Re - advertised Maafisa mauzo platinum credit Dar Es Salaam

Re - advertised Maafisa mauzo platinum credit Dar Es Salaam

Ukweli mtupu kaka utaskia kamtu kako kamekaa kanakwambia mauzo mbona hakuna akajui unavyo hangaika
 
sawa kama unadhani hatujawahi kufanya hizo kazi, nakuhakikishia kiwa baada ya miezi miwili utakuja tena kutafuta watu sales tena. washaulini hao mabos wenu kuwa mtaani product haziend,na pia nikwambie tu, wao wadada jukumu wanalolifanya ni kuprocess mikopo, baada ya nyinyi kuwa mmewatafuta, kama hujui kazi zao vizur,nenda makao makuu yao, ghorofa ya kumi, ingia kulia, utaona reception, kisha nenda kushoto ingia kwenye ofisi yao,pia kama vip nenda mwisho kabisa kunja kulia utaona meeting room, ukitoka hapo, ingia upanda wa kulia utaona ofisi ya washua, nimekupa picha zote kukwambia kuwa nafahamu iyo kazi.[/

🧐🧐🧐🧐
 
tatizo LA platinum ni kwamba wanategemea watumishi tu,so kwa sasa watumishi wamestuka kukopa kwenye tasisi kama hizo maana wamekwidwa riba kubwa sanaaa.sasa kasheshe inakuja kuwapata hao wateja,na ndio maana wanatanganza kazi kila kukicha za mafisa mauzo.,kuna hawa platinum,ASA, beibort na wengine, kazi ni ngumu kuwapata na hapo hapo utawakuta wale makao makuu vikinadada vinapigwa kiyoyozi pale wanakupigia kelele kuwa mbona umepata wateja wachache.....Siku moja waambieni watoke gorofani waje watafute wateja watano tu kwa mwezi, uone kama watapata hata mmoja......kazi ya sales ni ngumu kuliko kazi yoyote kwenye taasisi na nashangaa hawathaminiwi.ningekuwa Mimi kwenye kampuni yangu watu ambao wangekuwa wa commission au part time ni..............
Hao vidada kwa kikupwe
 
Watumishi bado ni wengi wana endelea kukopa na wataendelea kukopa kwa sababu tupo tayari kuwasaidia kutatua matatizo yao ya haraka.Katika kazi kila mtu ana majukumu yake hao wadada wa ghorofani una waita na nukuu wanafanya kazi ya kutafuta wateja kwa njia ya simu yaani 'telesales' na wanapata wateja wengi sana kwanini wewe unaye onana na wateja usiweze kupata na kujipatia kipato.
Kwa Riba kubwa?....



HAPANA

ODEEEEEE!!!!!!

DOHOOOO!!!!
 
Riba kwetu sio tatizo na malalamiko ya riba ni machache sana kwani riba ana jichagulia mtumishi kutokana na muda atakao kaa na mkopo wetu hivyo mtumishia akimaliza kutatua shida yake anafuta mkopo muda wowote.Watumishi wengi wanafurahia huduma hii na wanakuja kwetu kukopa kila mara anapo pata shida ya haraka.Mikopo yetu ni ya dharura ndani ya masaa 24 unakua umewekewa kiasi ulicho omba.

Kiongozi mkitaka sales iwetamu na simple kwenu lazima mkubi kubadilika kwendana na demand na uchumi afu pia management iwe na nguvu usifikiri hatujui yanayotendeka uko, tuna ndugu zetu walishafanya kazi uko na wapo wanaoendelea fanya kazi hakuna ata mmoja anaejivunia izo kazi zenu kwanza asilimia 90% wanakufa maskini tena na stress juu, kijimshahara cha laki 5 au laki 6 umpige namakato kama kodi, nssf unazani anabaki na kiasi gani?

Alafu maajabu eti mnakopesha wengine nyie mnashindwa kopeshana si upuuzi huu, mkitaka mfaidi ili soko la Magu lazima mkubali kubadilika lijikampuni gani miaka zaidi ya 10 halibadiliki eti boss wenu anakuja kutoka sijui south sijui kenya anafananisha nchi mbili tofauti huu niumama wa hali ya juu anasahau katika business kuna. Factor inaitwa environment inayobeba mambo mengi.

