RC Tanga Kuwafukuza VEO Handeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

RC Tanga Kuwafukuza VEO Handeni

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by IshaLubuva, Sep 18, 2009.

 1. I

  IshaLubuva JF-Expert Member

  #1
  Sep 18, 2009
  Joined: Dec 4, 2008
  Messages: 248
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Jana kwenye Taarifa ya habari ya Runinga ya Channel Ten RC wa Tanga aliwachimba mkwara Watendaji wa Vijiji katika Wilaya ya Handeni kuwa kama hawatasimamia vizuri mazao yanayovunwa sasa na wakulima wa maeneo yao ya kazi na badala yake wananchi/wakulima wakayauza na hivyo kupelekea kuibuka kwa upungufu wa chakula hatasita kuwafukuza. Alisema kuwa VEO yeyote atakayeenda na maelezo ya kuwa na upungufu wa chakula katika eneo lake la kazi aende pia na barua ya kujiuzulu kazi.

  Wana JF hebu tujiulize:

  1) VEO anawezaje kumzuia mkulima, ambaye anakabiliwa na matatizo, mathalani kuuguliwa au mwanae kudaiwa ada ya shule, kuuza mahindi yake ili akabiliane na kadhia hiyo?

  2) Je hili ni jukumu mojawapo la kazi za VEO kuzuia wakulima kutouza mazao yao (mkulima mwingine mahindi ni zao lake la biashara) au ndo hali ya uonevu wa kiutendaji?

  3) Kwa ufahamu nilionao RC hawezi (kama sheria za utumishi wa umma zitazingatiwa) kumfukuza kazi VEO kwa kutosimamia wakulima ili wasiuze mazao yao, ila ninachijiuliza ni nini anataka kutufundisha huyu RC?; kwamba anayo madaraka yanayovuka sheria au haelewi ukomo wa mamlaka yake?. Hii ilinifanya nimkumbuke enzi za Waziri Mkuu Sumaye alivyowachimba mkwara maDC kuwa yeyote atakayesema Wilaya yake ina njaa nayeye ajihesabu kazi basi

  Hali hii kila mara huwa inanifanya kuwa na mashaka ya uwezo wa viongozi wanaotokea kwenye ustaafu wa Jeshi na hasa ukizingatia kuwa wakati ule waliokuwa wakienda kwenye kazi za majeshi walikuwa wale waliokosa nafasi za kuendelea na Kidato cha nne au kwenye vyuo
   
 2. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #2
  Sep 18, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  VEO stand for what?
   
 3. I

  IshaLubuva JF-Expert Member

  #3
  Sep 18, 2009
  Joined: Dec 4, 2008
  Messages: 248
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  VEO stand for Village Executive Officer au kwa Kiswahili ni Afisa Mtendaji wa Kijiji
   
 4. MwalimuZawadi

  MwalimuZawadi JF-Expert Member

  #4
  Sep 18, 2009
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 643
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hivi vyeo vingine vilifaa tu wakati wa Nyerere
   
 5. O

  Omumura JF-Expert Member

  #5
  Sep 19, 2009
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Naunga mkono tamko la huyo RC,huko vijijini hao ma VEO wanaishi kama miungu watu fulani hivi, kazi ni kupiga wananchi na kunywa gongo usiku na mchana bila kusimamia wananchi walime!Tulipofikia baadhi ya watanzania wavivu ni kuacha porojo na kulalamika ovyo ili tuondokane na umaskini, tufanye kazi tuache porojo na mbwembwe za kulalamika vijiweni!
   
 6. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #6
  Sep 19, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Duh! Barubaru kweli wewe unaishi Doha
  hujui hata VEO inasimama kama nini
  kwani wewe uliondoka lini kijijini kwenu Kwemazandu?
  ila naona umeshajibiwa, hongera kwa kufahamu sasa
   
 7. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #7
  Sep 19, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kwanini?
   
 8. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #8
  Sep 19, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  VEO kwa mtazamo wangu bado wana umuhimu mkubwa san kwenye ngazi ya kijiji kutokana na kuwa wengi wao huwa wanatokea nje ya vijiji husika kwahiyo kutoa changamoto katika kuleta maendeleo ya kijiji husika. Pia umuhimu wao ni kutokana na wenyeviti wengi kuwa na uelewa mdogo kwenye kuandaa michakato mingi kuhusiana na maendeleo ya kijiji kwahiyo hawa VEO hutumia elimu yao ya kidato cha nne na kuendelea katika kusukumu gurudumu la maendeleo mbele.
  Lakini pia hawa VEO wana udhaifu wao kwenye maeneo mengi kama alivyosema mdau mmoja kuwa wanonekana kama miungu watu huko vijijini kiasi cha kutumia madaraka yao kunyanyasa wananchi kwa kuwapiga na kuwaweka ndani kwa kutumia mgambo wa kijiji. Pia wanahusika sana katika kuuza rasilimali za vijiji kama vile ARDHI kwa wawekezaji kwa mikataba feki na kwa kutowashirikisha wananchi wa vijiji husika.
   
Loading...