bombu
JF-Expert Member
- Jun 8, 2011
- 1,127
- 542
Wapendwa Sina jinsi ya kuielezea furaha yangu. Nimekuwa member wa JF kwa takriban mwaka sasa. Mie huwa si msomaji wa magazeti, na taarifa nyingi muhmu huzipata kupitia hapa JF. Kwa mara ya kwanza hii forum imenisaidia na nimeyaona matunda yake.
Nimefanikiwa kupata kazi, amabayo kwa mara ya kwanza niliiona hapa JF, katika forum ya "Nafasi za Kazi na Tenda". Mwanzoni sikuamini kama nami naweza pata kazi serikalini bila kuwa na mtu wa kunishika mkono, lakini leo imewezekana. Ni kweli kuna uwazi na ukweli na usawa kupitia Sekretariatiya Ajira na Utumishi. Tuliitwa watu saba na nafasi ilikuwa moja tuu.
Nimepata,
Namshukuru Mungu na WanaJF, Tuendelee kulijenga Taifa letu. Big up JF, LIVE LONGER.
Kwa wengine, Msikate tamaa, endeleeni kuomba kazi bila kuchoka, ipo siku mtafanikiwa, na tusipuuze kazi, na tufanye kazi kwa bidii na kutumia nafasi zetu kwa manufaa ya umma.
Asanteni.