Re - advertised Maafisa mauzo platinum credit Dar Es Salaam

Re - advertised Maafisa mauzo platinum credit Dar Es Salaam

albertno

Member
Joined
Sep 6, 2016
Posts
36
Reaction score
8
Sales Representatives (Afisa Mauzo)
Platinum Credit Ltd ni kampuni inayotoa huduma ya mikopo ya dharura kwa watumishi wa serikali ya Tanzania na wafanya biashara raia wa kitanzania wa rika la kawaida na rika la kati. Kampuni imejizatiti kuhakikisha huduma zake kwa wateja zinapatikana ndani ya muda wa saa 24.
Katika kuimarisha juhudi zake za kutoa huduma inayoridhisha kwa wateja wake, Kampuni inatangaza fursa ya ajira kwa vijana watanzania kama ifuatavyo:
  • Nafasi : Afisa Mauzo ( Nafasi 30)
  • Eneo la kazi: DAR ES SALAAM
  • Majukumu
a) Kupanga sehemu ya kwenda kufanya mauzo
b) Kushiriki katika shughuli za masoko na kutangaza bidhaa za kampuni
c) Kujibu maswali ya wateja
d) Kusaidia wateja kujaza fomu pamoja na nyaraka zinazohitajika
e) Kutoa ushauri juu ya mkopo wa kujaza na jinsi ya kusitisha mkopo kwa wateja waliopo
f) Kuwasiliana na meneja wako wa tawi kuhusu changamoto unazozipata sokoni
g) Kufuatilia wateja waliohama /wasiolipa
h) Kushirikiana na viongozi wa tawi kuidhinisha na kuingiza makato kwa mwajiri kwa kila mkopo
iv. Sifa za muombaji
a) Awe na elimu isiyo chini ya kidato cha Nne.
b) Awe mwenye kujituma kutafuta masoko na kuhudumia wateja
c) Awe na utayari na uwezo wa kujifunza kazi kwa haraka.
d) Awe na uwezo wa kuongea vizuri Kiswahili
e) Awe na lugha nzuri ya kuongea na wateja na kushirikiana na wafanyakazi wenzake.
f) Awe mwaminifu kwa wateja na kujitambua katika kazi na maisha binafsi.
g) Awe na umri usiopungua miaka 20.

v. Jinsi ya kutuma maombi
Muombaji anaweza kutuma maombi yake kwa njia mojawapo ya hizi zifuatazo:

a)*Maombi yaambatane na:
ü Nakala ya wasifu wa muombaji,
ü Nakala ya veti vya muombaji,
ü Picha ndogo(passport size) mbili za karibuni.

Barua pepe: maxmasoko@gmail.com
Imetolewa
Utawala,
Platinum Credit Ltd,
Makao Makuu-Dar es Salaam.
 
Kazi za kuzunguka jua kali mchana kutwa hazina tofauti na forever living
 
tatizo LA platinum ni kwamba wanategemea watumishi tu,so kwa sasa watumishi wamestuka kukopa kwenye tasisi kama hizo maana wamekwidwa riba kubwa sanaaa.sasa kasheshe inakuja kuwapata hao wateja,na ndio maana wanatanganza kazi kila kukicha za mafisa mauzo.,kuna hawa platinum,ASA, beibort na wengine, kazi ni ngumu kuwapata na hapo hapo utawakuta wale makao makuu vikinadada vinapigwa kiyoyozi pale wanakupigia kelele kuwa mbona umepata wateja wachache.....Siku moja waambieni watoke gorofani waje watafute wateja watano tu kwa mwezi, uone kama watapata hata mmoja......kazi ya sales ni ngumu kuliko kazi yoyote kwenye taasisi na nashangaa hawathaminiwi.ningekuwa Mimi kwenye kampuni yangu watu ambao wangekuwa wa commission au part time ni..............
 
Kumshawishi mtu aje kukopa napo ni kazi aisee
 
Back
Top Bottom