispania. Hivyo, alivunja rekodi iliyodumu kwa miaka 55 ya kuwa mchezaji mwenye umri mdogo kutinga ‘uzi’ wa kikosi hicho.
Wakala wake ni Rene Ramos, ambaye ni kaka yake. Jamaa huyo ndiye aliyesimamia dili la Ramos kutua Madrid akitokea Sevilla mwaka 2005, akiwa ndiye chipukizi wa kwanza wa Hispania kununuliwa kwa ada kubwa (euro milioni 27).
Kutokana na ustadi wake wa kuwazuia washambuliaji, moja kati ya rekodi zake kali katika soka la Hispania ni kushinda tuzo ya Beki Bora wa La Liga kwa misimu minne mfululizo, yaani kuanzia mwaka 2012 hadi 2015.
Baba yake mzazi, Jose Maria, ni shabiki mkubwa wa Manchester United. Ramos alifichua siri hiyo mwaka 2013, siku chache kabla ya Mashetani Wekundu hao kuvaana na Madrid katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kabla ya kukutana na bibiye Pilar, Ramos alikuwa mmoja kati ya mastaa waliokuwa wakisifika kwa kujiachia na warembo. Aliwahi kutajwa kutoka na walimbwende, Lara Alvarez, Amaia Salamanca, Elisabeth Reyes, Nereida Gallardo na Carolina Martinez.
Rafiki mkubwa wa Ramos ni kiungo wa Arsenal, Mesut Ozil, ambaye alicheza naye kwa misimu kadhaa Santiago Bernabeu. Ramos ni miongoni mwa wachezaji wa Madrid ambao hawakutaka Mjerumani huyo aondoke Hispania na kuhamia Arsenal.
Mama mzazi wa Romas, Paqui, ni shabiki mkubwa wa Real Madrid na inasemekana huchangia kwa kiasi kikubwa uamuzi wa mwanawe huyo kukataa mara kwa mara ofa za kujiunga na klabuni nyingine ambazo zimekuwa zikimtaka.
Ramos husherehekea ‘birthday’ yake Machi 30 kila mwaka. Kwa wafuatiliaji wa tasnia ya burudani, watagundua kuwa ni sawa na mwanamama anayefanya vizuri kwenye soko la muziki nchini Marekani, Celine Dion.
Kwa upande wa mkwanja, beki huyo wa kati, ambaye pia anacheza vizuri eneo la mlinzi wa pembeni, anatajwa kumiliki utajiri wa Dola za Marekani milioni 60, zaidi ya Sh bil. 130 za Tanzania.