Song of Solomon
JF-Expert Member
- Aug 5, 2021
- 2,733
- 5,490
Ukiingia katika tovuti ya Benki ya Dunia utaona Serikali ya Tanzania tarehe 22 September 2022 iliwasilisha na kuomba pesa ya mradi wa Mto msimbazi.
Mradi huo Benki ya Dunia (World Bank) uliusajiliwa kwa utambulisho wa namba P169425. Unaweza kutembelea na kuona. Mtasha hataki mambo ya gizani.
Serikali ya Tanzania kupitia wizara ya OR-TAMISEMI iliomba Jumla ya Kiasi cha Tsh billioni 650 kwa ajili ya mradi wa Mto msimbazi wenye madhumuni
1. Kuzuia mafuriko ya Mto Jangwani.
2. Kufanya bonde la Msimbazi kuwa na uoto wa kijani
3. Kutengeneza maeneo ya kupumzika Mto msimbazi na Jangwani
4. Kujenga Daraja la Jangwani kutoka Magomeni kwenda kariakoo
5. Kujenga kingo na sakafu ya Mto msimbazi
6. Kujaza maji na kufanya usafirishaji katika mto msimbazi.
24 November 2022 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa barabara (TANROADS) Mhandisi Rogatus H. Mativila akatangazia Dunia kuwa Serikali ya Tanzania imesainia Makubaliano na Benki ya Dunia.
Makubaliano kuhusu mradi huo na kwamba hatua za awali za kumtafuta Mkandarasi mshauri zimeanza na michoro imeshaanza kamilika na akaonyesha waandishi wa Habari michoro ya Jangwani na Mto msimbazi.
Bwana weeeee! Mvua ya mwaka huu kuanza na mafuriko kutokea tena Serikali ya CCM na watoto wa UVCCM wametugeuka kabisa kama vile siyo wale wa mwaka Jana. Leo wanasema
1. Mradi wote ni shilingi Billioni 300
2. Hawazungumzii tena shughuli zingine za mradi kama uboreshaji wa mazingira, uoto wa kijani
3. Hawazungumzii ujenzi wa kingo za Mto msimbazi
4. MWISHO anasema mama ndiyo katoa pesa (ameidhinisha) wala siyo benki ya Dunia tena.
Wakati ukiingia katika tovuti ya Benki ya Dunia inasema pesa zimeidhinishwa na Benki hiyo tangu mwaka 2022 November na mradi ulitegemewa kuishia 2028
Je, shilingi bilioni 350 za Benki ya Dunia mmezipeleka wapi? Zimepeperuka kwenda wapi? Nani amezitafuna?
Nimesikiliza mawaziri wawili, Innocent Bashungwa na Mohammed Mchengerwa wote wanazungumzia shilingi billioni 300, Vijana wa CCM na wao wamebeba gharama za mradi ni shilingi billioni 300 na zinatolewa na mama..