Afu kingine mnakua na turnover kubwa kila siku mnavijimikataba vya mwaka mmoja mmoja mnaenda mna renew huu kwangu ni ungese sana siwezi mruhusu ndugu yangu akafanya kazi uko anapoteza muda wake maana unaweza kuta mtu ni mzuri na alikua na mkataba wake mzuri mahala mnamchukua kwa kisingizio cha maslahi mazuri then akifeli kuendana na strategy then mnamtoa “ mmeshawai jiuliza kwanini staff alikotoka alikua bora kwenu ameshindwa?

Kiufupi lijikampuni lenu ni uswahili mwingi na HR Wenu nae ajielewi sijawai skia taasisi ina ajiri kalibia kila mwezi na kila baada ya miezi 4 wanaachishwa kazi zaidi ya watu 10
Hr gani ajui kuangalia administrative cost na hajali kabisa

Afu pili mnaundugu laizesheni wachaga au watu wa Arusha kama wote kampuni mzima.

Afu watu wenye skills wanaachwa wanawekwa watu wa janja janja sijui papaa fallyipupa
Kiufupi dunia ya sasa kaka hautapata sales officer zaidi ya 30 kwa mwezi ukijitahid sana utapata 5 washamba wasioelewa baadae watasepa , wataweza kaa kama wana base ya customer kubwa au kama hawana kazi za maana ila kwa mtu anaejielewa awezi jihusisha nayo
Riba ya 3.75 kwa mwaka ni 45 yani nikope mkopo wa 5 million kwa miezi 60 nirudishe M 15 uku ukiwa bank unakopa zaidi ya milion 5 tena kwa muda ule ule alafu mnakuja na kigezo cha kutoa mkopo wa dharura eti kwa masaa 24

Kwanini ampati wateja wa TRA au bandari mnakomaa na waalimu na wauguzi ndo mmeona maboya.
Mauzo yenu yatashuka sana mpk mtatafuta mchawi ni nani kumbe ni riba na upumbavu wa management ambayo haina final say inapokea order tu
 
Nimejaribu kufanya research ya kutosha wiki nzima kujua hawa jamaa wanalipa vipi hao watu wao wa sales so iko hivi wanalipana 1.0% ya total amount ya mikopo waliyotoa.kwa hesabu ya kawaida ni kama ifutavyo
1.0%÷100=0.01
Huyu mtu wa sales ameuza mikopo yenye jamani ya 30,000 kwa mwezi so itakuwa 0.01*30000000=300000 kwa hyo shilling lakitatu ndo mshahara wa mwezi so hapo tunatoa
Commission 300000
Tax (54,000)
NSSF (30,000)
NHIF (20,000)
Mshahara net ni 196,000 na hapo umejitahidi sana kufanya kazi so kuna watu huu mwezi wa 3 hajapata chochote sasa unasema hii ni kazi si Bora mtu afanye hata internship mahali

Kaka awa jamaa kuna ndugu yangu yupo uko analalamika kinoma soko gumu wenzao wanabadika wanamakato mpka ya 2000 wao wako pale pale

Wanatoa commission yaasilimia 7 kwa kila mteja alafu wanakupa na pesa nyingine sijui ya kuzungukia kila upatapo mteja, tatizo ni kua utapata mteja unaweza zunguka dsm nzima kwa pesa yako mwezi mzima ukaja pata mteja wa laki 4 sasa laki 4 x 7% ni sawa na 28,000 wakikupa na kaela ka kupata mteja kama kaposho apo haifiki ata 60 elfu
Sasa piga mahesabu mwezi mzima umetumia nauli kiasi gani, muda kiasi gani afu unakuja lipwa mfano iyo elfu 60 inayopigiwa kodi ya magu na nssf si bora mtu afanye kibarua cha 10 per day
 
Riba kwetu sio tatizo na malalamiko ya riba ni machache sana kwani riba ana jichagulia mtumishi kutokana na muda atakao kaa na mkopo wetu hivyo mtumishia akimaliza kutatua shida yake anafuta mkopo muda wowote.Watumishi wengi wanafurahia huduma hii na wanakuja kwetu kukopa kila mara anapo pata shida ya haraka.Mikopo yetu ni ya dharura ndani ya masaa 24 unakua umewekewa kiasi ulicho omba.

