RC wa Mbeya azuia watumishi kuchukua likizo

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,650
218,113
Haya ndiyo Maajabu ya Tanzania, Wakati wanafunzi ambao ni binadamu wakizuiwa kuendelea na masomo wakati wa likizo kwa madai kwamba wanapaswa kupumzika, binadamu wenzao ambao ni Watumishi wa umma hawatakiwi kwenda likizo na wanatakiwa kufanya kazi kama punda!

Uamuzi huu umetolewa na serikali ileile, ila safari hii aliyekataza watumishi kupumzika ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kama alivyonukuliwa na Mwananchi.

Sasa sijui tushike lipi tuache lipi?

-----
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya (RC), Juma Homera amefuta likizo kwa watumishi wote wa Serikali mkoa huo ambao idara zao zinahusika na ujenzi wa miradi ya miundombinu ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na madawati ambapo tayari Serikali imetoa fedha za miradi hiyo.

Homera ametoa agizo hilo leo Jumanne Desemba 7, 2021 wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Mwakibete alipotembelea chanzo cha maji cha Nzovwe kinachosimamiwa na Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira (Mbeya-Uwwas) huku akibainisha kufuta likizo kwa wakuu wa Wilaya, wakurugenzi wa halmashauri zote, maofisa manunuzi, watendaji wa kata, wahasibu na watendaji wa idara zingine za Serikali.

Amesema kuwa hatoweza kupokea barua za likizo pasipo kupata taarifa za kukamilika kwa ujenzi wa miradi ya madarasa, madawati na maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya wafanyabishara wadogo maarufu kama machinga.

''Hata mimi mwenyewe siwezi kwenda likizo wakati huu ambao Serikalini inaendelea kutoa fedha za miradi sasa nimefuta likizo zote mpaka hapo nitakapojiridhisha miradi hiyo imekamilika kwa wakati ili watoto waingie madarasani kusoma maeneo salama Januari 2022''amesema

Ameongeza kuwa ''Labda mtumishi augue na atakiwe kupelekwa kutibia katika hosptali ya Taifa Muhimbili lakini pia nitaangalia vigezo kama ugonjwa wanaougua utashidwa kutibika katika hosptali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya''amesema.

Chanzo: Mwananchi
 
Haya ndiyo Maajabu ya Tanzania, Wakati wanafunzi ambao ni binadamu wakizuiwa kuendelea na masomo wakati wa likizo kwa madai kwamba wanapaswa kupumzika, binadamu wenzao ambao ni Watumishi wa umma hawatakiwi kwenda likizo na wanatakiwa kufanya kazi kama punda!
WAtumishi wanakaa kazini toka January - December na ukitembelea ofisi nyingi za umma ni stori, kunywa chai, n.k. Ikifika December hali inabadilika wakuu wa mikoa wanapiga marufuku likizo, as if kazi zote za serikali zinatakiwa kufanywa December. Nchi hii haina taratibu za kazi ni mihemko tu
 
Likizo ni sharti la kisheria. Wafanyakazi hao ni wajinga hawataenda mahakamani.
Ni sharti la kisheria lakini huambatana na shrti kutoka kwa boss wako.
Boss wako anapokua na kazi ya kukupa, anaruhusiwa kukunyima likizo.
Hapo ndio ubaya wa kuajiriwa unapokuja. HUTAPATA likizo mpaka boss wako aamue
 
Tatizo watu wanasubiri Krismas ndipo waende likizo, unakuta idadi kubwa ya watumishi wanaondoka kwenda Likizo hii inakuwa kama vile serikali inaenda likizo.

Naunga mkono sababu za kumalizia miradi hasa inayohusu wanafunzi wanaoingia form one na darasa la kwanza mwakani. Uzuri wake amesema mradi ukikamilika atapokea hizo barua za likizo. - Nadhani hakuna tatizo.
 
Haya ndiyo Maajabu ya Tanzania, Wakati wanafunzi ambao ni binadamu wakizuiwa kuendelea na masomo wakati wa likizo kwa madai kwamba wanapaswa kupumzika, binadamu wenzao ambao ni Watumishi wa umma hawatakiwi kwenda likizo na wanatakiwa kufanya kazi kama punda!
Sema wewe muuza mayai hujui mambo ya utumishi wa umma majukumu ya RAS na DAS ndio unapiga kelele tu

USSR
 
Tatizo watu wanasubiri Krismas ndipo waende likizo, unakuta idadi kubwa ya watumishi wanaondoka kwenda Likizo hii inakuwa kama vile serikali inaenda likizo.
Naunga mkono sababu za kumalizia miradi hasa inayohusu wanafunzi wanaoingia form one na darasa la kwanza mwakani.
Uzuri wake amesema mradi ukikamilika atapokea hizo barua za likizo. - Nadhani hakuna tatizo.
Taasisi yoyote yenye utawala unaojielewa wanaandaa leave roster kila mwanzo wa mwaka. Kwa hiyo hii shida ya likizo kujirundika mwezi mmoja haijitokezi, kwa sbabu afisa utumishi atakuwa ameshandaa utaratibu wa likizo kwa kuzingatia kuwa shughuli za serikali zinatakiwa kuendela
 
Kama umenisoma vizuri ni kwamba na wewe una akili kama hao wafanyakazi wasioenda mahakamani.

Mahakamani huwezi kuongea unayosema, ni vifungu vya sheria tu.

Ni sharti la kisheria lakini huambatana na shrti kutoka kwa boss wako.
Boss wako anapokua na kazi ya kukupa, anaruhusiwa kukunyima likizo.
Hapo ndio ubaya wa kuajiriwa unapokuja. HUTAPATA likizo mpaka boss wako aamue
 
Alipaswa aseme wachache watakaobaki wajipange huduma chache muhimu kama hospitali, Polisi n.k zisisimame.

Mwezi wa 12 hadi mid of the following January watu wengi huenda mapumziko ya siku kuu za mwaka makundi mengi ya jamii ikiwemo wafanyabiashara, wafanyakazi, n.k

Kukatalia watu rikizo kutaka sifa haisaidii maana wataenda ofisini lakini watabaki idle bila kuhudumia yeyote maana wale wa kuhudumiwa na wenyewe wameenda mapumziko.
 
Watumishi wa umma ni kikundi cha watu kisichojitambua.
Likizo zipo kwa mujibu wa sheria, anatokea muhuni mmoja aliyepewa cheo cha kikoloni anajamba .... likizo hamna bila kudurusu popote?
Gazeti nalo bila kwenda ndani na kumuuliza sheria zinasemaje lina andika tu. Nasi wasomaji tunasoma bila kuhoji
Ghhhhhj
 
Back
Top Bottom