RC Paul Makonda atoa miezi michache mpaka Januari kila kampuni na taasisi iajiri walemavu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
RC wa Dar, Paul Makonda amesema kwa mujibu wa Sheria ya Watu wenye Ulemavu ya mwaka 2010 namba 9, kifungu cha 31 kila Mwajiri mwenye wafanyakazi 20 na zaidi anatakiwa kutenga 3% kwa ajili ya walemavu

Asema jijini Dar kuna Makapuni, Mashirika na Taasisi zisizopungua 300 ambazo hayajatoa fursa kwa watu wenye Ulemavu kupata ajira

Amesisitiza "Hatuombi wapate ajira kwa upendeleo kwa kuwa ni Walemavu bali ni matakwa ya kisheria yanayowataka waajiri wote kuzingatia sheria"

Matokeo yake ni kwamba ukatili wa kuwaua watoto wanaozaliwa na ulemavu kwa kuonekana ni mzigo utaondoka kwa kuwa itaonekana kuwa wananafasi ya kufanya vizuri katika jamii

Aidha, amesisitiza kuwa jiji la Dar lazima liwe la mfano katika kusaidia walemavu ambao ni asilimia 9.3 ya Watanzania wote
Dnh06ccWsAUvQgA.jpg


Bongo 5
 
Hii ni dunia ya ushindani ubashite pelekeni koromije!.. Kuna watu competent na viungo vyote hawana kazi. Kama ulemavu ndio sababu ya kutotoboa maisha wakawajaze maofisini kwao!.
Hela ya mshahara natoa mwenyewe unipangie wa kuajiri!
 
RC Paul Makonda ameyataka Makampuni yote Jijini Dar Es Salaam kuajiri watu wenye ulemavu kama sheria ya nchi inavyotaka.

"Nawapeni muda wa miezi hii michache, ifikapo mwezi wa kwanza mwakani tunataka kuona kila Kampuni, kila Taasisi inakuwa na mfanyakazi mlemavu"

View attachment 872144

Bongo 5
BASHITE kabla ya kuja na mengine mapya ungetueleza kwanza yale ya matunzo kwa watoto imeishia wapi? vipi kuhusu zile cv ulizokusanya pale leaders wale vijana wameshapata kazi
 
Sio kwamba hatupendi...idea zake ni nzuri sana
Kitu ambacho hatupendi ni unafiki wa kuja na macamera wakati utekelezaji ni 0..
Angalia project gani aliyoanzisha amewahi kuikamilisha.. hakuna hata moja zote ni sinema za mapicha picha tu
Mbona kuna moja mbichi kabisa ya juzi ya huko Ukonga. Ilifanikiwa sana na "cheaz" zikagongwa mbele ya makamera.
 
Huyu hana ubunifu wowote, ajira zote zinahitaji sifa husika, pia sekta binafsi zipo vibaya kipindi hiki kutokana na uchumi kutokuwa rafiki
 
Back
Top Bottom