Tatizo lenu ni kutokutoa settlement kwa wakati
Kuwadanganya wateja , mkiwa mnajaza mikataba muwaambie ukweli kua ukikopa milioni 6 kwa miezi mfano 72 atalipa 18M na mnapo jaza zile karatasi za kuingiza makato muwape waone kama wateja mtawapata zaidi ya hapo ni janja janja tu
Mnatumia nguvu nyingi sana kuuza product yani mnaiforce sana mnashindwa ata na TRA Saccos afu mnajiita international microfinance with more than 50 branches

Afu kiongozi kingine mwambie boss wako yule papaa mzeee wamisifa atauwa kampuni asizani porojo zinaesabika au saidia katika mauzo
Mkubali badili riba other wise mtakua mnapata wateja wa manati yani dsm yenye taasisi kama zote unakuta mnapata mauzo ya milion 15 apo ndo mmejitahidi uku watu kma URU SACCOS ya walimu au TRA Saccos wanauza mpk 400 milion dsm tu
 
tatizo LA platinum ni kwamba wanategemea watumishi tu,so kwa sasa watumishi wamestuka kukopa kwenye tasisi kama hizo maana wamekwidwa riba kubwa sanaaa.sasa kasheshe inakuja kuwapata hao wateja,na ndio maana wanatanganza kazi kila kukicha za mafisa mauzo.,kuna hawa platinum,ASA, beibort na wengine, kazi ni ngumu kuwapata na hapo hapo utawakuta wale makao makuu vikinadada vinapigwa kiyoyozi pale wanakupigia kelele kuwa mbona umepata wateja wachache.....Siku moja waambieni watoke gorofani waje watafute wateja watano tu kwa mwezi, uone kama watapata hata mmoja......kazi ya sales ni ngumu kuliko kazi yoyote kwenye taasisi na nashangaa hawathaminiwi.ningekuwa Mimi kwenye kampuni yangu watu ambao wangekuwa wa commission au part time ni..............
Umeongea ukweli kabisa hawa watu wanasubiri watumishi tu na ukitaka kuamisha mkopo kwenda labda NMB hawataki, bayport, platnum, faidika sijui fanikiwa washakuwa bomu.
 
Watumishi wa serikali wata endelea kukopa mpaka mwisho wa dunia na tuna washukuru kwa kutupongeza kwa huduma zetu nzuri na tuna ahidi kuendelea kuwapa huduma nzuri kila kukicha.Kamisheni zetu ni nzuri sana na maafisa mauzo wengi wana zifurahia maana tuna lipa mara mbili kwa mwezi.
Tatizo lenu nyie ni waongo siyo watu wa ahadi
 
Tatizo lenu ni kutokutoa settlement kwa wakati
Kuwadanganya wateja , mkiwa mnajaza mikataba muwaambie ukweli kua ukikopa milioni 6 kwa miezi mfano 72 atalipa 18M na mnapo jaza zile karatasi za kuingiza makato muwape waone kama wateja mtawapata zaidi ya hapo ni janja janja tu
Mnatumia nguvu nyingi sana kuuza product yani mnaiforce sana mnashindwa ata na TRA Saccos afu mnajiita international microfinance with more than 50 branches

Afu kiongozi kingine mwambie boss wako yule papaa mzeee wamisifa atauwa kampuni asizani porojo zinaesabika au saidia katika mauzo
Mkubali badili riba other wise mtakua mnapata wateja wa manati yani dsm yenye taasisi kama zote unakuta mnapata mauzo ya milion 15 apo ndo mmejitahidi uku watu kma URU SACCOS ya walimu au TRA Saccos wanauza mpk 400 milion dsm tu
Duuuh
 
tehe tehe tehe.......ukiona wanarudiarudia tangazo ujue wanakimbia sana hiyo nafasi.
kwanza wakopaji wengi saizi hukopa vikoba na kwene vikundi. kumshawishi mtu huku umwambie awake hati, Mara mali zake lehani nani ...
 
Back
Top Bottom