Re: Ardhi ya kijiji imeporwa. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Re: Ardhi ya kijiji imeporwa.

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by KARLMARX., Jun 7, 2012.

 1. K

  KARLMARX. Member

  #1
  Jun 7, 2012
  Joined: Jun 3, 2012
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwenyekiti wa kijiji amemega ardhi ya shamba la kijiji na eneo la ofisi akauza kwa tajiri mmoja halafu kila anayejaribu kuhoji anaundiwa kesi ya uongo na yule tajiri halafu anawekwa ndani kwa kuhonga hadi kila mtu ameogopa na ukizingatia maisha ya kijijini ukiwekwa ndani familia yako inateseka sana.

  Naomba msaada wa kisheria, ni mbinu gani zinaweza kutumika ili kumshughulikia huyu fisadi?
   
 2. Chipukizi

  Chipukizi JF-Expert Member

  #2
  Jun 7, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 1,970
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Wanakijiji unganeni,andikeni barua na kuisaini wote then waoneni Haki ardhi hawa ni wanaharakati na wanasheria wa maswala ya dhuluma ya ardhi.Pia pitieni na msome sheria ya ardhi za vijiji muangalie iwapo Mwenyekiti amekosea ama la! Isije mnalalamika tu kumbe akuna sheria iliovunjwa! Vipi vikao vya madiwani wenu akijausishwa pia?
   
Loading...