RE: Mrejesho wa maoni yenu kuhusu mwanamke niliyempenda, 12/12 / 2020

Chairman Lee

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
1,352
1,485
Wasalaaam, habarini za mchana wakuu?

Bila kupoteza muda nimeona niwashirikishe hili kwani kipindi cha mwanzo mliweza kunishauri vizuri sana, ukweli nilipenda sana ushauri wa kila mmoja wenu katika tatizo langu.

Huyu binti nilimpenda sana kama mlivyojua na nili tanabaisha hapa jamvini kuwa ananikosesha amani sana.

12/12/2020 naona ndio siku ambayo mapenzi yetu yamekwisha kwani aliweza kutamka ya moyoni japo mimi nilikuwa nafahamu nini atakacho sema, nilijaribu kumpa muda na kuvuta subira ili nione atasema nini kweli ametamka yaliyo sahihi kwake kamasintakuwa nimekosea.

Nitashare nanyi baadhi ya text zake na zangu kwa hatua zenu kama washauri wa hili swala , kwani mwanzo mliweza kunishauri vizuri na nikafuata ushauri wenu, nadhani tutafanikiwa kumaliza swala hilo wote.

Mwanamke huyu, nimejaribu kila njia chini ya jua kuwa nae baada ya kuhisi penzi letu limeingiliwa lakini imeshindikana , hasikii wala haelewi chochote , nimejidhalilisha sana kwake hata watu wengine wanashangaa ili kunusuru penzi langu lakini wapi, kama najaza maji kwenye gunia.

Nimejaribu kumshauri, kumlinda, kumuongoza kiroho na kimwili, lakini hamna kilichothaminiwa naweza nikasema hivyo, hakuna kitu sijafanya labda ambayo viko nje ya uwezo wangu lakini asilimia kuwa nimejitahidi sana.

Ili nisiwachoshe sana kutokana na uzi wangu wa mwanzo kuomba ushauri kwenu naleta mrejesho wa mwisho kwenu mpaka nilipofikia, ambapo naona ndio mwisho wa penzi langu japo roho inaniuma sana sina namna lazima nikubali matokeo.

12/12/ 2020 naona mwisho wetu hata hivyo sina kinyongo nae namtakia Maisha mema huko alikochagua kama ndio sahihi kwake, nimemwambia mimi nipo akitaka msaada wowote kwangu nipo tayari kumsaidia sina tatizo na yeye, nadhani haikuwa bahati yangu kuwa nae.

Najua hapa hayupo ila D, nakutakia maisha mema yenye furaha na amani, nimejaribu kuwa mtu mwema kwako kiasi cha kuuza na kudhalilisha utu wangu ili niwe na wewe lakini umeamua kuchagua njia yako. Mungu akubariki nashukuru kwa penzi lako nilifarijika sana na hata Mwanaume atakayekuwa na wewe atafaidi pia .

Asante kwa vyote na nadhamini mchango wako katika maisha yangu, nakupenda sana na utaendelea kuwa moyoni mwangu.

Nazileta kwenu baadhi ya text alizonitumia na niliyomjibu

Nawashukuru sana ndugu zangu kwa mchango na maoni yenu, hakika mmekuwa msaada mkubwa kwangu mpaka leo naamua kuagana na mwanamke niliyempenda katika maisha yangu .

Mungu awabariki sanaView attachment 1648854View attachment 1648856
20201213_124710.jpg
 


Kudhamini ❌❌❌
Kuthamini ✔✔✔✔✔

Muache aende.....kuumizwa na mapenzi ni jambo la kawaida na wengi wetu tume/tunapitia hizo hali

Kimsingi kama utakuwa umeamua kuendelea na mambo yako unatakiwa uwe umemaanisha,sio nzuri sana kuonesha udhaifu unaouonesha kwake....atakutesa akiamua

Pole
 
Huyo hakufai piga chini Jomba na ukate kabisa mawasiliano nae, tatizo umeonyesha udhaifu mkubwa sana kujidhalilisha juu yake ndio maana amejiona yeye ni Madini ya Lulu.

Endelea na mishe zako, hasira zako zihamishie kwenye kutafuta pesa na kumuabudu Mungu, huyo atakuja kukutafuta mbeleni ila usimpe nafasi, kwa muda huu usitafute mpenzi mwingine kwa haraka ukidhani kuwa utapoza machungu yako, relax and take ur time mpaka siku za mbeleni huko.

Kumbuka kuwa wewe sio mtu wa kwanza kupita katika hali hiyo, utazoea tu na utakuja kujilaumu sana kwa jinsi ulivyojidhalilisha juu yake.

Keep going brother, maisha lazima yasonge mbele, be happy and enjoy ur life.
 


Nimependa ujasiri wake hana kona kona...unajua siri ya wamawake wa namna hii?
Huwa wanatest mitambo...yaani ashakujua ubora wako na udhaifu wako then anaenda kwingine kuchek...sasa baada ya muda atacompare sample kama tatu amini kwamba kwa hiki alichoandika kama hajafake.....She will definitely come back trust me...2021 haitaisha atarudi na usimpe nafasi akirudi.......
 
Hapa wa kulaumiwa ni wewe. Binafsi napenda mtu akiwa mkweli. Mtu kakuambia hajazaliwa ili akuumize na anafikiri unapaswa kupata kitu bora kwa mema yako, kosa lake ni lipi? Tambua wanawake wanapenda mara moja tu akigeuka umeumia.
 
Kudhamini
Kuthamini

Muache aende.....kuumizwa na mapenzi ni jambo la kawaida na wengi wetu tume/tunapitia hizo hali

Kimsingi kama utakuwa umeamua kuendelea na mambo yako unatakiwa uwe umemaanisha,sio nzuri sana kuonesha udhaifu unaouonesha kwake....atakutesa akiamua

Pole
Asante mkuu
 
Huyo hakufai piga chini Jomba na ukate kabisa mawasiliano nae,tatizo umeonyesha udhaifu mkubwa sana kujidhalilisha juu yake ndio maana amejiona yeye ni Madini ya Lulu,

Endelea na mishe zako,hasira zako zihamishie kwenye kutafuta pesa na kumuabudu Mungu,huyo atakuja kukutafuta mbeleni ila usimpe nafasi,kwa muda huu usitafute mpenzi mwingine kwa haraka ukidhani kua utapoza machungu yako,relax and take ur time mpaka siku za mbeleni huko,

Kumbuka kua wewe sio mtu wa kwanza kupita katika hali hiyo,utazowea tu na utakuja kujilaumu sana kwa jinsi ulivyojidhalilisha juu yake,

Keep going brother,maisha lazima yasonge mbele,be happy and enjoy ur life.
Asante mkuu barikiwa sana
 
Nimependa ujasiri wake hana kona kona...unajua siri ya wamawake wa namna hii?
Huwa wanatest mitambo...yaani ashakujua ubora wako na udhaifu wako then anaenda kwingine kuchek...sasa baada ya muda atacompare sample km tatu amini kwamba kwa hiki alichoandika kama hajafake.....She will definitely come back trust me...2021 haitaisha atarudi na usimpe nafasi akirudi.......
Asante mkuu hata hivyo sijafikiria kuwa nae tena
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom