Homa la jiji
Senior Member
- Jan 13, 2014
- 129
- 28
Mimi ni mmoja ya waathirika wa utendaji wa RCO huyu aliniomba rushwa ya sh. Milioni 3 nikapuuza mpaka sasa miezi 7 faili langu naambiwa bado linaendelea na uchunguzi na amekua akifanya hivyo kwa baadhi ya watu ambao anajua wana uwezo wa kifedha hata kama ushahidi hakubani yeye anaweka uzito ili uogope utoe pesa.
Kuna siku tulikua tumekaa nje ya ofisi yake watu wanne tukisubiri huduma kila mmoja wetu alizungumzia kuombwa rushwa tena sio chini ya milioni moja na usipo toa anaanza kujenga mazingira magumu kwenye tuhuma zako ili uwe mtuhumiwa kamili au anakuchelewesha makusudi kwakukuambia uchunguzi bado unaendelea miezi mingi itapita yaani kamwa mungu mtu huyu RCO
Mimi binafsi nimechoshwa na utendaji wake na nina ushahidi wa kutosha nilishawahi kuufikisha TAKUKURU nao wakamgwaya wakaniambia kua niupeleke kwanza ushahidi ule kwa RPC akishindwa kunisikiliza bas ndipo nirudi kwao yaani anaweza akakuzungusha kwa jambo la wazi kabisa du anakera