Mwandishi ahukumiwa kwenda jela miezi 8 kwa kuomba na kupokea rushwa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,007
9,873
Mwandishi wa habari wa kujitegemea wa Mkoani Kilimanjaro, Patrick Chambo amehukumiwa na Mahakama ya Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, kwenda jela miezi minane kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa.

Hakimu wa mahakama ya Wilaya ya Babati Victor Kimario ametoa hukumu hiyo ya kesi ya CC 14/2019 Novemba 24 mjini Babati.

Hakimu Kimario ametoa hukumu hiyo baada ya waendesha mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Takukuru, Martin Makani na Evelyn Onditi kuiomba Mahakama hiyo kuendelea na hatua ya hukumu baada ya mshtakiwa kuruka dhamana.

Chambo aliruka dhamana ya mahakama hiyo baada ya upande wa mashtaka kukamilisha ushahidi na Mahakama hiyo kutoa uamuzi mdogo kuwa Chambo ana kesi ya kujibu hivyo badala ya kujitetea akaruka dhamana na kujinyima haki ya kusikilizwa ila hati ya kumkamatwa ili atumikie kifungo imeshaandaliwa.

Awali, Chambo alifikishwa Mahakamani hapo na kushtakiwa kosa la kuomba rushwa ya shilingi 300,000 na kupokea rushwa ya shilingi 100,000.

Amesema Chambo aliomba rushwa hiyo kutoka kwa mkurugenzi wa kampuni ya kiwanda cha maji Mati Super brands ya Mjini Babati, akidai kuwa wamekwepa kulipa kodi.

Amesema Chambo alimueleza Mkurugenzi huyo kuwa endapo wasingempatia kiasi hicho cha fedha angewaandika kwenye vyombo vya habari kuwa wanakwepa kodi ya serikali.

Amesema Mkurugenzi wa kampuni hiyo alifikisha malalamiko hayo TAKUKURU ambao waliweka mtego na kumkamata Chambo kisha kumfikisha Mahakamani na kuhukumiwa.

Mkuu wa TAKUKURU Mkoani Manyara Holle Joseph Makungu ametoa rai kwa waandishi wa habari kuwa endapo watabaini ushahidi wa kukwepa kodi watoe taarifa Mamlaka ya mapato nchini TRA au TAKUKURU.

Makungu amesema na kukamatwa kwa Chambo walifanya uchunguzi na kubaini ni kweli kampuni ya Mati Super brands Ltd ilikwepa kodi zaidi ya shilingi milioni 5.

"Tuliitaka kampuni ya Mati Super brands Ltd kulipa kodi hiyo iliyokwepa shilingi milioni 5 na adhabu ya shilingi milioni 50 kwenye mamlaka ya mapato nchini TRA na wanaendelea kufuatilia mienendo ya ulipaji kodi wa kampuni hiyo ili mapato halali ya serikali yasihujumiwe.

"Watu wa Manyara tukumbuke kuwa hakuna haki wala wajibu hivyo kila mmoja ana haki ya kufanya biashara halali inayomwingizia faida ila ni wajibu alipe kodi halali kwa maendeleo ya Taifa" amesema.

Amesema endapo kuna mwananchi anataarifa ya kampuni inafanya biashara bila kulipa kodi anapaswa kutoa taarifa TRA au kwa Mkuu wa TAKUKURU Mkoani Manyara kwa namba za simu 0738150124 kwa manufaa ya Taifa.

Amesema endapo suala hilo likijitokeza ni bora taarifa zitolewe na hatua kuchukuliwa kama zilivyochukuliwa kwa kampuni ya Mati Super brands Ltd kuliko kufanya kama chambo alivyofanya na kuhukumiwa kwenda jela.
 
Back
Top Bottom