Re: Udahili wa wana funzi wenye stashahada ni tatizo ndani ya mfumo wa tcu

chusemale

Member
Jun 9, 2012
11
2
HI! WANA JF.
Kuna jambo ningependa kufahamu juu ya ukosefu wa majina kwa baadhi ya wanafunzi wa stashahada ktk taasisi ya serikali(TCU).Mfano mdogo ni ukosefu wa majina yote ya wanaCBE-MWANZA kujikuta hawapati usajili eti kwa kuwa RECORD zao hazipo.Sasa NaNi alaumiwe kwa ubabaishaji huu? Vilevile vijana hao wafanyeje ili waweze kupata fursa ya kujiunga na elimu ya JUU? Wana JF naomba mnijibu.

pole sana mkuu, mi nadhani hili ni tatzo ambalo serikali inatakiwa kuliangalia kwa mapana yake, kwa sababu tatizo hilo la kukosekana kwa taarifa za wanafunzi wanaotakiwa kuwajibika ni chuo husika ina maana kimeshindwa kuweka kumbukumbu vizuri za wanafunzi wake.

Lakini mie nakwenda mbali kidogo kuwa hata mfumo mzima wa udahili wa mwaka huu kupitia TCU kwa wanafunzi wenye stashahada waliomaliza mwaka huu umewatenga watu hawa. Nasema umewatenga kwa sababu vyuo vingi wanafunzi wanaosoma stashahada wanamaliza mwezi huu au mwezi ujao, na mpaka matokeo yatoke inaweza kufika mwezi wa nane

sasa TCU wametoa maelekezo kuwa mwisho wa kuomba ni Juni 30 mwaka huu, sasa hawa watu ambao walitaka kuunganishia kujiunga na shahada kwa mwaka huu ina maana hawana nafasi hiyo na wanatakiwa kubaki mtaani mpaka mwakani. Hapa serikali haijatenda haki, ni bora ingeacha utaratibu wa mwaka jana wa kuomba moja kwa moja chuoni badala ya kuomba TCU ili wenye nia ya kuunganisha shahada kwa mwaka huu wapate hiyo fursa au iwaruhusu waliomaliza stashahada mwaka huu waombe mara matokeo yao yanapotoka.
 
mkuu tcu itafunguliwa mwezi wa nane tena kwa taarifa 2liyopewa chuoni..
 
Back
Top Bottom