RE: Ufisadi Hela za Benki ya Dunia Wizara ya Maji

anney

Senior Member
Jul 9, 2010
155
45
Tanzania ni moja nchi iliyochukua mkopo (US$ 951.00 million) ili kuboresha huduma ya maji kwa wananchi wake. Mradi huu unaogharimiwa na benki ya dunia umeshaanza kutekelezwa katika wilaya mbalimbali hapa nchini. Taarifa zilizopo ni kwamba hela hizi zimeshindwa kuonyesha matokeo yaliyotarajiwa kutokana na utekelezaji wake kuingiliwa na ufisadi. Mazingira ya ufisadi ni kama ifuatavyo.
1. Watu waliopewa tenda ya kuchimba visima virefu vya maji katika baadhi ya wilaya mfano Handeni, Babati, kibaha nk, hawakuchimba kulingana na ushauri wa kitaalamu, kwa kuchimba urefu wa mita zinazotakiwa, hivyo maji hayajaoneka! mfano sehemu ambayo wanatakiwa/walitakiwa kuchimba mita 120 wao wamechimba mita 60 au pungufu.
2. Kuna baadhi ya sehemu mtu aliyepewa tenda anajenga tanki la maji kabla maji hayajapatika, hivyo baada ya kuchimba kisima na hakuna maji tenki linakuwa hakuna kazi.
3. Baadhi ya waliokuwa wafanyakazi wa wizara ya maji walijianzishia makampuni ya kuchimba maji ambayo hayana uwezo wa kutosha. Lenge lao ni kuzengea hiyo hela. Inasemekana wengine waliacha kabisa kazi.
4. Baadhi ya tenda walipewa wanasiasa au makada (CCM) wa vyama vya siasa. Baadaye wao/yeye akaanza kutafuta mtu wa kufanya kazi kwa niaba yake.
5. Baadhi ya maeneo machache ambapo maji yamepatikana kwa bahati njema, miradi imeshindwa kukamilika kama Dare es salaam maana fedha za kumalizia hakuna.

Jana nimeona wizara ya Maji imewasilisha bajeti yake nilitegemea huu ufisadi ungeibuliwa. Tunawashauri PCCB wafanye uchunguzi wa hili jambo.
Ukitaka kufahamu zaidi kuhusu hii project soma hii link.
Projects : Water Sector Support Project*|*The World Bank
 
Naomba nikupe pole: swali, wewe umeshawahi kuona PCCB imemkamata kiongozi yeyote? Jibu ni hapana, kwa sababu wao PCCB kabla ya kukukamata wewe kiongozi wanakupigia simu kuona kama kuna mgao wao na kama hakuna ndipo wanaanza kelele. Kwa kifupi, hapa Kikwete kawatafutia ulaji washikaji wake as they are not fair in kukamata watu.
 
Naomba nikupe pole: swali, wewe umeshawahi kuona PCCB imemkamata kiongozi yeyote? Jibu ni hapana, kwa sababu wao PCCB kabla ya kukukamata wewe kiongozi wanakupigia simu kuona kama kuna mgao wao na kama hakuna ndipo wanaanza kelele. Kwa kifupi, hapa Kikwete kawatafutia ulaji washikaji wake as they are not fair in kukamata watu.
PCCB wameshamkamata mbunge wa Bahi kama umesahau. ila kesi ikiika mahakamani ndiyo basi haiishi maana kesi mbunge wa bahi hatuisikii tena!
 
Well said, kwa nini watu wengi wangependa kuacha kazi zao za sasa na kujiunga na pccb? Tafakari, chukua hatua!
 
PCCB kumbe kuna ulaji wa kutosha, inabidi vijana waanze ku-opt kujiunga na PCCB warekebishe maisha. Inaelekea mbunge wa bahi alikuwa mgumu kwenye kutoa mgao.
 
PCCB wameshamkamata mbunge wa Bahi kama umesahau. ila kesi ikiika mahakamani ndiyo basi haiishi maana kesi mbunge wa bahi hatuisikii tena!

Kakamatwa ila kesi itakaa muda mrefu sana bila kutolewa hukumu na pindi hapo baadae kutolewa hukumu utaambiwa hana kosa na ndivyo mahakama zetu zilivyo kwa viongozi wetu wanashindwa tu kuidhinisha kuwa viongozi wapo juu ya sheria
 
Hii ndo Tz iliyotawaliwa na rushwa mpaka sasa imefika hatua ya kufanya matangazo ya rushwa, mfano halisi ni Tangazo la magodoro ya comfy ambayo mnuzi anapewa godoro fake anawatisha wauzaji ataenda police wauzaji wanamwambia watampa godoro bure ili asiende police, sasa kama tumefikia kutangaza rushwa basi tena!
 
Mradi huu hauwezi kufanikiwa (angalia proposal yake ndio utajua hili) na pale utakapofanikiwa kwa japo 50% hautaweza kudumu. Mradi huu ulichoweza kufanya ni kununua land cruiser za kutosha zimemwaga katika wilaya zote za mradi. Hivi inaingia akilini kweli kuwa kwa kununua magari haya tunaongeza upatikanaji wa maji vijijini????
Kingine ni aina ya wakandarasi waliopewa kazi. Sina tatizo na watumishi wa mamlaka za maji kujianzishia kampuni na kupewa/ kujipatia tenda; shida yangu ni uwezo wao. Uwezo wa kampuni hizi kwa maana ya vifaa hasa na pia ujuzi.

Visima vilivyoweza kuchimbwa (hata kama vimetoa maji kwa wiki moja) ni vile tu ambavyo h/shauri husika ilitaka ifunguliwe na VP au mwenge wa uhuru. Zaidi ya hapo hakuna lolote linalofanyika.
Bahati mbaya wananchi wa Tz tumekalia kupiga kelele juu ya ufisadi wa sehemu moja tu na uliwahusu wakubwa wachache kama ule wa BoT na Richmond/ Dowans. Tunajifanya hatuwaoni mafisadi hawa waliojazana katika ofisi za halmashauri na mashirika ya umma huku ngazi ya chini na kati.
Nani hajui kinachofanyika leo katika idara/ mamlaka za maji?
Nani hajui kuwa wahujumu wakuu wa miundo mbinu ya umeme ni watumishi wa TANESCO?
Nani hajui udhaifu wa tendaji wa TANESCO, unaomba kuunganishiwa umeme leo utakamilika baada ya mwaka 1 au miaka 2? Na hapo umelipa malipo yote halali na kuhonga juu?
Hivi hatujui kuwa kila mara h/shauri/ manispaa/ jiji wanapotangaza mradi wa upimaji viwanja basi kila afisa ardhi hujipatia viwanja vingi na kuviuza kwa bei mbaya? Huu ndio mradi wa vijana wa Mama Tibaijuka
Hivi hatujui wakuu wa mikoa/ wilaya na wakurugenzi wa h/mashauri hunyamazishwa kwa kupewa viwanja kwa haraka? Nao wakishapata hawataki kujua wananchi wengine wataishi wapi?
Hivi hatujui kuwa kampuni zote za kukusanya ushuru ktk vituo vya mabasi/ na parking ni za watendaji wa h/shauri?
Hatujui kampuni zote zinazoshinda tenda za ujenzi aidha ni za madiwani (mara nyingi meya/mwenyekiti au naibu wake au wajumbe wa kamati ya fedha?) au watendaji wa h/shauri?
Nenda kaangalie mzabuni wa dawa za mifugo na pembejeo za kilimo ni nani. Kama sio DALDO basi afisa yoyote ktk idara hii.

Ndugu zangu kuthibitisha haya ushahidi ni huu:
1. Mchakato mzima wa manunuzi ktk h/shauri umegubikwa na wingu zito jeusi. Hata km watatangaza tenda huwa ni kutimiza wajibu lakini mzabuni huwa amekwishajulikana.
2. Mzabuni/ mkandarasi anapewa kazi kila mwaka ktk h/shauri hakamilishi au hufanya chini ya kiwango lakini hakosi tenda kwa kazi inayofuata. Kwa nini? Kampuni inamilikiwa na mkuu wa idara/ mkurugenzi wa h/shauri au mwenyekiti au meya; nani anaubavu wa kumwadibisha?
3. Bei zinazoandikwa siku zote na wazabuni ktk h/shauri huwa za juu mno. Zimeongewa kwa hila kupita kawaida. Vial moja ya kuku kwa ajili NCD inauzwa kati ya sh.3500-4000/ lakini utakuta huko imeandikwa sh.6000-8000/= . Na mzabuni anayeshinda huwa ametaja bei hizi hizi. Yaani kama zabuni ni ya aina kumi za bidhaa basi mzabuni huweka bei zote sawaswa na zilizopo ktk bajeti ya h/shauri. Unaweza kujiuliza je, huyu mzabuni alikuwepo wakati wa kupanga bajeti? Aidha

