RC Mrisho Gambo, amsimamisha kazi Afisa Elimu wa Mkoa wa Arusha

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amemsimamisha kazi Ofisa elimu wa mkoa huo Gift Kyando kwa madai ya kuzuia wanafunzi waliochaguliwa kuingia kidato cha kwanza huku akilazimisha kila darasa kuwa na wanafunzi 40 tu.

Pia anadaiwa kusababisaha wanafunzi hao kukosa nafasi za masomo kwa kukataa kusajiliwa kwa shule mbili mpya za Oldonyowasi na Losikito kwa madai ya kukoda mahabara.

Gambo amesema kitendo hicho ni cha kukwamisha juhudi za serikali kupitia ilani ya chama cha mapinduzi kwa kuwa uamuzi aliouchukua Ofisa huyo haukumuhusisha kiongozi yeyote yule wa serikali ngazi ya wilaya au mkoa

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Arusha Dk. Wilson Mahera amesema kitendo hicho alichokifanya ofisa huyo kiliwachanganya na kusababisha ugomvi kati yao na wazazi wa wanafunzi hao

Amesema ofisa huyo angesababisha wanafunzi 6,819 kukosa elimu wakati yapo madarasa ambayo yaliachwa na wanafunzi waliohitimu kidato cha nne ambayo yangeweza kutumiwa na wanafunzi hao

'' Madarasa yaliyopo yangeweza kuchukua wanafunzi kwa kipindi kifupi wapatao 55 kwa darasa moja '' alisema Mahera.Dkt. Mahera amesema kuhusu mapokezi wanafunzi kati ya shule 4239 wameshapokelewa katika shule 28 za halmashauri ya Arusha wakiwemo wavulana 1,853 na wasichana 2,386 ambao ni sawa na asilimia 62 huku waliobakia wakiendelea kuripoti na wengine wakichukua fomu za kujiunga.

Kwa upande wake Mwenyakiti wa CCM mkoa Loata Sanare amesema alichokiona ni hujuma za waziwazi kwa ofisa huyo dhidi ya serikali na kutaka kuzuia wanafunzi wasianze masomo.Sanare anasema alianza kupokea simu za malalamiko kutoka kwa wazazi wawanafunzi hao na alipompigia ofisa elimu huyo alimjibu majibu ambayo hayakumridhisha ndipo alipoamua kuwasikiana na mkuu wa mkoa.
 
Kimsingi gambo hana mamlaka ya kusimamisha ofisa elimu kazi kwa sababu ofisa huyo akienda mahakamani kukata rufaa atamshinda kwa kishindo maana alicho fanya ofisa elimu huyo ni kufuata sheria ambayo inaimbwa kila siku na serikali hii kwa ni lazima tufuate sheria

Sheria ya elimu inasema darasa moja watakaa wanafunzi 40 na si zaid ya hapo sasa sijui gambo katumia kigezo gani kufukuza kazi na hayo mamlaka kayatoa wapi

Nisawa na dereva kuzidisha abiria kwenye basi au hilo hawalioni au kufuata sheria kuna kundi linatakiwa kufuata na lingine halitakiwi kufuata ? Kuna shida kwa mkuu wetu huyu wa mkoa nitamtafuta private nimshauri atumie busara zaidi kuliko mihemko
 
awamu hii kila mtu kwenye nafasi yake anainua mapembe!
Elimu ni kundi linalo onewa sana na hawa wakuu wa mikoa na wilaya NA WAZIRI WA WIZARA HUSIKA YUPO TUU HASEMEI WIZARA YAKE SIJUI NI WAZIRI WA KITU GANI KAMA WIZARA YAKE INAINGILIWA NA KILA MTU

maana hata wao wakuu wa mikoa na wilaya wanavunja sheria hawasikii ealisha ambiwa na mamla ya utumishi kuwa mkuu wa wilaya au mkoa hana mamlaka ya kusimamisha kazi mtumishi yeyote yule maana sio mamlaka yao lakini nao wana vunja sheria hawasikii wanakaidi mamlaka

Huyo ofisa elimu aandike barua kwa mkuu wa mkoa akiambatajisha na waraka wa elimu ili huyo mkuu wa mkoa ausome vyema aache kuendesha mkoa kwa kichwa chake atumie sheria
Na sijui ni lini tanzania tutaacha kuchanganya SIASA na maswala ya kitaaluma maana hapo naona kuna CCM sijui wameingiaje hapo wakati haya ni maswala ya yasio husu SIASA
 
Afisa Elimu Maskini ya Mungu aliishia kusoma mambo ya sera ya Elimu Na Miongozo ya kazi Kuwa Shule lazima iwe na Maabara Na Darasa Moja wanafunzi 40

Alisahau Kuwa 'Siasa' Ni zaid ya Taaluma, Miongozo Sijui sera

Pole Afisa Elimu uliesimamishwa

Pole Sana Tena Sana Afisa Elimu utakaekaimu
Maana usipofuata vigezo vya kitaaluma Matokeo yakija ya hovyo Pia wanakuibukia kwa kushindwa kwenda na 'Kasi yetu'

Ugali moto,mboga Moto, maji Moto
 
Ni vema kujua na kutambua kuwa sii kila mahali Sheria ina apply. Ni kweli Darasa 1 linapaswa kuwa na watoto 40 maximum, ila pale ambapo Hakuna alternative, hupaswi kuzuia wanafunzi zaidi ya idadi hiyo,kufanya hivyo Ni kukiuka misingi ya Katiba inayompa mtoto Haki ya Elimu. Tusiwe Maroboti, tunasoma na kuelimika ili kutatua changamoto katika Jamii!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni vema kujua na kutambua kuwa sii kila mahali Sheria ina apply. Ni kweli Darasa 1 linapaswa kuwa na watoto 40 maximum, ila pale ambapo Hakuna alternative, hupaswi kuzuia wanafunzi zaidi ya idadi hiyo,kufanya hivyo Ni kukiuka misingi ya Katiba inayompa mtoto Haki ya Elimu. Tusiwe Maroboti, tunasoma na kuelimika ili kutatua changamoto katika Jamii!

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama ni hivyo, nadhani viongozi walitakiwa kulitolea hili suala muongozo wa maandishi kwa kumpa amri Afisa Elimu awachukue wanafunzi hivyo hivyo licha ya ufinyu wa nafasi. Suala ka kumsimamisha kwa kisa amefuata taratibu na miongozi sioni kama lina afya sana ki haki na kitaaluma

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo REO afanye kama RPC wa hapo aliye tenguliwa na Lugola na akampuuza na kuendelea kuchapa mzigo
 
Back
Top Bottom