kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,301
- 12,600
TCU ni taasisi inayodhibiti ubora wa elimu ya juu. Inakagua, inashauri, inaruhusu Na kusimamisha au kufuta vyuo visivyokidhi vigezo vya ubora. Hivyo, vyuo vyote ambavyo vinatoa mafunzo vimefikia vigezo (minimum) vya ubora wa kumudu kutoa mafuzo yaliyokusudiwa. Ingawa ni kweli vyuo vinatofautiana kwa ubora.
TCU ndiyo yenye takwimu za vyuo vikuu vyote kuhusu kozi, ubora na idadi ya wanafunzi wanaoweza kudahiriwa kwenye kila chuo pamoja na ada inayotozwa kwa kila chuo.
Kabla ya kufutwa na Rais JPM wanafuzi walikuwa wanatuma maombi ya kujiunga vyuo vikuu kwa kutumia CAS kuchagua kozi na vyuo na mfumo huo wa udahiri ulikuwa na uwezo wa kumpangia mwanafuzi kozi aliyoomba kwenye chuo alichoomba kulingana na ufaulu wake na idadi ya walioomba kozi hiyo kwenye chuo hicho. Na kama nafasi kwenye chuo hicho imejaa mfumo ulikuwa ukimpeleka kwenye chuo kingine chenye nafasi bila usumbufu na gharama ya ziada kwa mwanafunzi.
Sasa hivi wanafunzi lazima waombe wenyewe kwenye vyuo husika kwa gharama zao, hivyo mwanafuzi atalazimika kuomba vyuo zaidi ya kimoja kwa gharama za uombaji za kila chuo na chuo ndicho kinanachochagua wanafunzi wa kusoma kwenye chuo chao na kutuma majina TCU kwa uhakiki.
Kufanya hivi kuna hasara zifuatazo:
1. Mwanafunzi anatumia hela nyingi kwenye maombi ya nafasi vyuoni.
2. Wanafuzi wanarundikana kwenye chuo kimoja wakati kuna nafasi kwenye vyuo vingine.
3. Unatoa nafasi ya wazazi kutoa rushwa kubwa vyuoni ili watoto wao wachaguliwe kozi fulani kwenye chuo fulani.
4. Baadhi ya vyuo vimepata nafasi ya kuwabagua wanafunzi wanaotoka kaya maskini wenye hela za kudunduliza kulipia karo kubwa za vyuo vyao.
5. Utaratibu unatoa mwanya kwa watendaji wa vyuo kuchagua ndugu zao, kabila na rafiki zao kupata nafasi ya kusoma chuoni kwao na kuwaacha watoto wengine wenye ufaulu mkubwa kuliko walioingizwa chuoni.
6. Mfumo unatoa mwanya wa UDINI kwenye selection. Anaechagua nani achaguliwe anaweza kusukumwa na vionjo vya udini na dhehebu lake kupatia nafasi kwanza watoto wa dini na dhehebu lake hata kama walioachwa wana ufaulu mkubwa kuliko waliopendelewa.
7. Vyuo vinadahiri kupita uwezo wao waliokadiriwa.
Faida zilizokusudiwa za utaratibu huu wa sasa ni moja tu, kuwa mwanafunzi atachagua chuo anachokitaka yeye. Lakini uzoefu unaonyesha kuwa hata kwenye utaratibu huu sio kweli kuwa wanafunzi wote wanachaguliwa kwenye vyuo walivyovitaka, bado wanaendelea kudahiriwa kwenye vyuo vyenye nafasi kama zamani baada ya kukosa nafasi kwenye vyuo wanavyovipenda.
Wanafunzi na wazazi wanadanganywa na majina ya vyuo kumbe elimu ni ileile hata kwa vyuo vingine.
Kudhibitisha ukweli huu TCU ipitie ufaulu wa wanafunzi wote walioomba kwenye vyuo ilinganishe na ufaulu wa wanafunzi wote waliodahiriwa kwenye vyuo wataogundua dhambi hii ya ubaguzi.