4. Matumizi na bajeti ya h/shauri huwa sawa kwa 100%; yaani kama walitenga sh. 12,500,679.80 kwa ajili ya ukarabati wa chumba kimoja cha ofisi basi taarifa ya utekelezaji itaonesha walitumia sh.12,500,679.80. Swali la kuhoji hapa ni je, tangu bajeti ilipoandaliwa na kupitishwa mwanzoni mwa mwaka wa fedha (tufanye June,2012) hadi shughuli inakuja kufanyika (fanya March 2013) hakukuwa na mabadiliko ya bei hata kwa kifaa kimoja? Je, hiki tunachokiiita mfumuko wa bei haugusi h/shauri?
Wataalam mnaniambia kuwa wakati wa kuandaa bajeti walizingatia mfumuko wa bei (inflation) na kupanda na kushuka kwa thamani ya sarafu yetu! Kama kuna kitu huwa hakitazamwi wakati wa kuandaa bajeti za h/shauri ni suala la inflation. Tafuta bajeti ya h/shauri yoyote angalia bidhaa moja tu utaona imewekewa bei ya aina moja kwa miaka 3 mfululizo. Yaani kama ream ya karatasi 2009/2010 walisema watanunua kwa 8000/ basi hadi 2011/012 bei ni hiyohiyo. Kama chumba cha darasa (jengo tu) walisema wanatejengwa kwa sh.30,000,000/ mwaka 2008/2009 hadi leo 2012/013 gharama ni ile ile!
Kituko kikubwa ni taarifa zinavyoandikwa
Shughuli: Ujenzi wa choo cha shule
Gharama/ bajeti iliyopitishwa: 70,000,000.00
Kiasi kilichopokelewa: 70,000,000.00
Matumizi halisi: 70,000,000.
Ufanisi kwa kazi: 100% lakini ukitembelea utakuta choo hakijakamilika na kitatengewa mil 70 kwa hata miaka 3 mfululizo!
AU wanaweza kupokea fedha pungufu kwa 30% lakini watakwambia kazi imekamilika kwa 100%

HUU NDIO UFISADI ULIKITITA KTK HALMASHAURI ZETU. HAPA NDIPO TUNAPOTAKIWA JM KUANZA KUPIGIAKELELE!


EJL
 
Utaratibu wetu ni ule ule: Mwalimu usinibaini, wajinga ndio waliwao; nikipata mbili moja yangu, moja yako.Kiitikio mnakijua bila shaka.
 
Hii ndo Tz iliyotawaliwa na rushwa mpaka sasa imefika hatua ya kufanya matangazo ya rushwa, mfano halisi ni Tangazo la magodoro ya comfy ambayo mnuzi anapewa godoro fake anawatisha wauzaji ataenda police wauzaji wanamwambia watampa godoro bure ili asiende police, sasa kama tumefikia kutangaza rushwa basi tena!

Well said mate, nilikuwa sina pa kusemea kuhusu lile tangazo, halifai ktk jamii kwakweli.
 
Yaani watz hawana huruma kabisa na nchi yao. Wako tayari wananchi wafe kwa kukosa huduma mradi bank account zao zimejaa, inauma na inasikitisha
 
Mara nyingi sipendi kuongea ya kusikia. Ni kweli huyu mbunge wa Bahi amekamatwa lakini kuna habari kuwa mmoja wa watu wa PCCB ana bifu naye hivyo walimtegea. Narudia hizi ni habari za kusikia tu si zangu. PCCB haina jipya ni upuuzi tu.
 
Back
Top Bottom